Wana CCM Wajipanga Kuikomboa Moshi Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana CCM Wajipanga Kuikomboa Moshi Mjini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ben Saanane, Sep 6, 2008.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Wana CCM wajipanga 'kuikomboa' Moshi Mjini

  Na Heckton Chuwa, Moshi

  BAADHI ya wanachama wa CCM wanadaiwa kuunda timu maalumu ya siri ndani ya chama hicho, kijulikanacho kama Tuikomboe Kilimanjaro (TUKI), chenye nia ya kulikomboa jimbo la Moshi Mjini na kulinda yanayoshikiliwa na wabunge wa CCM.

  Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya chama hicho, hali hiyo imeleta hofu kubwa ndani ya chama hicho wakiwamo wabunge walioko madarakani sasa hivi.

  Timu hii inadaiwa kujumuisha makada wenye majina katika medani ya siasa mkoani Kilimanjaro na ambao wajumbe halali wa kura za maoni ndani ya chama hicho katika wilaya zao.

  Imeelezwa kujitokeza kwa kikundi hiki ambacho viongozi mbalimbali wa CCM wamesema hakina uhalali wowote umeanza kuleta chuki miongoni mwa wana CCM wakiwamo wakongwe wa siasa mkoani hapa.

  Hata hivyo, uongozi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro na wa Moshi mjini, umekanusha kukijua au kuhusika na kikundi hicho.

  Majimbo yanayodaiwa kulengwa na timu hiyo na majina ya wabunge wake kwenye mabano, ni Hai, (Fuya Kimbita); Vunjo (Aloyce Kimaro); Moshi Vijijini (Dkt. Cyril Chami); Rombo (Basil Mramba); Mwanga (Profesa Jumanne Maghembe) na Same Magharibi (Dkt. Mathayo David), Moshi Mjini (Bw.Philemon Ndesamburo) CHADEMA.

  Majimbo ambayo yanaonekana kutolengwa na timu hiyo ni ya Siha la Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Aggrey Mwanri na Same Mashariki la Bibi Anne Kilango-Malecela, kwa madai kuwa wabunge wake wamejitahidi kutekeleza sera ya CCM kiasi cha wananchi kukosa sababu za kutowarudisha bungeni.

  Uchunguzi uliofanywa na Majira umebaini kuwa kuna baadhi ya watu tayari wanatajwa kuwa wagombea katika baadhi ya majimbo.

  Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, wahusika katika timu hiyo wamekuwa wakifuatilia kwa njia moja au nyingine, mienendo ya wabunge waliopo sasa wakiwamo wa CCM yenyewe kuangalia kama kazi walizofanya katika majimbo yao zinaweza kuwauza wakati wa kampeni zijazo.

  “Unajua hatutaki kupata matatizo ambayo tumeyapata mwaka 2000 na 2005 katika kuuza wagombea wetu,” alisema kada wa CCM, ambaye alikiri kuwa mmoja wa wanatimu hiyo.

  Alisema tayari wana ripoti za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya wabunge wote wa chama hicho na kwamba ripoti hiyo itakuwa ndiyo dira yao kuamua wamrudishe mbunge mhusika au la, na pia kuwa wamekuwa pia wakifuatilia maoni ya wananchi wa jimbo husika.

  Pamoja na timu hiyo kuonekana kulenga kukiimarisha chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2010, lakini baadhi ya wana CCM walisema kwa upande mwingine, huenda ikaleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho na hatimaye kuzaa makundi, jambo ambalo walisema linaweza hata kupunguza idadi ya majimbo ambayo CCM inayashikilia.

  “Ugonjwa huu wa makundi wakati wa uchaguzi mkuu mbalimbali ndiyo umeimaliza CCM hapa Moshi mjini na kuna hatari ya ugonjwa huu kuenea katika majimbo mengine mkoani hapa na hii ni hatari kwa chama chetu,” alisema kada huyo.

  Akizungumzia suala hilo hivi karibuni, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Vicky Nsilo Swai, alisema CCM haina na wala haiundi vikundi vya namna hiyo.

  "Uongozi wa CCM mkoa hauna habari na kikundi hicho na watu wa namna hiyo ni agents of confusion (wanatumika kuchanganya watu)," alisema.

  Alisema chama mkoani humo kingependa kuwafahamu wale waliounda kikundi hicho na waeleze ni nani aliyewatuma kukianzisha na kwamba kama kuna mtu mwenye uchungu na CCM hana budi kushirikiana na uongozi wa chama hicho katika azma ya kukiendeleza.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Moshi Mjini, Bw. Godfery Mwangamilo, pia alikanusha kukifahamu kikundi hicho ambapo alisema CCM ina utaratibu wa kuteua wagombea na kwamba wakati ukifika ndio utakaotumika

  Source.Majira.
  NB: Upinzani mmejipanga vipi kuhakisha mmeongeza majimbo na kushikilia mliyo nayo? Mzee Ndesa hatutaki kusikia mafisadi wanalichukua hilo jimbo.Jimbo la Moshi mjini pamoja na kwamba mzee Ndesa amekua akiwekewa mtimanyongo na CCM ya huko lakini ameweza kabisa kulibadili lile jimbo.Natamani hii spirit kama ingekua kwa majimbo angalao 60 ya Tanzania.

  Jimbo la Rombo CCM hata wasiahangaike ninarudi very soon kuongeza kasi ya mapambano,nimejiandaa vya kutosha.Hilo tumeshawapokonya.Na warudi baada ya miaka mitano waje waangalie maisha ya Warombo
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2

 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Wanahaha hawa, inasemekana kuna bwana mmoja yuko vodacom anawania jimbo la moshi vijijini anaitwa mmasi, mosho mjini kuna aggery mareale
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sijui Chadema watamsimamisha nani Moshi maana Ndesa ametokea kuwa kipenzi cha wengi kwa misaada lukuki ya ambulance na misaada mengine ila nadhani itakuwa ngumu sana kwa CCM kuchukua Moshi mjini na kama bado wanataka kumsimamisha Mama Minde wachore chini wajue wameumia sijui watamsimamisha nani!Zakhia Meghji mwenyewe ni wa kuteuliwa miaka nenda rudi ila kwa Moshi mjini for as long as Babu Ndesa is around its gonna be pretty hard for SisiEmu!
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  wacha watapetape na sasa hivi inabidi kuendeleza siasa za kijasusi pia.Ndio muda muafaka wa opposition kupenyeza mamluki ndani ya makundi kama hayo na kuwajengeaufa mkubwa utakaosaidia kupenya kirahisa.Hoja nzito+sera makini+Ufa kati yao wenyewe= Kubakisha Jimbo

  Naona wanaona hata vikundi vya akina Tambwe Hiza na akina Ngawaiya haviwasidii tena? Wanshikwa kiwewemapema badala ya kuwatumikia wananchi.That's just a sumersault and the will be back at the centre stage.Wamuulize Mama Minde shemejie Mkapa.Alipigishwa sarakasi kwa takribani miaka Kumi,nadhani ameshakata tamaa sasa ni wakati wa akina Agrrey Marealle kujaribu
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,Kevo huyo Zakhia Meghji hata CCM wasije wakakosea kabisa maanake Ndesa atamshinda kirahisi sana,Mama Minde nae hata wasijaribu tena maanake hata huyo mama mwenyewe ataishia kuwashangaa CCM sasa,

  Mtu ambae ataweza kuleta ushindani pale ni Aggrey Marealle ambae nae bado Watu kama akina Peter Kisumo hawataki kumsikia.Watapiga sarakasi sana.
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mods naomba msaada wenu kidogo nimekosea nikapost mara mbili.Thanks in advance
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mzee Ndesa kachoka kimwili na ki-akili apumzike na kuwaachia vijana. Bunge la bajeti alikuwa ni kinara wa ma absentees na vikao vichache alivyo hudhuria most of the time alikuwa fast asleep!
   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hope Kingunge Ngombale Mwiru sounds like kijana according to you, Fikira zake ni hai na zimelikomboa lile Jimbo.Hebu jaribu kufunga safari uende jimboni kwake ukajionee only if you are a True patriot.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka kuna siku Babu alisimama bungeni akawa anawakaribisha watu waje wachuane kwenye jimbo lake haswa wale wanao limezea mate...huyu babu pale hana mpinzani hata kama kachoka wananchi watamchagua tu.
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Sasa ukishaona CCM hawaawamini hata akina Tambwe Hiza na Ngawaiya jua Ndesa kawashika pabaya.No wonder walimfanyia mtimanyongo kwenye ile ishu ya kujenga soko la kisasa kule Kiborloni.It sounds pathetic!
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Toa spin zako hapa ebu tupe ushahidi
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huo ushauri ungempa mzee mnafiki Kingunge ingeeleweka zaidi.
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzee Ndesa naona ni katika watu wa kuwaiga, maneno machache lakini matendo kibao. CCM hawatafanikiwa kumwondoa huyo mzee Moshi Mjini.

  Kama mbunge una deliver kwa wananchi sioni kwanini wakutupe. Tatizo la wabunge wengi ni maneno mengi Dar na Dodoma lakini kwenye majimbo yao sifuri. Ndesamburo sio mmoja wao.

  Ninaamini na mwombea aendelee kushinda Moshi mjini.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,665
  Likes Received: 82,492
  Trophy Points: 280
  Tungepata mikoa 15 tu ya Tanganyika kama Kilimanjaro ambao wameshagundua kwamba CCM haina jipya zaidi ya ufisadi wao kila kukicha na kusaini mikataba isiyo na maslahi ya Tanzania basi tungeikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa mafisadi. Hongereni sana wapiga kura wote wa Kilimanjaro kwa mwamko wenu mkubwa na hivyo kutowapa kura wagombea toka chama cha mafisadi.
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Taarifa za UHAKIKA ni kwamba si Kilimanjaro tu bali ni nchi nzima kuna vikundi vya watu (MAFISADI) ambao wanajipanga kuwang'oa wabunge wa sasa na kuingiza watu wao na kwa Kilimanjaro wamepotosha kujifanya wanawatetea kuna Anne Kilango, wakati huyo ndiye wa kwanza ambaye hawamtaki na wametenga mabilioni kwa kazi hiyo nchi nzima. Sitaki kutaja majina lakini kwa Moshi Vijijini, mtumishi mmoja wa Vodacom tayari amepelekwa huko kuvuruga ili aingie bungeni kama alivyoingia Ngeleja na gazeti la Mtanzania liliandika habari kwamba Vodacom itatoa ajira 550 kwa jimbo la Moshi Vijijini, wakati wakijua ni UONGO mtupu.

  Tutaona na kusikia mengi na kwa taarifa hiyo kutoka katika gazeti la Majira, tena baada ya kijana wao, kurejea kutoka safari ya Marekani na mzee, ujue ni habari kutoka jikoni.
   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Alisema atatoa ajira ni mmasy wa vodacom, hakuna ubaya wowote kama ataweza kummondoa cyril chami, huyu mtu ni mzigo kwa wanachi wa moshi vijijini hakuna lolote alilofanya zaidi ya kujisifu eti alikuwa na phd first class, pia ni mkabila wa kutupwa, yeye anadhani kuwa mbunge ni kutetea maslahi ya wakibosho wenzake, huku wa-uru akiwabagua wazi wazi
   
 18. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mimini mpiga kura wa hili Jimbo

  Napenda kuwahakikishia Cyril Harudi kwani hajafanya lolote. Pili mgombea yeyote atakae toka sehemu za kibosho kwa ujumla awe ccm ama chadema et.al kwani wabunge wote waliopita baada ya Mrema wametoka huko na hakuna walichofanya (Ngotolainyo, Chami na Ngawaiya)
  Hata Kikwete aliambiwa wakati wa Kampeni 2005 akishindwa watamfukuza na itakuwa zamu ya URU na Old moshi kutoa mmbunge regardless ya chama.

  Pia wauru na oldimoshi wanakura zaidi ya 65% ya jimbo zima so wanaouwezo wa kutoa mmbunge. Nilikua huko miezi michache iliyopita na wazee kwa vijana wamesema imetosha.

  Kikwete aliwaahidi mmbunge wao atakuwa waziri hivyo atawaletea maendeleo ndio sababu kubwa ya Chami kushinda jimbo hilo kwa small margin.

  Ombi langu ni kwa vyama vya upinzani kuanza mchakato mapema wa kutafuta mgombe kwenye jimbo hili la Moshi vijijini na awe ametoka maeneo nilioanisha. Pia ikumbukwe kwenye hili jimbo pia hawaangalii sana itikadi bali deliverance. Angalia miaka 15 vyama 3 tofauti hi hayo tu.
   
 19. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  MBUNGE WETU MOSHI VIJIJINI ACHA KUOGOPA KIVULI CHAKO

  Mh. Sana, Daktari Cyril chami, mbunge mtukufu wa jimbo la moshi vijijini, nakuandikia waraka huu nikiwa na matumaini kuwa utausoma kwa makini na kuulewa badala ya kukurupuka na kumwagiza anayeitwa msaidiizi wako maalumu kunijibu.

  Ninakuandikia kukuonya mapema kuwa mwaka 2010, siyo mbali, kama ukilinganisha na safari ya kutoka moshi kwenda dare s salam mlioianza mwaka 2005, sasa mmeshafika njia panda ya segera. Hivyyo kujidanganya kuwa bado upo muda ni sawa na kumdanganya mt0to kwa pipi ili alale.

  Ninakuandikia nikikkukumbusha kuwa mwaka 2005, ilibidi uongozi wote kitaiifa uhamie moshi vijijini kukunusuru, wananchi waliamua kukupa kura za huruma na kwa bahati mbaya, umeligawa jimbo kwa misingi ya ukabila.

  Wakati wananchi wa uru mawela , wakilalamika kwa ngazi zote kuhusu kudhulumiwa kwa ardhi yao , na majengo waliompangisha mwekezaji aitwaye laitolya tours, kiasi kwamba mwekezaji huyu hataki kulipa kodi ya pango kwa miaka 12 sasa, huku akisaidiwa na baadhi ya viongozi kutengeneza hati miliki hivyo kuwadhulumu wananchi hawa, wewe umekaa kimyaa kabisa, na wala hutaki kujiingiza kwenye mgogoro, labda unafaidi toka kwa mwekezaji au kwako matatizo ya wananchi wa uru hayana nafasi. Huko kibosho unakotoka mgogoro mdogo wa ardhi kati ya wananchi na chuo kule mweka uliufungia safari toka dar es alam ukautatua kwa muda mfupi sana. Mweka ni kama nusu kilomita toka uru mahali ambako wananchi wanavutana na kutishiwa kuuawa na mwekezaji. Nawe ukekaa kimya hali ukijua kama mwekezaji yule angebanwa akalipa kodi anayodaiwa kama 467m, pesa hizo zingetosha kufanya maajabu kieleimu na afya kwa tarafa zima ya uru. Mwekezaji yule anavuna mamilioni kila kukicha na ukweli ni kuwa anao uwezo wa kulipa kiasi hiki, ila kiburi unampa wewe na wenzako huko serikalini.

  Mwaka juzi, uliahidi wananchi wa uru mawela kuwa utamleta balozi wa japan, ambaye angesaidiana kiufadhili na wanachi kujenga kidato cha tano na sita katika shule yetu ya mawela. Kwa masikitiko makubwa ukampeleka kwako kibosho, wakati kule mawela wananchi walikuwa wanakusubiri hadi giza hukutokea! Badala yake baadaye ukawajibu kuwa eti serikali ina mpango wa kujenga shule za kidato cha tano na sita hivyo wasubiri. Ni nani asiyejua kuwa mipango ya serikali inachukua muda mrefu? Kwa nini balozi aende kujenga shule kibosho, na uru wa subiri serikali?

  Mheshimiwa , labda nikukumbushe tu kuwa, barabara ya uru iliahidiwa kuwekewa lami, barabara ile ina urefu wa kilomita 20. naona utapeli umeanza wa kuweka mita 300 kila mwaka, na sasa wako pale rau kama mita 700 toka mjini, hii danganya toto haitawafanya wananchi wa uru waamini kuwa eti unatimiza ahadi. Tunachotaka ni barabara ijengwe yote kilomita 25 kabla ya mwaka 2010, la sivyo hakuna cha ngawaiya kuzunguka na wewe au yeyote kukuombea kura. Mambo ya kudanganywa na rangi za bendera za vyama vya siasa sio uru, mkajaribu mahali pengine.

  Mheshimiwa sana mbunge na waziri. Wananchi wa moshi vijijini hatutaelewa somo lolote kama ahadi zako hazitatimia kuhusu hasa elimu, majji, ajira nakadhalika. Kamwe usihangaike kuandika litania za mambo uliyofanya ukidanganywa na wasaidizi wako, wananchi hawataangalia makaratasi, bali kama ni lami ionekane barabarani, na kama ni maji yaonekane yanatiririka. Ngonjera tulishazichoka

  Mwisho, ni vema nikakuonya mapema, kwani kuna watu wananyemelea jimbo la moshi vijijini. Yeyote aliye tayari kufanya kazi na sisi tunamkaribisha. Hatujali wadhifa ulio nao au kipaji chako cha kufaulu darasani, tunachotaka ni maendeleo na wala siyo litania za sifa.tunazo taarifa kuwa badala ya kukazania kutimiza ahadi unatumia rasilimali ulizo nazo kupambana na wote wanaojitokeza kuwania jimbo hili. Hii haitakusadia sana, san asana itazidi kutuongezea wasiwasi tulio nao dhiidi yako, na uwezo wako wa kujibadilisha kwa siku chache zilizobaki, Ni matumaini yangu kuwa utasoma barua hii kwa makini kwani bado hujachelewa

  Ahsante sana

  Mwikimbi mwitori
  moshi
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Hapa mkuu tupo ukurasa mmoja, ninakumbuka siku moja jinsi nilivyomsaidia sana huyu mbunge somewhere majuu, kununua malori mawili ya Fire kwa ajili ya jimbo lake, akiwa na mtoto wake mmoja wa kike, ambaye ni jaji wa mahakama moja Kibaha, huyu ni lazima ashinde tu na CCM wanajua sana kuwa hilo halina ubishi na wala huwa hawajisumbui,

  Unless ametokea mgombea wao mmoja asiyeelewa na mwenye hela sana, huwa wanamuachia aumie na kumcheka baadaye kwenye private.
   
Loading...