Wana MMU tushirikiane kuboresha Jukwaa letu

Wana MMU tushirikiane kuboresha Jukwaa letu

Status
Not open for further replies.
Idea ya kufutilia mbali thread zisizofaa hapa MMU naiunga mkono...

Laiti ningekuwa na muda...mngeona kazi ya Babu mnoko....

Kama hakuna mada ya maana, watuache tufanya reference kwenye thread zilizowahi kutuweka macho hadi jogoo wanaamka!!

Babu DC!!

mzee mwenzangu kazi ushapata tena unakuwa babu kifimbo cheza....... enzi zile unasoma page ya 1 hadi mwisho bila kukosa kwa mapoint uwakute Mbu na soulmate wake MwanajamiiOne hutoki kwenye mada salam zimfike Lizzy
 
Last edited by a moderator:
MC Umeongea vitu muhimu sana ktk kuboresha hili jukwaa!
Thanks!
Lakini umeegemea sana, sana, sana kuwatetea memba wakongwe!!!! Ni kweli memba wapya hujisahau sana! Ila memba wakongwe wanaongoza kwa kuchati!!!!!
Vile vile, wanadharau ya hali juu! Ngoja nikupe mfano hapa! Unamkuta kwa vile yeye kajiunga mapema, bila shaka ameshaona mada nyingi zikijadiliwa, hivyo basi akikuta mada yenye content kama ile, badala ya kutoa mchango unaufaa (hata kueka link) yeye anakejeli na kujiona anajua kila kitu! This is not fair!!!!!!!
...
Kitu kingine hawataki kukosolewa!
...
Jaman! Tukijadili, tuangalie pande zote!!!!
Hivi wanafunzi wa 0, A level na wanachuo hawapaswi kujiunga?????????
Mbona mi nahisi matatizo mengi ya mahusiano huwakumba hao?!
...
Jengine, sikubaliani na wote waanzishaji mada za ki.puuzi!
Vile vile sikubaliani na wanaochangia ki.puuzi na hasira kali! Ngoja nifafanue hapa!
Mfano mtu anaanzisha threed anaulizia ni mkoa gani unawarembo ili akaoe! Huu ni upuu.zi! Lakini huyu matusi hayatomuelimisha! Na ukitoa matusi mi nahisi na wewe ni Mpuu.zi hata kama umejianga mwanzo!!!
...
All in all, UJUMBE UMETUFIKA!
 
jamani nasisitiza tena tuseme hao wanaokosea wanakosea wapi na majina yao ili tujijue tunajirekebishaje. lol
 
Mentions zote..na hadi sasa nafuatilia mwanzo mwisho......sitaki kumiss a thing.......

Mr Rocky akishindwa kumfikishia ujumbe Hamisi hiyo kazi waweza kunipa mimi!!!!!

hahahha, kumbe na wewe unamjua hamisi, basi naomba ufikishe ujumbe. sio hapa lakini. hii thread nimeipenda kweli, leo sibanduki hapa.
 
Ahsante sana Mkuu Rocky katika jitihada zako za kulirudisha jukwa hili na kwa maoni yangu JF yote katika hali ambayo ilipendwa na kukubaliwa na wanachama wengi wa miaka ya nyuma. Pia shukrani zangu kwa wote waliochangia mawazo yao katika kumuwezesha Mkuu Rocky kuandika uzi huu kwa kina. Tuhakikishe hili jukwaa haliharibiwi na wachache kwa kisingizio kwamba JF imekuwa kubwa mno miaka ya karibuni pamoja na ukuaji huo wa JF na kufikia karibu wanachama 160,000 lakini bado tunaweza kuhakikisha jukwaa linakuwa na sifa nzuri iliyokuwepo miaka ya nyuma.

BAK nashukuru sana mkuu na wewe ni mmoja wapo wa watu walionitia moyo kufanya haya na kufikia kuandika haya na bila mchango wako wa mawazo tusingekuwa hapa
Naamini tutaendelea kushirikishana mengi katika kuweka mambo sawa na kila mmoja aelewe kuwa hakuna thread inayomlenga personally hii ni kwa wote hata mimi naweza kuwa nimeanzisha thread ambayo haikuwa na tija ila muhimu ni kujua ni waopi tuliteleza na tusije tena tukateleza eneo hilo hilo moja na kuangalia mbele kuna nini na ni nini la kufanya kufikia pale tunapopataka
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Kipaji Halisi ndo manake kupitia key board anafanya hayo kwani hawezi kupatikana mkuu
kupitia keyboard unjuaje kuwa huyu "demu mkali"..BTW tuache hayo mie sio mpnz sana wa hili jukwaa..niko hapa kujifunza..ila umeongea ukweli humu MMU siku hizi sio..pamoja na ugeni wng..ila mada zingine hazina mashiko...
 
nimekumiss pia mr rocky!ila mimi naomba mnivumile maana siwezi kuguarantee kuwa nitabadilika.

Mfano halisi ndio huu: "Mmeanza kuchakachua ninyi haohao "thread" yenu...mmemisiana eti?" LOL...
 
Kuna watu wanaangalia mambo objectively. Lakini pia wapo baadhi ambao wanaangalia mambo subjectively. Wanaamni kuwa kila wanachokifanya basi kinafanywa na kila mtu au kinatakiwa kufanywa au kuaminiwa na kila mtu.

Pia wapo baadhi ya watu wengine wana closed minds. Wanaamini wanachokiamini and they are not prepared to even listen to the other side of the coin.

At the same time kuna baadhi ya watu ambao they can't tolerate. They are not prepared to allow the existence, occurrence, or practice of something that one does not necessarily like or agree with without any interference.

Then kuna baadhi ya watu ambao probably ni attention seeker. Hawa watu wana-seek attention kutoka kwa watu wengine as a form of feedback. Hili siyo tatizo lakini linakuwa tatizo kwa both parties kama hii tabia inakuwa too excessive and inappropriate. Wenyewe wanaita "attention seeking disorder".

Nikiongezea kwa upande wa Wabongo tunapenda sana kujadili mada za kiudaku udaku. We really love this. Tukisikia or kuona kitu in private, we can't keep our months shut. But wapo wachache ambao they don't like this.

Kwa hiyo, unapoweka watu hawa wote kwenye kapu moja lazima kutatokota tuu. Hata hivyo, naamini kuwa watu wa aina hii hawapatikani kwenye social media tuu. Wanapatikana pia mitaani. Tunaishi nao kila siku. Wengine ni ndugu zetu, majirani na marafiki zetu. It is just how we handle them.
EMT nakubaliana na wewe kabisa
Ila katika safari ya kwenda kwenye mema ni lazima tugombane na kubishana humu kati na lazima kutokee mtu atakayekuambia hii njia sio na wengine watakosoa hata utembeaji wako na mwendo wako ila lengo lao wote hao ni kufika mwisho wa safari bila kujali kuna nini njiani
Watu wote uliowataja wapo na hatuwezi kuwaepuka na wala huwezi ukawaondoa na kuwatupa nje kisa wanaleta vitu ambayo wewe na mimi na yule hawakubaliani navyo ila je tuwaache njiani
No njia sio kuwaacha na kuwa nao kwenye kundi na kujaribu kuwaleta kwenye mwanga waone kuwa yale wanayoyafanya yanachelewesha safari na hatutafika
 
Last edited by a moderator:
Mashaxizo asante sana kwa ujumbe wako
Hakuna mkongwe zaidi ya mwenzake ndani ya MMU ni kama umeingia darasani na unataka kuanza degree yako ya kwanza au ya pili na wakati huo huo tayari una degree nyingine ya kitu tofauti huwezi ukasema wewe ni mkongwe kwenye elimu ila na wewe unatakiwa ujifunze mapya na upate kipya kutoka kwa wenzako
Humu ni kisima cha kuchota elimu na busara na maarifa kwa kila mtu hakuna ambaye ni mtaalam zaidi ya mwenzake ila wote tnaenda sawa katika kupata kitu kipya na cha maana
Asante sana kwa mchango wako mkuu
 
Last edited by a moderator:
kupitia keyboard unjuaje kuwa huyu "demu mkali"..BTW tuache hayo mie sio mpnz sana wa hili jukwaa..niko hapa kujifunza..ila umeongea ukweli humu MMU siku hizi sio..pamoja na ugeni wng..ila mada zingine hazina mashiko...

Mkuu Kipaji Halisi hayo yaache kama yalivyo maana wanasema ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
mzee mwenzangu kazi ushapata tena unakuwa babu kifimbo cheza....... enzi zile unasoma page ya 1 hadi mwisho bila kukosa kwa mapoint uwakute Mbu na soulmate wake MwanajamiiOne hutoki kwenye mada salam zimfike Lizzy
Blaki Womani umenikumbusha Mbu sijui kapotelea wapi yule mtu siku hizi na Lizzy na MwanajamiiOne hao watu walikuwa balaa kwa mada moto moto unasoma comments mpaka unajiuliza dah sasa hapa nichangie nini
 
Last edited by a moderator:
jamani nasisitiza tena tuseme hao wanaokosea wanakosea wapi na majina yao ili tujijue tunajirekebishaje. lol

Hapa tutakua tunakosea. Siyo suala la kusema nani anakosea wapi... Mie kwa haraka haraka naona kama wote ni wakosefu.

1. Mtu unapo ona kabisa mada haifai unaiacha badala ya kui report hilo ni kosa. Ikiwa kila mmoja anaye ona mada haifai aka report na mods wakaona kabisa mada haifai then ina maana mada nyingi (hasa za kitoto zitatolewa).

Kuna vi mada titles zinakuja kama vile;

- Nimelala na kidenti.
-Namtamani housegal wangu.
- Ukubwa ama udogo wa Vikojoleo.
- Naweza sana game.

Ni mada ambazo kweli zipo katika jamii, hivyo zikiletwa kwa lengo la kuelimisha, na hoja kujengwa walau basi zitahamishiwa Jukwaa la Wakubwa. Ubaya ni kuwa nyingi ni kuhamisisha ngono... Inakuwa kana kwamba MMU ni ambassodor wa ngono. Haipendezi.

2. Kuna pia wimbi kubwa la watu kujiunga, si wote watoto, ila wengi tokana na mada zao unaona kabisa hii ni under 18. Hat msomaji ukisoma unaona aibu. Hili kundi wamekuwa wengi na wanakuwa kwa kasi. Kuachwa kwa mada isiyo msingi inamhamasisha kurusha nyingine kwa kuona ni sawa tu.

Suala la misimamo ya watu.... Huwezi kuibadilisha bali kwa hoja na kama umeweza kum convince yeye kusimamia kila unacho amini ama vice versa ndiyo matokeo ya mijadala.
 
mimi niweje sasa, kama tunataka kurekebishana tutajane humu kila mtu aambiwe anakosea wapi, wapi abadilike wapi ajiboreshe. karibuni

Heheh
Zamani kulikuwaga na kale ka mtindo ka kuchakachua threads zisizokuwa na muelekeo . . .
Sijui kaalishia wapi!
 
AshaDii umeongea na naomba nimwambie tena Husninyo hatuna nia ya kumtaja mtu wala kutaja thread ambazo zinaonekana kabisa hazina mshiko ila mwenye uelewa ataelewa tunamaanisha nini tunapoongea haya na sio kwa faida yang au yako ila kwa faida ya wote ambao ni member wa hili jukwaa na jukwaa jingine lolote.
Nia haswa ni kujua kuwa tunaingia hmu kufundishana na kupata uelewa wa mambo mengi na kujua hata kama niko mtaani ni wapi nimeenda wrong na wapi nirekebishe sio kwenda tuu kama kuku aliyekatwa kichwa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo ni kujichanganya watu wazima na watoto! Hata vilinge vya wakubwa vikishindwa kuwafukuza watoto vinaharibikiwa.
 
Heheh
Zamani kulikuwaga na kale ka mtindo ka kuchakachua threads zisizokuwa na muelekeo . . .
Sijui kaalishia wapi!
Avemaria ukichakachua thread ya mtu bado unaongeza comments kwenye thread yake na hapo ndo unaikuta iko page ya 10 kutokana na watu wataacha kuchangia mada wataanza kuchangia ule uchakachuzi
 
Last edited by a moderator:
Umepotelea wapi shostito ?
upo sahihi kabisa mr rocky kasi ya kumis-use hili jukwaa inaongezeka kwa kasi,utoto,kejeli,kuchambana,matusi vimekuwa kawaida wakati hapo awali havikuwa na nafasi,pamoja na kureport mi naona hamna haja ya kuchangia sredi zisizokuwa na mantiki unapotezeaa tu
 
Hapa tutakua tunakosea. Siyo suala la kusema nani anakosea wapi... Mie kwa haraka haraka naona kama wote ni wakosefu.

1. Mtu unapo ona kabisa mada haifai unaiacha badala ya kui report hilo ni kosa. Ikiwa kila mmoja anaye ona mada haifai aka report na mods wakaona kabisa mada haifai then ina maana mada nyingi (hasa za kitoto zitatolewa).

Kuna vi mada titles zinakuja kama vile;

- Nimelala na kidenti.
-Namtamani housegal wangu.
- Ukubwa ama udogo wa Vikojoleo.
- Naweza sana game.

Ni mada ambazo kweli zipo katika jamii, hivyo zikiletwa kwa lengo la kuelimisha, na hoja kujengwa walau basi zitahamishiwa Jukwaa la Wakubwa. Ubaya ni kuwa nyingi ni kuhamisisha ngono... Inakuwa kana kwamba MMU ni ambassodor wa ngono. Haipendezi.

2. Kuna pia wimbi kubwa la watu kujiunga, si wote watoto, ila wengi tokana na mada zao unaona kabisa hii ni under 18. Hat msomaji ukisoma unaona aibu. Hili kundi wamekuwa wengi na wanakuwa kwa kasi. Kuachwa kwa mada isiyo msingi inamhamasisha kurusha nyingine kwa kuona ni sawa tu.

Suala la misimamo ya watu.... Huwezi kuibadilisha bali kwa hoja na kama umeweza kum convince yeye kusimamia kila unacho amini ama vice versa ndiyo matokeo ya mijadala.

ila mi nasema aunt msiseme ni under 18. kuna watu wazima humu ila akili za kitoto na wapo watoto wamekomaa akili. best optn ni kuwaelimisha tu badala ya kuwashambulia hao. halafu nimekumiss kiukweli ukweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom