Wana JF tumsaidie kijana huyu!

Status
Not open for further replies.
Samahani wakuu

naomba nichukue muda wenu kidogo kuwashukuru kwa kazi nzito mnayofanya na kuwapa pole .. Dhumuni ya kuandika hii thread
ni kuhusiana na thread iliyofunguliwa na mwanajamvi mwenzetu VIKWAZO.. (saidia Mtanzia mwenzetu anateseka) weli wengi tumeisoma na imetugusa sana na kuna wanajamvi ambao tuko tayari kujitolea kidogo tulicho nacho. Ila tatizo hakuna wakukusaya.

Waheshimiwa tungeomba sana muda wenu kidogo mtu tekelezee hili ( Kukusanya hizo fedha) Hata kama hazitatosha kwa hospitali lakini zitamsaidia kwa sukari ..... Inapendeza sana kuona wana JF tunajitolea kwa moyo na kumsaidia Mtanzania mwenzetu.. anaye taka kujionea na kusoma link hii hapa..

https://www.jamiiforums.com/habari-...mtanzania-mwenzetu-anateseka.html#post2209158

Asanteeni sana wakuu Tunaomba sana tena sana Na samahani kwa usumbufu...

Kwa watakao penda kuchangia directly Iko kwenye article ya gazeti la mwananchi :
Anayetaka kumsaidia awasiliane kwa namba 0786272409 au 0655304336

Article yenyewe hii hapa
http://www.mwananchi.co.tz/makala/-/...aidieni-jamani.

UPDATE:
- Kijana amefikishwa KCMC asubuhi hii kwa msaada mkubwa wa Mhe. Hood wa Mogorogoro ambaye amejitolea kugharimia mitibabu.
- Hadi hivi sasa haijajulikana bado gharama zote za matibabu zikuwa ni kiasi gani na kama matibabu hayo yanaweza kufanyika hapa nchini au la
- Familia ya Abbas ni maskini kwa maana ya neo "maskini" na hivyo pamoja gharama hizo bado kutakuwa na mzigo mkubwa kwa familia.
- Kampuni ya Mwananchi ambao wamekuwa wakicoordinate suala hili wanafanya mpango wa kuweza kufundua Abdallah Abbas Medical Fund ya kusaidia gharama za matibabu na nyingine kwa familia. Endapo litafanikiwa hili mapema leo au siku chache zijazo itakuwa ni njia rahisi ya kuweza kuchangia kutoka sehemu yoyote duniani.

Asante kwa update nawasiliana na hizo namba niweze kutupia chochote
 
wakuu toeni chochote, hela ya bia na vinywaji wiki end moja inaweza kuokoa maisha ya mtu
 
Tunashukuru sana AD ngoja nicheki through those numbers hapo ili niweze kuona naweza kusaidiaje. Once again thanks
 
Maxence atapokea michango yote ya wana Jamii Forum
Na ata toa report baada ya kupokea michango ...

ataweka details zake juu ya hii thread muda si mrefu

Asanteeni..
 
AD Tuko pamoja kwa hali na mali kumsaidia huyu kijana mwenzetu, mwenyezi mungu atuepushe na maradhi na mabala,
 
Nikweli mkuu, soon na submit mchango wangu, vp wewe umeshapiga hizo namba?

long time mkuu niko katika siko tanzania kwa sana ila mjumbe wangu nimesha mtuma naye kaisha nijulisha kwamba analikamilisha ilo hiyo by leo naona ajanirudia lakini naamini ilimekamilika
 
Mhhhhh! AD ahsante sana kwa moyo wako wa huruma katika kumsaidia huyu mwenzetu. Mungu akubariki sana kwa kuanzisha uzi huu muhimu sana. Pia ahsante sana kwa kunishtua, kusema kweli nilikuwa sijauona uzi huu maana JF siku hizi imekuwa kubwa sana.
 
Nimechelewa sana kuiona hii post.
Asante sana AD kwa kutukumbusha.
Nimeona mtu wa mwisho kutoa maoni yake hapa ni Mamengazi tarehe 14/7. Kimekuwa kikiendelea nini? Kumeanzishwa thread mpya sijaiona? Mwitikio wa watu kuchangia uko vipi?
AD alisema:
"Maxence atapokea michango yote ya wana Jamii Forum. Na ata toa report baada ya kupokea michango ...ataweka details zake juu ya hii thread muda si mrefu"
Ziko wapi hizo details?
Naomba tuelezwe zaidi na kinachoendelea. Vyenginevyo itaonesha kuwa hisia za huruma zetu tulizoeleza na ahadi tulizotoa zimeishia midomoni mwetu. Wana JF, kutoa kwataka moyo, si utajiri. Naamini tunaweza kuwaonesha wanasiasa na matajiri wa nchi hii kuwa "sisi tunaweza, kwa sababu tuko kitu kimoja, kwa sababu tunajali".
Ninaomba kuwe na uwazi katika hili, hizo details ya kinachopatikana ziwekwe kila siku, vyenginevyo wengine wanaweza kuvunjika moyo na kurudi nyuma. Vile vile ieleweke kuwa wana JF wengine wako nje ya TZ, kumeandaliwa mpango gani wa wao kuchangia? Kama upo waelezwe, kama haupo uandaliwe.
Wana JF, tuoneshe kuwa sisi ni wanafamilia wa kweli.
 
I updated the 1st post.

Walochangia specifically kwa ajili ya kijana huyu ni wawili tu, wengine michango ilikuja ajili ya JF lakini kwa uhitaji uliopo imeingizwa kwenye makusanyo ya kumsaidia Abdallah.
 
I updated the 1st post.

Walochangia specifically kwa ajili ya kijana huyu ni wawili tu, wengine michango ilikuja ajili ya JF lakini kwa uhitaji uliopo imeingizwa kwenye makusanyo ya kumsaidia Abdallah.
Makusanyo hayo yatapelekwa kwenye account au kunautaratibu umepangwa tofauti na kuweka banki? Sababu ya kuuliza hili kuna mahitaji muhimu kama chakula kwa mgonjwa na anayemhudumia ambavyo vinatakiwa kwa haraka
 
Makusanyo hayo yatapelekwa kwenye account au kunautaratibu umepangwa tofauti na kuweka banki? Sababu ya kuuliza hili kuna mahitaji muhimu kama chakula kwa mgonjwa na anayemhudumia ambavyo vinatakiwa kwa haraka
Naweza kuongea nawe kwa simu please? I will appreciate BW, kuna jukumu nataka ukabidhiwe kwa haraka ili niweze kuandika hapa
 
Status
Not open for further replies.
39 Reactions
Reply
Back
Top Bottom