Nadhani ni changamoto za kukua na kupanuka kwa Jukwaa kama matokeo kupanuka kwa teknolojia.....
Leo hii kila mtu unayekutana naye mwenye simu yenye windo au android utamkuta ana shortcut ya app ya JF na hata ukimkuta ambaye hana ukimuwekea kesho anakupigia simu ya kukushukuru kwa kumuunganisha na JF.
Baya kuliko lote ni wakongwe kulikimbia jukwaa na japo napo huwezi kuwalaumu maana hali ya majukumu inabadilika, nakumbuka wakati najiunga JF nilikuwa nina ajira ya kuunga-unga tu wala majukumu hayakuwa tait sana ila leo hii vitu ni tofauti sana, hata ukipata mda kama huu ni majaaliwa sana.
Hivyo ukiangalia hivi vitu vinakuwa-complicated sana.
Mambo katika hii dunia yametengenezwa kuwa unfair kwenye maeneo mengi, mfano kwenye music tunasema "old is gold' na hata hapa JF tunaambiwa "enzi hizo" JF ilikuwa tamu zaidi wengi wanakumbuka "good old days".....
Ila ndio hivyo hatuwezi kuzirudisha hizo siku japo kwa kuelekezana kama hivi inapendeza sana na nadhani kila siku tuna nafasi ya kufanya kitu kizuri zaidi na cha kukumbukwa.
Inawezekana, kila mtu achukue nafasi yake!
Ahsante
AshaDii kwa kuniita, maana bila hivyo ningepitwa na uzi mzuri namna hii.