Nimepambana nimeishia hapa, nimelileta jambo langu kwenu Wana-JF

Jan 13, 2023
92
99
Habari zenu wadau wa JF

nimekuja kwenu na jambo langu naomba kuwashirikisha natumaini kupitia nyie natapa solution. Direct to the point, nimejenga nyumba moja kubwa yenye pande mbili zinazojitegemea upande mmoja ni kwa ajili yangu na upande wa pili nilijenga kwa ajili ya kuweka mpangaji.

Naomba nijikite kwenye upande huu wa kupangisha, upande wa mpangaji unavyumba viwili vyakulala, sebule, dinning, stoo na jiko. Nyumba imefikia 80% ya ujenzi hadi sasa, bado vigae, vioo na rangi. Nimeshindwa kuikamilisha kwa 100% kutokana na changamoto za kiuchumi zinazonikabili kwa kipindi hiki, kiukweli sioni kama naweza kuimaliza kwa vijisenti nilivyobaki navyo kama akiba yangu.

Lengo la andiko hili ni kuomba/kutafuta mtu ambaye anaweza kunisaidia kumalizia kazi hii ya ujenzi kwa makubaliano ya malipo ya baadaye. Kwa mfano, mtu anaweza kunikopesha hela ya kumalizia ujenzi kwa makubaliano ya maandishi, yakuwa anachukua kodi ya nyumba deni hadi pale deni lake litakapomalizika. Au kama kuna mtu anahitaji nyumba ya kuishi tuingie makubaliano anilipe kodi ya mwaka mzima mapema kabla hajaamia nitumie hela (kodi) hiyo kufanya finishing.

Kwa makadilio aliyofanya fundi hela inayohitajika ili kamilisha ujenzi wa nyumba upande wa kupangisha ni Tsh 3,000,000 na makadilio ya kodi ni Tsh 250,000 kwa mwezi. Baadhi ya vitu kama vile cemment, gypsum body, wallput mikada ya maua ya gypsum body ipo na pia umeme na maji pia vipo

Location ni Mwanza, Ilemela jirani na Malaika Beach, sehemu ni nzuri, usalama wakutosha na panafikika kwa urahisi, kiufupi ni rahisi kupata mpangaji kama ikikamilika 100%.

Maoni na ushauli wenu ni muhimu ili niweze kupata njia ya kutoka hapa nilipokwama, pia unaweza kunipigia nikakutumia picha au nikakuelekeza ukaja directly kwenye nyumba tukafanya majadiliano na kufikia makubaliano
+255758779170
 
Picha ungeweka hapa hapa tu kiongozi

Ningekushauri ujaribu kwenye taasisi hizi sema na wenyewe wana Riba ya kijinga sana, ili ukipata Kodi uielekeze huko mpaka deni liishe..

Ila pambana upate mpangaji atayeweza kulipa mwaka mzima maana Hapo utapata 2.8 unamaliza na yeye anaingia anakaa mwaka wake fresh tu

Kila la kheri mkuu
 
1. Nyumba iko sehemu gani?
2. Ulikuwa unajenga nyumba ya kuishi au kupangisha?
3. Kwani hizo fedha za kujenga hadi ukafika hapo ulipoishia ilizipataje?
4. Je ulizinganga kwa muda gani?
5. kwa nini sasa unataka umalizie haraka? Kwa nini usisubiri upate pesa taratibu?
 
1. Nyumba iko sehemu gani?
2. Ulikuwa unajenga nyumba ya kuishi au kupangisha?
3. Kwani hizo fedha za kujenga hadi ukafika hapo ulipoishia ilizipataje?
4. Je ulizinganga kwa muda gani?
5. kwa nini sasa unataka umalizie haraka? Kwa nini usisubiri upate pesa taratibu?
1. Nyumba iko Mwanza, Ilemela
2. Nilijenga kwa nyumba moja kubwa yenye pande mbili (two in one) upande mmoja nikae mimi na upande mwingine ni kwajili ya kupangisha
3. Wakati huo nilikuwa nafanya kazi kwenye mradi fulani
4. Miaka miwili
5. Muda mwingi nitakuwa sikai Mwanza nataka nimalizie haraka ili kuwe na usalama wakati ambao sitokuwepo, mtu akiwa anaishi upande wa pili usalama unakuwepo hata nisipokuwepo miezi 3
 
Back
Top Bottom