Wana JF, niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba baraka zenu & moral support yenu jambo langu hili liwe! Mniombee Mungu asaidie, awezeshe liwe!

Wana JF wenzangu,
Kuna msemo usemao "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu", "Vox Populi is Vox Dei"

Hili ni Bandiko la kukusanya sauti za wengi ili iwe ni sauti ya Mungu. Mimi mwana jf mwenzenu Pascal Mayalla, nina jambo langu ambalo mimi kama mimi peke yangu kama Pascal Mayalla peke yangu na familia yangu tuu, na ndugu zangu tuu, na jamaa zangu tuu na rafiki zangu tuu, pekee, hatuwezi, hivyo naomba kuwashirikisha wana jf ili hili jambo langu, lisiwe ni jambo langu tuu, bali liwe ni jambo letu, umoja ni nguvu, together we can.

Pasikali, sio tuu ni mwenzenu, humu jf, bali mimi ni ndugu yenu. Baadhi tuko humu pamoja toka ile 2006, jf ikiitwa Jambo Forums hivyo ni zaidi ya miaka 15 pamoja!. sasa. Kuna watu tunafahamiana kupitia jf, kuna watu tumesaidiana kupitia jf, na wengine hadi kutembeleana home na kushirikiana kwenye shida na raha na kuna misiba ya wana jf, we drive all the way hundreds of kilometers just to bid farewell to a jf member!.

Enzi zile najiunga jf nilikuwa kijana shababi, kuna mikoa ya baridi, nilikuwa nikitua tuu na kupost kitu chochote, kutoka mkoa huo, pm zitaingia kuniulizia niko nimefikia wapi na hadi blangeti la kuzuia baridi napata kutoka kwa mwana JF!, what a love!.

JF is Like Home to Me, It's More Than A Friend, It's A Family. Nalala jf, naamka jf, nashinda jf, jf is everything!, its a big family, tukianza kuji consolidate na kutumia a consolidated powers ya nguvu yetu ya ushawishi as a pressure group, we can do wonders!. Hii togetherness yetu lets start using it as one, Kwanza Kwa kusahau tofauti zetu za kisiasa na vyama vyetu, tuka supportiana as one, tuka stand together as one kwa jambo letu, ile powers ya pamoja ndio the magic behind!,tutatusua!.

Msione watu wanakusanya the multitude of people nje kwao for a whole day na jioni baada tuu ya kuzama jua, kuwagawia Ten Ten,kuwalisha au kuwafuturisha!.

Au matajiri wanashindana kudhamini timu za mpira za Simba na Yanga, spending billions!. Go find out wafanyakazi wa viwandani kwa matajiri hao wanalipwa shilingi ngapi!, unaweza usiamini, it's not for nothing, the will power is everything!. Hivyo kitu ninachokiomba kwenye bandiko hili kutoka kwako ni kimoja tuu, your will!.

Hivyo kwenye hili jambo langu,
, nawaomba tusimame pamoja kwa kunigawia will zenu!.
  1. Kuna wakati nilipataga ajali mbaya ya Piki Piki, watu wa kwanza to break the news ni JF, hivyo nikasaidiwa nikaokolewa. Thanks JF to save my life, Thanks God for JF.
  2. Nikapelekwa South Africa kutibiwa, Hospital ya Milpark, Wana JF wa Joburg walinifariji Sana. Thanks for all JF brotherhood na Sisterhood
  3. Gharama za Treatment ya South Africa zikawa kubwa kuliko family affordability, hivyo tukatafuta cheaper option, tukapata India, Apollo Hospital, New Delhi. Wana JF wa Dheli walinifariji Sana. Nilichangiwa gharama za matibabu na Wana JF dunia nzima!. Thanks Wana JF for support.
  4. Nikiwa India, kuna tangazo la kazi lilipostiwa humu jf kwenye nafasi za kazi, FCO ya Uingereza, nikaomba na nikapata, nikaajiriwa na FCO na kupostiwa DAR es Salaam. Thanks for JF Kunipatia kazi.
  5. From there JF ndio kama ndugu zangu wa kwanza. Nilikuja kupata matatizo ya kuitwa Dodoma baada ya gazeti la Raia Mwema kuichapisha makala yangu ya jf as their lead story.
  6. Kufuatia matatizo hayo wife akaimaind Sana jf na kunishauri nichague moja ama jf ama yeye!. Huwezi amini, ili kulinda familia niliamua kuachana na if.
  7. Huwezi amini, nilijikuta nimeshindwa ndipo nikajua kumbe jf ni very addictive. Kwanza nikawa naingia Kwa siri, usiku mkubwa akiwa amelala, alipogundua akanikumbusha kuchagua moja, nilichagua jf. Thanks for her understanding. Bado yupo.
  8. Enzi niko fit kiuchumi, enzi zile za harambee, mimi ni miongoni mwa wana JF tuliochangia jf 6 figures!.
  9. Kauli huumba!. Baada ya kuitwa njaa, kiukweli kauli ile iliniumbia njaa kwani, tenders zangu zote za publicty zilifutwa na njaa ya kweli ikanitembelea kweli!. Ukijumlisha na Corona, licha ya kuwa na ndugu, jamaa na marafiki wenye uwezo, ni mwana JF mmoja fulani alijitokeza to my rescue to save me!. Thanks kwa mwana JF huyu!
  10. Sasa leo ninakuja tena kwenu wana JF, nina jambo langu.
  11. Kabla sijalitaja Jambo lenyewe, naomba kwanza kwa unyenyekevu kabisa, kuwaeleza Wana JF wenzangu, kuwa mimi ni binadamu tuu na sio malaika, hivyo kuna watu humu tumepishana kauli, tumekwazana, tumekosana, tumetukanana, nimewakosea, nawaomba msamaha kwa yote niliowakosea na wote walionikosea nimewasamehe, ignore list yangu nime unignore, samahanini Sana!.
  12. Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana!. Naomba msamaha mnisamehe kwa yote kwasababu sisi binadamu wote ni viumbe dhaifu, kukosa ni ubinaadamu na hakuna mkamilifu!. Please forgive me for everything and I apologize for whatever I did wrong to whoever niliye mkosea, samahani sana naomba mnisamehe!.
  13. Jambo langu ni baada ya kujaribu Kawe na kuambulia kura moja!, sasa kumejitokeza fursa nyingine. Hivyo kitu cha kwanza nilichofanya ni kuwashirikisha nyinyi Wana jf, ninacho kiomba kwenu ni kitu kimoja tuu, naomba baraka zenu na support yenu, ya will ili, kuniwezesha kutupa karata yangu tena kwenye hili jambo langu.
  14. Naomba kwa sasa nisilitaje hilo jambo, na nakuomba na wewe hata kama utalihisi, nakuomba usitaje, please!. Kuna sababu.
  15. Baada ya hiyo fursa kutangazwa, mimi nimejipima uwezo wangu, ability yangu na capabilities nilizo nazo, nikakuona ninaweza, nina uwezo nalo in terms of ability, na capabilities niko capable ninachohitaji ni just moral support.
  16. Ninachohitaji kwenu ni kitu kimoja tuu, moral support Kwa kuniunga mkono kwa sala zenu, kupitia a collective bargaining "powers of will" za wana jf wote collectively kuniwezesha by goodwill zenu. Just wish me good, hiyo will power yako ina nguvu kuliko kitu kingine chochote!. Naombeni tutumie powers of positivism na affirmative kuniwezesha niweze.
  17. Wale msio nikubali au kukubaliana na mimi, naowamba sana sana sana, na niko chini ya miguu yenu, mnisamehe kwa yote ya nyuma na kunisaidia kwa kutochangia negative kwenye uzi huu, kama mmeshindwa kabisa kunisamehe, basi please just ignore me kwa kutochangia chochote kwenye bandiko hili ili msilete negative powers nikaja kuambulia kura moja tena!. Please nihurumieni!.
  18. Baada ya kujipima na kujiona nina uwezo, ability na capabilities, lakini natakiwa kujengewa uwezo zaidi in terms of capacity, niwe capacited ili niwe capable, niwezeshwe niweze, hata nikihitajika kunyoosha mkono mahali popote parefu, niwe na uwezo wa kuunyoosha huo mkono, urefuke na kufika popote. Hivyo nawaombeni mniunge mkono kwa hili kupitia moral support yenu
  19. Ewe Mwana jf mwenzangu, tusahau tofauti zetu, nakuomba uniunge mkono kwenye hili, together we can!.
  20. Naamini nitayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu!. Mungu Nisaidie!. Sema Amen!. Hiyo Amen yako is all that I need!. Natanguliza shukrani na ubarikiwe sana!
Paskali.
Mkuu niliomba namba ya kukuchangia iwe wazi!
 
Kuna watu siku wakiondoka hapa duniani, kutatokea upweke wa kutisha! Pascal Mayalla is one of them. Yaani mpaka afikie kwenye point, basi ataipaka mafuta story yake kiasi huwezi kuchoka kusoma

Kila la heri mkuu. Ingawa una wakati mgumu kwa namna fulani. Maana siku zote ccm ina wenyewe. Labda kama na wewe ni sehemu ya hao wenyewe! Maana unaweza ukawa mwanachama, au unavaa yale mashati yao ya kijani yenye nembo ya jembe na nyundo, na suruali nyeusi! Halafu bado usiwe sehemu ya wenye chama.
Huyu sifa zote anazo.
 
Natamani uchaguliwe na chama, Ili UENDE bungeni kwenye interview, pale nitajua kama wewe unaweza kujieleza vizuri kama unavyoandika?? Uandishi ni kipaji, kujieleza pia ni kipaji kingine, Pascal Mayalla
Mkuu @ngaiwaye, Amen, Amen!.
Umenianzishia vizuri hii siku yangu ya leo.
Wana JF wenzangu,
Kuna msemo wa lugha ya Kilatini usemao "Vox Populi is Vox Dei" kumaanisha "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu"
Hili ni Bandiko la kukusanya sauti za wengi ili kutumia sauti hizo ziwe ni sauti ya Mungu.

Mimi mwana jf mwenzenu Pascal Mayalla, nina jambo langu ambalo mimi mwenyewe tuu, yaani mimi kama mimi, Pascal Mayalla peke yangu, siliwezi!. Mimi na familia yangu tuu pekee hatuwezi!, Mimi na ndugu zangu tuu, na jamaa zangu tuu na rafiki zangu tuu, pekee yetu, hatuwezi, hivyo sasa naomba kuwashirikisha nyinyi ndugu zangu wana jf ili kuli transform hili jambo langu, lisiwe ni jambo langu tuu, bali liwe transformed into jambo letu, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, together we can, if kila mmoja wetu will play his/her part!.

Hivyo kwenye hili jambo langu,
, nawaomba tusimame pamoja kwa kunigawia will zenu za YES kuliwezesha hili jambo langu liwe!.
  1. Ninachohitaji kwenu ni kitu kimoja tuu, moral support kwa kuniunga mkono kwa sala zenu, kupitia a collective bargaining "powers of will" za wana jf wote collectively kuni endorse na kuniwezesha by goodwill zenu. Just wish me good, hiyo will power yako ina nguvu kuliko kitu kingine chochote!. Naombeni tutumie powers of positivism na affirmative kuniwezesha niweze kwa wewe kusema tuu YES hata kimoyo moyo!.
  2. Wale msio nikubali au kukubaliana na mimi, naowamba sana sana sana, na niko chini ya miguu yenu, mimi ni binadamu tuu, mnisamehe kwa yote ya nyuma na kunisaidia kwa kutochangia negative kwenye uzi huu, kama mmeshindwa kabisa kunisamehe, basi please just ignore me kwa kutochangia chochote kwenye bandiko hili ili msilete negative powers nikaja kuambulia kura moja tena!. Please nihurumieni!.
  3. Baada ya kujipima na kujiona nina uwezo, ability na capabilities, lakini natakiwa kujengewa uwezo zaidi in terms of capacity, niwe capacited ili niwe capable, niwezeshwe niweze, hata nikihitajika kunyoosha mkono mahali popote parefu, niwe na uwezo wa kuunyoosha huo mkono, urefuke na kufika popote!. Hivyo nawaombeni mniunge mkono kwa hili kupitia moral support yenu
  4. Ewe Mwana jf mwenzangu, tusahau tofauti zetu, nakuomba uniunge mkono kwenye hili, together we can!.
  5. Naamini nitayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu!. Mungu Nisaidie!. Sema Amen!. Hiyo Amen yako is all that I need!. Natanguliza shukrani na ubarikiwe sana!
Paskali.
Ubarikiwe sana.
P
 
PASKALI licha ya kukutakia kila la kheri kwenye hilo jambo lako, lakini naona kama umejibana sana kwa kuweka all your eggs kwa one basket which I think is not fair to me, there is always next chance in life no matter what..
Mkuu @dennoJ, its true hili jambo nimelipania sana, ila sijaweka mayai yangu yote kwenye kikapu kimoja, mimi bado ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea na pia ni wakili wa kujitegemea pia kwa kujitolea, hivyo bado naweza kuendesha maisha yangu yote hadi siku ya 6ft under, bila kumatatizo yoyote.
P
 
Pascal Mayalla kwenye hilo Jambo lako unataka kubeba Agenda gani. Misimamo yako ni kama ya Massele au wewe misimamo yako ni kama ya Kibajaji?
Mkuu Allen Kilewella , kwanza mimi nimebahatika, kuwa miongoni mwa waandishi wa habari tuliadhaminiwa na EAC kuzungunguka nchi zote za EAC wakati tukianzisha Custom Union na Common Market, hivyo nimeona jinsi wenzetu walivyo makini not only kwenye ku set agenda, pia ku push forward agenda zao!. Kati ya nchi zote 7 za EAC, Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa fursa, na comparative advantage ya kufaidika na EAC kuliko nchi nyingine zote, lakini Watanzania hatujazichangamkia fursa hizo ipasanyo na kikamilifu, hivyo agenda yangu kuu ni kuwafungua macho Watanzania kuhusu fursa hizi ili Watanzania wazitambue na kuzi grab!.

Nimeanza kwa kuandika mfufulizo wa makala za EAC Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na Fursa za Mtangamano-1 Ni Nchi ya 4 Duniani yenye Maliasili, Rasilimali Lukuki!. Watanzania Tuchangamkie Fursa! ambazo zitafuatiwa na kipindi cha TV na baadaye ope dialogues.
ila pia I have a certain specific agenda, naomba nisiitaje humu nikaja kuwa preempted na wengine nikaishi kuonekana ni copycat!.
P
 
Kuna watu siku wakiondoka hapa duniani, kutatokea upweke wa kutisha! Pascal Mayalla is one of them. Yaani mpaka afikie kwenye point, basi ataipaka mafuta story yake kiasi huwezi kuchoka kusoma
Mkuu Tate Mkuu , asante sana for this
Kila la heri mkuu. Ingawa una wakati mgumu kwa namna fulani. Maana siku zote ccm ina wenyewe. Labda kama na wewe ni sehemu ya hao wenyewe! Maana unaweza ukawa mwanachama, au unavaa yale mashati yao ya kijani yenye nembo ya jembe na nyundo, na suruali nyeusi! Halafu bado usiwe sehemu ya wenye chama.
Pi hii ni kweli, mimi ni mwana CCM contemporary, kuna wana CCM wenyewe aombao ndio wenyewe, ma proletariats halafu kuna sisi wana CCM ma lumpen!, mimi ni lumpen, CCM ya sasa ni CCM ya ma proletariats, there is no way a lumpen unaweze kuwa considered, nilichofanya ni kukiandikia chama changu barua ya wazi kukiomba kikuteulie watu wazuri hata wakiwa ni ma lumpen!.

Kumejitokeza wagombea 187 kuwania nafasi 6 za CCM. Kati ya nafasi hizo, nafasi 3 zimetengwa kwa wanawake, hivyo nafasi zimebaki tatu, nafasi moja lazima iende Zanzibar, hivyo zimebaki nafasi 2!, wagombea wanaume tuko zaidi ya 100!, hivyo pamoja na mimi kuwa sifa na vingezo, there are chances, naweza kuzidiwa na wengine kwa sifa na vigezo, hivyo naweza kabisa kukosa kihalali kabisa na tukapeleka the best of the best kule!.

Kama nitakatwa tena, kama nilivyofanyiwa Kawe, na wakachukuliwa matapeli wale mikono mirefu, that is detrimental kwa taifa na sio kwangu!, chama changu CCM kitakuwa hakija watendea haki Watanzania hivyo karma hainaga mswalie Mtume!, itambeza tena bakora zake!.
Mungu nisaidie!.
P
 
Shida yako umevaa suti nyeupe (hiyo agenda yako) lakini unataka kuuza mkaa (Kugombea kupitia CCM).
Mkuu Allen Kilewella, kwanza ni kweli kabisa, mimi sio tuu nimavaa suti nyeupe, nimavaa suti nyeupe ya kitambaa cha less material ambayo transparent, kama shela la bibi harusi!, huku CCM ni masizi!. Mimi ni muumini wa ukweli na uwazi, namna pekee ya kuiponya CCM ni kuwaingiza watu wakweli na wawazi.
Hutoboi na ukitoboa hiyo agenda yako haitatekelezeka.
Hili niliwaomba hapa na wewe nakuomba tena
Wana JF wenzangu,
Kuna msemo wa lugha ya Kilatini usemao "Vox Populi is Vox Dei" kumaanisha "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu"
Hili ni Bandiko la kukusanya sauti za wengi ili kutumia sauti hizo ziwe ni sauti ya Mungu.
  1. Ninachohitaji kwenu ni kitu kimoja tuu, moral support kwa kuniunga mkono kwa sala zenu, kupitia a collective bargaining "powers of will" za wana jf wote collectively kuni endorse na kuniwezesha by goodwill zenu. Just wish me good, hiyo will power yako ina nguvu kuliko kitu kingine chochote!. Naombeni tutumie powers of positivism na affirmative kuniwezesha niweze kwa wewe kusema tuu YES hata kimoyo moyo!.
  2. Wale msio nikubali au kukubaliana na mimi, naowamba sana sana sana, na niko chini ya miguu yenu, mimi ni binadamu tuu, mnisamehe kwa yote ya nyuma na kunisaidia kwa kutochangia negative kwenye uzi huu, kama mmeshindwa kabisa kunisamehe, basi please just ignore me kwa kutochangia chochote kwenye bandiko hili ili msilete negative powers nikaja kuambulia kura moja tena!. Please nihurumieni!.
Paskali.
Just say YES!.
P
 
Mchakato umefikia wapi? i believe you can at least say something there. Ila yule mama atakusamehe kweli?
Leo CC ya CCM wanakaa pale CCM Lumumba kupitisha chekecheke. Yule mama wa hii issue A shock of my life, furaha yageuka shubiri. Be good to people on your way up, you might meet them on your way down, mwenzenu leo yamenikuta! kitendo tuu cha kuamka na kuja kinisalimia kunikuuliza kama namkumbuka, ni dalili ya msamaha tosha!, maana angekuwa bado yuko bitter na mimi, wala asingenisalimu, ni kuta tuu jina na kutupa kule pipani fasta!.
Hivyo nisipo pita nitakuwa ni nimezidiwa na sifa na wengine wazuri kuliko mimi.
P
 
Leo CC ya CCM wanakaa pale CCM Lumumba kupitisha chekecheke. Yule mama wa hii issue A shock of my life, furaha yageuka shubiri. Be good to people on your way up, you might meet them on your way down, mwenzenu leo yamenikuta! kitendo tuu cha kuamka na kuja kinisalimia kunikuuliza kama namkumbuka, ni dalili ya msamaha tosha!, maana angekuwa bado yuko bitter na mimi, wala asingenisalimu, ni kuta tuu jina na kutupa kule pipani fasta!.
Hivyo nisipo pita nitakuwa ni nimezidiwa na sifa na wengine wazuri kuliko mimi.
P
Huwezi jua kuna msemo wa watu kukuua huku akicheka.
 
Back
Top Bottom