Wana UKAWA tunamhitaji Prof. Lipumba lasivyo patachimbika

Wana UKAWA tunamhitaji Prof. Lipumba lasivyo patachimbika

Wana Jf wasalaam!
Likiwa joto la uchaguzi limeanza kupanda lakini kwa upande wa UKAWA bado wana mtihani mkubwa sana kumchagua atakaye wawakilisha kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Wana UKAWA wengi wamekuwa wakipendelea Mh prof .Lipumba apeperushe bendera ya UKAWA kwani kwa sasa ana mvuto ndani na nje ya UKAWA kuliko Dr Slaa ambaye anaonekana kulazimisha lazima agombee!

Wana Jf mwezi December nilipata nafasi ya kukaa na vijana kama kumi pale Tengeru na tulibadilishana mawazo kuhusu siasa za Tanzania na wengi walijikita kujadili nani anafaa kugombea Urais kati ya Lipumba na Slaa hapa ndio ubishi ulipo anza na wengi walitaka Slaa apumzike wakisema Lipumba ndio anaye faa kipindi hiki kama wanataka kuchukua nchi na atawasaidia kufuta zile propaganda za udini.

Lakini wengine walishikilia msimamo kuwa hata kielimu Lipumba anamzidi Slaa kwani Slaa hana Elimu yeyote zaidi ya kusomea dini na Ikulu hatupeleki kiongozi wa dini kwakweli kwenye hili walibishana sana wengi wakisema Elimu ya Slaa haitambuliki kimataifa na si mtaalam wa jambo lolote.
Kuna mwingine aliendelea kusema kuwa Slaa hafai kugombea Urais maana amekuwa akichochea migogoro ndani ya chama chake na kuwagawa wanachama kwenye makundi!

Wengi walikuwa wana sisitiza kuwa patachimbika kama Lipumba hatopitishwa na hakutakuwa na maelewano kwenye hilo na wakasema Lipumba asipopitishwa kura zao watampa mgombea wa CCM kama walivyo fanya 2010!

Wana Jf joto la uchaguzi liliendelea nilipo pata safari ya kwenda Tanga nilipita mtaa fulani pale Tanga mjini na hapo nilikuta wakijadili siasa kwa upana na wengi walionekana kuunga mkono UKAWA na walikuwa wanasema wana furahishwa na mwenendo wa UKAWA lakini wana kerwa nakampeni za chinichini zinazo fanywa ili kumpitisha Slaa kugombea Urais.. na wengi walikuwa wakiongea kwa jaziba huku wakisisitiza kuwa mipango ya kumpitisha Slaa kugombea Urais hazito kubalika na patachimbika kabisa siku hiyo na hawatoburuzwa na mtu...
Kuna kijana mmoja alisema kuwa wao kama UKAWA wana mhitaji Lipumba lasivyo patachimbika ..maana wanaona dalili za mizengwe! Pia alisema ana kerwa na baadhi ya viongozi wao kuwatuma vijana wao kwenye mitandao ili wawapambe na kuwapigia campaign wakati muda bado....na aliendelea kusisitiza kuwa "kama chadema wanataka kuwajua CUF ngangari kwa vitendo wajaribu mizengwe".

Kwakweli wana Tanga walionekana wenye imani kubwa na Lipumba na walisisitiza kuwa ni wakati sasa Mchumi huyo kuiongoza nchi hii!

Karibuni wana jamvi!

aliye kutuma kueneza hii kitu mwambie hatudanganyiki na upumbavu huu. sawa we kilaza?
 
Heshima ikurudie nawe pia Mkuu. Wapumbavu sana hawa Mkuu, ya kwao yanawashinda sasa wameamua kufanya uchochezi dhidi ya UKAWA ili kuleta vurugu palipo na mshikamano mkubwa.

heshima yako mkuu hawa wahuni wa ccm wameshindwa kumpata mgombea wao wa ccm wamekuja UKAWA hii inaonyesha kiasi gani ccm inakaribia kuanguka.
 
Waitu kulikoni tena huko lumumba.... mbona mwaweweseka? Subirini oktoba tu....
wakola waitu!!!
 
Nyie tunawajua mnaogopa nguvu ya Dr slaa nani kawaambia ni mzee nenda zako
Na malipo yako kiduchu hayo mtakoma mwaka huu andaeni makazi ya kujificha maana ni lazima
mjiharishie

Kwani Slaa ni mgombea kupitia Ukawa?
 
Eheeee!! Leo wewe Lumumba unataka kuwa ukawa? Dunia hii haitaisha vituko!! Leo umewakimbia Chabruma,Lizaboni,Simiyu Yetu,Ritz, Aminalango,Gsam, Musalani kuja hapa kutoa pumba zako?

Haya ni maoni ya wana UKAWA wengi wana mhuhitaji Lipumba!
 
Wakuu Pamoja Kuwa Mimi Ni Mwanachama Mtiifu Wa CHADEMA Mwenye Dhamira Ya Kweli Ya Kuikomboa Nchi Hii Lakini Simwoni Dr Slaa Kama Mkombozi Wa Kweli Nchi Yetu Ina Ugonjwa Wa Uchumi Ulosababishwa Na Virus Aina Ya Ulafiwaviongozi Na Tiba Halili Ya Virus Hivi Ni Prof Wa Uchumi Alobobea Duniani Prof. Lipumba Cdm Tuachane Na Dhana Kuwa Sisi Ni Bora Kuliko Wapinzani Wote Bali Tuangalie Alie Bora Kwa Watanzania Wote
 
Wakuu Pamoja Kuwa Mimi Ni Mwanachama Mtiifu Wa CHADEMA Mwenye Dhamira Ya Kweli Ya Kuikomboa Nchi Hii Lakini Simwoni Dr Slaa Kama Mkombozi Wa Kweli Nchi Yetu Ina Ugonjwa Wa Uchumi Ulosababishwa Na Virus Aina Ya Ulafiwaviongozi Na Tiba Halili Ya Virus Hivi Ni Prof Wa Uchumi Alobobea Duniani Prof. Lipumba Cdm Tuachane Na Dhana Kuwa Sisi Ni Bora Kuliko Wapinzani Wote Bali Tuangalie Alie Bora Kwa Watanzania Wote
Worse propagandist ever, you should go back to the class to learn how to be a good propagandist. Today you've failed miserably!
 
Historia ya mleta mada jf ni mtetezi na pro ccm.

Hizi kampeni mnazopiga mwisho wa siku ccm mtavurugwa na nyumba isowahusu.

Nyumba yenu muinusuru kwani mnavurugana ,usiingilie kwa jirani.

Kocha ya yanga katu haipangii simba aina ya wachezaji ktk mechi ya Mtani Jembe
 
Upumbavu nao ni sifa kwa baadhi ya watu, miongoni mwao ndiyo ninyi. Kwa kuwa Slaa hana mvuto, ombeeni UKAWA imteue Slaa ili CCM iweze kushinda kwa kishindo.

huyu babu silaa nani atampa, mropokaji, tunahitaji watu wenye maauzi magumu wasio wakukurupuka,
 
Kulonga mbali, kutekeleza na kusimamia mbali!
 
wewe usituvuruge.. pia usituvurugie ukawa yetu. utuache mda ukifika wenye kadi tutapiga kura kumchagua mgombea wa ukawa. lipumba kutogombea uraisi au kutosimamishwa kt post ya uraisi haina maana kuwa hatokuwa kt serikali ya ukawa inshalla ukawa wakishinda.

ivyo uwe mpole usituvuruge. 2tapiga kura kumpata atakaye simamishwa na ukawa na anayekubalika pande zote. na we are very serious kt hili.. usilete uZushi wako wa lumumba
 
Kuhusu elimu isiyotambulika na kwamba ni yakidini(Catholic), hapo umechapia pakubwa.

Unapaswa kufahamu jambo hili, "ELIMU WANAYOIPATA MAPADRI NI MARADUFU UKILINGANISHA NA ELIMU TUNAYOISOMEA KWENYE NORAMAL UNIVERSITIES""

Katika suala la elimu, hata kama Lipumba atakuwa na degree milioni za uchumi; bado kwa elimu aliyonayo SLAA, yupo juu ya Lipumba. Tena mbali mno.

Mengineyo niwakaribishe wadau waendelee kuchambua.

Naomba fafanua mkuu hiyo elimu gani ambayo hata mtu akiwa na degree kumi haifikii???
 
Lipumba ni msomi na ni mchumi aliebobea, ndio mgombea pekee anaefaa Ukawa, Slaa ni padri Tanzania haina dini
 
Watakutukana sana umegusa sehemu ambayo huwa hawataki iguswe japo kwa kuangalia upeo wa mambo lipumba anaweza kuwa wa msaada zaidi kuliko slaa kwanza lipumba hana kisilani kama mzee slaa hata busara za lipumba ziko angalau kuliko dr slaa.
 
Lipumba akipitishwa kugombea urais ccm itapata wakati mgumu sana.
 
Historia ya mleta mada jf ni mtetezi na pro ccm.

Hizi kampeni mnazopiga mwisho wa siku ccm mtavurugwa na nyumba isowahusu.

Nyumba yenu muinusuru kwani mnavurugana ,usiingilie kwa jirani.

Kocha ya yanga katu haipangii simba aina ya wachezaji ktk mechi ya Mtani Jembe
Tupia michango yake na mada zake kuthibitisha maneno yako lakini bila uthibitisho unaweza kuitwa mmbea.
 
Wakuu Pamoja Kuwa Mimi Ni Mwanachama Mtiifu Wa CHADEMA Mwenye Dhamira Ya Kweli Ya Kuikomboa Nchi Hii Lakini Simwoni Dr Slaa Kama Mkombozi Wa Kweli Nchi Yetu Ina Ugonjwa Wa Uchumi Ulosababishwa Na Virus Aina Ya Ulafiwaviongozi Na Tiba Halili Ya Virus Hivi Ni Prof Wa Uchumi Alobobea Duniani Prof. Lipumba Cdm Tuachane Na Dhana Kuwa Sisi Ni Bora Kuliko Wapinzani Wote Bali Tuangalie Alie Bora Kwa Watanzania Wote

Hijja Madava Kama huyo SLAA sio Mkombozi kwako na wewe ni CHADEMA ni kwanini anapata kura nyingi zaidi ya huyo LIPUMBA?
Kuongoza nchi sio lazima uwe na VYETI VYA UCHUMI angalia KAGAME anavyoiendesha RWANDA vizuri...

LIPUMBA Amegombea Urais toka 1995.... kwahiyo ametoa sera zake na Wananchi hawazioni kuwa zinafaa...

Alikuwa Mchumi wa RAIS Mwinyi - Ndio hapo tulianza kuwa na MATABAKA ya MATAJIRI na MASIKINI... kuwa MaKUBWA
 
Back
Top Bottom