Wana JF, niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba baraka zenu & moral support yenu jambo langu hili liwe! Mniombee Mungu asaidie, awezeshe liwe!

Mkuu, hizo nafasi zinahitaji uwe mtu wa aina flani hivi.

Yaani uwe mtoto wa kigogo.

Huko ndiko wanakofichana wenye nchi.
Ndio maana siku zote tunaomba Karma itende maana this is too much !! Na hawatapata peace of mind katika maisha yao pamoja na kujilimbikizia mali nyingi katika hii dunia !! Mungu ni fundi sana !!!
 
Kaka Pascal kama JF humu tushasema umepita. Ila kupingwa na kwa ccm hii ya comrade Kinana hakika unafaa kabisa ila.usije ukageuka Kimbisa amehudumu ubunge huko miongo kadhaa bila kupisha kijiti.

Huwa namuona yule mkewe somebody mjema na Eange rover nyeupe ina namba za Diplomatic East Africa miaka nenda rudi . Kula miaka 10 pumzika waachie wengine.
 
Shida ni nini kaka Mathewson? Ila kiuwezo si unaona anaweza?
Mkuu

Anamuweza nani?

Anaweza kazi zake zinazomuhusu yeye binafsi,sisi hatuhusiki,even kupiga kura sio sisi!

Hiyo ni his own problem ajifunze kutatua matatizo yake binafsi ya kupenda madaraka

Kama ni kura awafate wahusika,kama ni bajeti atafute hela zake au akakope benki,etc

Sio anahamisha uchu wake wa kupenda uongozi kwetu sie tusiohusika

Haya ni makelele yake tu ya kuhamisha mavitu yaliyojaa ubongoni mwake kwa wengine apate chochote....

Fvck him!
 
Mkuu

Anamuweza nani?

Anaweza kazi zake zinazomuhusu yeye binafsi,sisi hatuhusiki,even kupiga kura sio sisi!

Hiyo ni his own problem ajifunze kutatua matatizo yake binafsi ya kupenda madaraka

Kama ni kura awafate wahusika,kama ni bajeti atafute hela zake au akakope benki,etc

Sio anahamisha uchu wake wa kupenda uongozi kwetu sie tusiohusika

Haya ni makelele yake tu ya kuhamisha mavitu yaliyojaa ubongoni mwake kwa wengine apate chochote....

Fvck him!
Umeongea ukweli japo mkali. Ila katika hili bro huoni kama ni vizuri tumuunge mkono hata kwa 'will' tu?
 
Wana JF wenzangu,
Kuna msemo usemao "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu", "Vox Populi is Vox Dei"

Hili ni Bandiko la kukusanya sauti za wengi ili iwe ni sauti ya Mungu. Mimi mwana jf mwenzenu Pascal Mayalla, nina jambo langu ambalo mimi kama mimi peke yangu kama Pascal Mayalla peke yangu na familia yangu tuu, na ndugu zangu tuu, na jamaa zangu tuu na rafiki zangu tuu, pekee, hatuwezi, hivyo naomba kuwashirikisha wana jf ili hili jambo langu, lisiwe ni jambo langu tuu, bali liwe ni jambo letu, umoja ni nguvu, together we can.

Pasikali, sio tuu ni mwenzenu, humu jf, bali mimi ni ndugu yenu. Baadhi tuko humu pamoja toka ile 2006, jf ikiitwa Jambo Forums hivyo ni zaidi ya miaka 15 pamoja!. sasa. Kuna watu tunafahamiana kupitia jf, kuna watu tumesaidiana kupitia jf, na wengine hadi kutembeleana home na kushirikiana kwenye shida na raha na kuna misiba ya wana jf, we drive all the way hundreds of kilometers just to bid farewell to a jf member!.

Enzi zile najiunga jf nilikuwa kijana shababi, kuna mikoa ya baridi, nilikuwa nikitua tuu na kupost kitu chochote, kutoka mkoa huo, pm zitaingia kuniulizia niko nimefikia wapi na hadi blangeti la kuzuia baridi napata kutoka kwa mwana JF!, what a love!.

JF is Like Home to Me, It's More Than A Friend, It's A Family. Nalala jf, naamka jf, nashinda jf, jf is everything!, its a big family, tukianza kuji consolidate na kutumia a consolidated powers ya nguvu yetu ya ushawishi as a pressure group, we can do wonders!. Hii togetherness yetu lets start using it as one, Kwanza Kwa kusahau tofauti zetu za kisiasa na vyama vyetu, tuka supportiana as one, tuka stand together as one kwa jambo letu, ile powers ya pamoja ndio the magic behind!,tutatusua!.

Msione watu wanakusanya the multitude of people nje kwao for a whole day na jioni baada tuu ya kuzama jua, kuwagawia Ten Ten,kuwalisha au kuwafuturisha!.

Au matajiri wanashindana kudhamini timu za mpira za Simba na Yanga, spending billions!. Go find out wafanyakazi wa viwandani kwa matajiri hao wanalipwa shilingi ngapi!, unaweza usiamini, it's not for nothing, the will power is everything!. Hivyo kitu ninachokiomba kwenye bandiko hili kutoka kwako ni kimoja tuu, your will!.

Hivyo kwenye hili jambo langu,
, nawaomba tusimame pamoja kwa kunigawia will zenu!.
  1. Kuna wakati nilipataga ajali mbaya ya Piki Piki, watu wa kwanza to break the news ni JF, hivyo nikasaidiwa nikaokolewa. Thanks JF to save my life, Thanks God for JF.
  2. Nikapelekwa South Africa kutibiwa, Hospital ya Milpark, Wana JF wa Joburg walinifariji Sana. Thanks for all JF brotherhood na Sisterhood
  3. Gharama za Treatment ya South Africa zikawa kubwa kuliko family affordability, hivyo tukatafuta cheaper option, tukapata India, Apollo Hospital, New Delhi. Wana JF wa Dheli walinifariji Sana. Nilichangiwa gharama za matibabu na Wana JF dunia nzima!. Thanks Wana JF for support.
  4. Nikiwa India, kuna tangazo la kazi lilipostiwa humu jf kwenye nafasi za kazi, FCO ya Uingereza, nikaomba na nikapata, nikaajiriwa na FCO na kupostiwa DAR es Salaam. Thanks for JF Kunipatia kazi.
  5. From there JF ndio kama ndugu zangu wa kwanza. Nilikuja kupata matatizo ya kuitwa Dodoma baada ya gazeti la Raia Mwema kuichapisha makala yangu ya jf as their lead story.
  6. Kufuatia matatizo hayo wife akaimaind Sana jf na kunishauri nichague moja ama jf ama yeye!. Huwezi amini, ili kulinda familia niliamua kuachana na if.
  7. Huwezi amini, nilijikuta nimeshindwa ndipo nikajua kumbe jf ni very addictive. Kwanza nikawa naingia Kwa siri, usiku mkubwa akiwa amelala, alipogundua akanikumbusha kuchagua moja, nilichagua jf. Thanks for her understanding. Bado yupo.
  8. Enzi niko fit kiuchumi, enzi zile za harambee, mimi ni miongoni mwa wana JF tuliochangia jf 6 figures!.
  9. Kauli huumba!. Baada ya kuitwa njaa, kiukweli kauli ile iliniumbia njaa kwani, tenders zangu zote za publicty zilifutwa na njaa ya kweli ikanitembelea kweli!. Ukijumlisha na Corona, licha ya kuwa na ndugu, jamaa na marafiki wenye uwezo, ni mwana JF mmoja fulani alijitokeza to my rescue to save me!. Thanks kwa mwana JF huyu!
  10. Sasa leo ninakuja tena kwenu wana JF, nina jambo langu.
  11. Kabla sijalitaja Jambo lenyewe, naomba kwanza kwa unyenyekevu kabisa, kuwaeleza Wana JF wenzangu, kuwa mimi ni binadamu tuu na sio malaika, hivyo kuna watu humu tumepishana kauli, tumekwazana, tumekosana, tumetukanana, nimewakosea, nawaomba msamaha kwa yote niliowakosea na wote walionikosea nimewasamehe, ignore list yangu nime unignore, samahanini Sana!.
  12. Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana!. Naomba msamaha mnisamehe kwa yote kwasababu sisi binadamu wote ni viumbe dhaifu, kukosa ni ubinaadamu na hakuna mkamilifu!. Please forgive me for everything and I apologize for whatever I did wrong to whoever niliye mkosea, samahani sana naomba mnisamehe!.
  13. Jambo langu ni baada ya kujaribu Kawe na kuambulia kura moja!, sasa kumejitokeza fursa nyingine. Hivyo kitu cha kwanza nilichofanya ni kuwashirikisha nyinyi Wana jf, ninacho kiomba kwenu ni kitu kimoja tuu, naomba baraka zenu na support yenu, ya will ili, kuniwezesha kutupa karata yangu tena kwenye hili jambo langu.
  14. Naomba kwa sasa nisilitaje hilo jambo, na nakuomba na wewe hata kama utalihisi, nakuomba usitaje, please!. Kuna sababu.
  15. Baada ya hiyo fursa kutangazwa, mimi nimejipima uwezo wangu, ability yangu na capabilities nilizo nazo, nikakuona ninaweza, nina uwezo nalo in terms of ability, na capabilities niko capable ninachohitaji ni just moral support.
  16. Ninachohitaji kwenu ni kitu kimoja tuu, moral support Kwa kuniunga mkono kwa sala zenu, kupitia a collective bargaining "powers of will" za wana jf wote collectively kuniwezesha by goodwill zenu. Just wish me good, hiyo will power yako ina nguvu kuliko kitu kingine chochote!. Naombeni tutumie powers of positivism na affirmative kuniwezesha niweze.
  17. Wale msio nikubali au kukubaliana na mimi, naowamba sana sana sana, na niko chini ya miguu yenu, mnisamehe kwa yote ya nyuma na kunisaidia kwa kutochangia negative kwenye uzi huu, kama mmeshindwa kabisa kunisamehe, basi please just ignore me kwa kutochangia chochote kwenye bandiko hili ili msilete negative powers nikaja kuambulia kura moja tena!. Please nihurumieni!.
  18. Baada ya kujipima na kujiona nina uwezo, ability na capabilities, lakini natakiwa kujengewa uwezo zaidi in terms of capacity, niwe capacited ili niwe capable, niwezeshwe niweze, hata nikihitajika kunyoosha mkono mahali popote parefu, niwe na uwezo wa kuunyoosha huo mkono, urefuke na kufika popote. Hivyo nawaombeni mniunge mkono kwa hili kupitia moral support yenu
  19. Ewe Mwana jf mwenzangu, tusahau tofauti zetu, nakuomba uniunge mkono kwenye hili, together we can!.
  20. Naamini nitayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu!. Mungu Nisaidie!. Sema Amen!. Hiyo Amen yako is all that I need!. Natanguliza shukrani na ubarikiwe sana!
Paskali.
Hakika mungu ni mwema siku zote aombae humpa kile aaminicho,inshallah mungu akufanyie wepesi katika hitaji lako.
 
Mkuu

Anamuweza nani?

Anaweza kazi zake zinazomuhusu yeye binafsi,sisi hatuhusiki,even kupiga kura sio sisi!

Hiyo ni his own problem ajifunze kutatua matatizo yake binafsi ya kupenda madaraka

Kama ni kura awafate wahusika,kama ni bajeti atafute hela zake au akakope benki,etc

Sio anahamisha uchu wake wa kupenda uongozi kwetu sie tusiohusika

Haya ni makelele yake tu ya kuhamisha mavitu yaliyojaa ubongoni mwake kwa wengine apate chochote....

Fvck him!
Duh !! Si0 bure !!!
 
Kwanza wote tuseme Amen, ila kwenye mchakato huu Paskali utaikumbuka sana Chadema na kuyaona madhara live ya Magufuli.

Shyrose Banji alisha nafasi ya ubunge wa Africa mashariki kwa kura za Chadema, ni Freeman Mbowe alikubali kumbeba Shyrose Banji licha ya kwamba Shyrose ni ccm.

Tumekuwa tukisema hapa kila siku madhara ya ushetani alioufanya Magufuli kwa Taifa hili yataendelea kuleta athari kwa miaka mingi ijayo, sasa unakwenda kurealize wewe mwenyewe.

Kwa hii mijitu ya ccm ambayo rushwa ipo kwenye damu yao ni jina lako tu ndio huenda na kama Mungu amepanga ndio vitakubeba.

Mungu akutangulie kila la kheri.

Mmh kwa kura ngapi za chadema?! Na kumbuka shyrose alivyokua mbunge Magu hakua Rais ukiwa muongo usiwe msahaulifu bye
 
Kwani Shyrose Banji alivyoombewa kura na Freeman Mbowe kwq wabunge wa Chadema hakuwa mwanachama wa ccm?

Au hujui Le Mutuz alikosa huo Ubunge baada ya wabunge wa Chadema kumtosa dakika za mwisho? Tena mbaya zaidi alidanganywa na mtoto mdogo tu Joshua Nasari.

Kuna aja ya JF hizi ID ziwe zinadisplay na umri hii itasaidia kutoshindana na watoto ambao mlikuwa shule miaka michache iliyopita ila humu kwenye forum ni mahodari wa matusi wakati Mwenyekiti Mbowe alishawakataza kutukana watu.

We bwana ni zero shyrose alikua mbunge 2012 to 2017 hapo magufuli alihusika vipi na hao chadema walimpaje kura jinga kubwa hata kama unamchukia magu usimzulie uwongo woiii
 
Ndugu Emanueli misalaba , ndugu P yeye hafai kwenye huo u DC, hiyo ni kumfanya asitumie akili, uwezo na uzoefu wake.
P ni mkubwa zaidi ya u DC, u DED au u RC.
Naamini akipewa nafasi ya kuwa mtunga sera,mtunga sheria au mtekelezaji sera,atafanya vyema zaidi ya watu wengi waliopo au waliokuwepo kwenye nafasi hizo.
Hivi P kwa mfano akipewa TBC aiendeshe, au apewe TCRA, si kutakuwa na mabadiliko makubwa sana yenye maslahi kwa taifa na wananchi!!???
Usemayo inaweza kuwa kweli, lakini itatengemea na anaye mchangua matakwa yake ni yapi?
Akiambiwa afanye kwa kadiri ya katiba na viapo alivyoapa atakuwa huru kuitendea haki tasnia yake, lkn km kutakuwa na kufungwa mikono hamna Kipya.
 
Dhati yako kwa wahitaji wa Uwajibikaji wako kulingana na nafasi yako na ibebe Nia na Dhamira yako.

Na kama Dhati yako si juu ya Ustawi wa wakuzungukao basi Matamanio yako si Kitu kwao, na hata kama utayafikia itakuwa kazi bure.

Tumaini DHATI uliyonayo, itakutendea.
 
Back
Top Bottom