Moshi, kati ya Manispaa Chache Chafu Zaidi Tanzania Bara!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
16,954
Reaction score
26,048
Manispaa ya Moshi iliyopo mkoani. kilimanjaro inayoongozwa na Mbunge wa CCM-Ibrahimu Shayo, Meya wa CCM ndugu Kidumuyo, RC naDC wa CCM ndio manispaa chafu zaidi kwa sasa.

Kipindi CHADEMA wakiwa na mbunge Ndesamburo na Mayor Ray Mboya , ndio manispaa iliyokuwa safi zaidi Tanzania na Afrika Mashariki.

Baada ya Priscus Tarimo , MB wa CCM kuingizwa Madarakani, kijana ambaye kwa asili inasemekana siyo msafi , alianza kwa kushirikiana na Mayor na viongozi wengine by then alikuwa Juma Raibu [aliyejiuzulu kwa kashfa ya ushoga-kuhudhuria hafla ya mashoga] walianza kuchukua maeneo ya wazi, vibali vya ujeni mjini kujenga nyumba za chini, wamachinga kupanga bidhaa popote , na kuua mji kabisa na sasa Moshi imekuwa chafu na kurudisha pale CHADEMA ya Ray Mboya alipoachan itachuyua miaka 15.

BUSTANI PEKEE UHURU PARK: Moshi kuna bustani ambayo ipo Manispaa, ikiitwa Uhuuru PArk, kwanza wakaanza na kuweka vibanda vya mama lishe, ikapunhua ukubwa na wakaweka kiingilio, tena wakaenda mbali zaidi , wakajenga jengo la mghahawa akakodisha kampuni ya MIMOSA na kushindwa biashara sasa amepewa ALTEZZA Tours, hii ni kampuni ya MRusi japo hajaanza biashara.

MANISPAA kwa akili yao, wameanza kujenga ukuta kuweka maduka kwenye hiyo garden, menas mtu akipita itakuwa haionekani , wanashindwa kujifunzwa kwa Dar es salaam kwani jijin lilishindwa kuweka maduka kuzunguka mnazi mooja, tena pale fremu ingekuwa ziaidiu ya milioni kodi kwa mwezi lakini ieahwa ionekani na mji upumulie hapo, sasa hiyop garden ya kuweka fremu mtu ataenda kupumzika garden ama itakuwa kusikiliza makelele garden?
 
Moshi Manispaa: Maswali ya Uwajibikaji Yanayohitaji Majibu ya Haraka
Moshi Manispaa imekuwa ikikabiliwa na malalamiko na maswali mengi kutoka kwa wananchi kuhusu usimamizi wa fedha za umma, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uwazi katika matumizi ya rasilimali za walipa kodi.
Miongoni mwa masuala yanayoibua maswali ni:
Mradi wa Uwanja wa Majengo unaodaiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 2. Wananchi wanahitaji maelezo ya kina kuhusu gharama halisi za mradi huo, hatua za utekelezaji na thamani ya fedha iliyotumika.
Bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya. Umma una haki ya kujua madarasa hayo yamejengwa katika maeneo gani, yamegharimu kiasi gani na yamefikia hatua gani.
Kumekuwa na madai na hisia za wananchi kuhusu uwepo wa usimamizi usioridhisha wa fedha za halmashauri. Madai hayo yanahitaji uchunguzi wa kitaalamu na wa kina ili ukweli ujulikane.
Aidha, yapo malalamiko kuhusu mfumo wa utendaji ndani ya halmashauri, ikiwemo madai ya ukosefu wa uwiano katika uteuzi wa viongozi wa idara na vitengo pamoja na hoja kuhusu uwezo wa baadhi ya watendaji kusimamia majukumu yao kwa ufanisi. Haya ni masuala yanayopaswa kutazamwa kwa misingi ya utendaji, weledi, uwazi na maslahi ya umma.
Wananchi pia wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kuhusu utendaji wa baadhi ya viongozi wa halmashauri, hususan katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, matumizi ya fedha za umma na michango mbalimbali inayokusanywa kutoka kwa watumishi au wananchi. Endapo yapo malalamiko yenye ushahidi, ni muhimu vyombo husika vifanye uchunguzi wa kina.
Hatari ya TISS na TAKUKURU Kushindwa Kuchukua Hatua
Iwapo taasisi za dola kama Tanzania Intelligence and Security Service (TISS) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) zitashindwa kufuatilia kwa haraka malalamiko yanayoibuliwa na wananchi, madhara yake yanaweza kuwa makubwa:
Kupungua kwa imani ya wananchi kwa Serikali na taasisi zake.
Kuongezeka kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji.
Kudhoofika kwa utoaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya na miundombinu.
Kuongezeka kwa malalamiko, migogoro na hisia za kutotendewa haki miongoni mwa wananchi.
Kuzuia maendeleo ya Manispaa kwa sababu fedha zinazopaswa kuwaletea wananchi maendeleo zinaweza kutotumika ipasavyo.
Wananchi wa Moshi Manispaa wanahitaji majibu, uwazi na hatua za kisheria pale ambapo kuna viashiria vya ukiukwaji wa sheria au matumizi mabaya ya fedha za umma. Uchunguzi huru, ukaguzi wa kina wa miradi na uwajibikaji wa viongozi wote bila upendeleo ndiyo njia bora ya kurejesha imani ya wananchi na kuhakikisha fedha za walipa kodi zinatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.
 
Maswali ya Msingi hapa. Moshi ilikuwa Munispaa inayoongoza kwa usafi kwa kipindi cha nyuma kwa muda wa miaka 10. Ilikuwa ukikaribia Moshi kila mtu alikuwa anaheshimu kutupa taka ovyo..kulinda maeneo ya wazi, mpangilio wa maeneo ya biashara etc. Kwa sasa inasemekana wamerudi nyuma. sasa wanahitaji kujifunza kupitia wilaya nyingine. Nini tatizo?
 
Moshi ipi ndugu yangu mimi niko hapa sasa hivi
Moshi yote ni kama jalala. Nenda tu hapo YMCW uone palivyojaa mabanda kama kwa Mtogole..then pandisha hiyo njia ya KCMC ulivyo panavyotia kinyaa

Ukimaliza nenda kazunhuke soko la Memorial uone kulivyo hivyo na ukimaliza kaangalia garden wajinga wanajenga vibanda vya maduka.
 
Moshi Manispaa: Maswali ya Uwajibikaji Yanayohitaji Majibu ya Haraka
Moshi Manispaa imekuwa ikikabiliwa na malalamiko na maswali mengi kutoka kwa wananchi kuhusu usimamizi wa fedha za umma, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uwazi katika matumizi ya rasilimali za walipa kodi.
Miongoni mwa masuala yanayoibua maswali ni:
Mradi wa Uwanja wa Majengo unaodaiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 2. Wananchi wanahitaji maelezo ya kina kuhusu gharama halisi za mradi huo, hatua za utekelezaji na thamani ya fedha iliyotumika.
Bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya. Umma una haki ya kujua madarasa hayo yamejengwa katika maeneo gani, yamegharimu kiasi gani na yamefikia hatua gani.
Kumekuwa na madai na hisia za wananchi kuhusu uwepo wa usimamizi usioridhisha wa fedha za halmashauri. Madai hayo yanahitaji uchunguzi wa kitaalamu na wa kina ili ukweli ujulikane.
Aidha, yapo malalamiko kuhusu mfumo wa utendaji ndani ya halmashauri, ikiwemo madai ya ukosefu wa uwiano katika uteuzi wa viongozi wa idara na vitengo pamoja na hoja kuhusu uwezo wa baadhi ya watendaji kusimamia majukumu yao kwa ufanisi. Haya ni masuala yanayopaswa kutazamwa kwa misingi ya utendaji, weledi, uwazi na maslahi ya umma.
Wananchi pia wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kuhusu utendaji wa baadhi ya viongozi wa halmashauri, hususan katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, matumizi ya fedha za umma na michango mbalimbali inayokusanywa kutoka kwa watumishi au wananchi. Endapo yapo malalamiko yenye ushahidi, ni muhimu vyombo husika vifanye uchunguzi wa kina.
Hatari ya TISS na TAKUKURU Kushindwa Kuchukua Hatua
Iwapo taasisi za dola kama Tanzania Intelligence and Security Service (TISS) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) zitashindwa kufuatilia kwa haraka malalamiko yanayoibuliwa na wananchi, madhara yake yanaweza kuwa makubwa:
Kupungua kwa imani ya wananchi kwa Serikali na taasisi zake.
Kuongezeka kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji.
Kudhoofika kwa utoaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya na miundombinu.
Kuongezeka kwa malalamiko, migogoro na hisia za kutotendewa haki miongoni mwa wananchi.
Kuzuia maendeleo ya Manispaa kwa sababu fedha zinazopaswa kuwaletea wananchi maendeleo zinaweza kutotumika ipasavyo.
Wananchi wa Moshi Manispaa wanahitaji majibu, uwazi na hatua za kisheria pale ambapo kuna viashiria vya ukiukwaji wa sheria au matumizi mabaya ya fedha za umma. Uchunguzi huru, ukaguzi wa kina wa miradi na uwajibikaji wa viongozi wote bila upendeleo ndiyo njia bora ya kurejesha imani ya wananchi na kuhakikisha fedha za walipa kodi zinatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.
UFISADI WA WAZI WA MOSHI MV:
1. Ujeni wa stendi Nganga- Mfumuni
2. Ujenzi wa Ukuuta wa Manispaa.
3, Ujenzi wa Uwanja wa Majengo.

Katika kutoa tenda na ujenzi huo, Watu wamenunua mabasi -Eicher, Coaster na Wengine wamejenga , namaanisha viongozi wa Kipindi cha 2015-2025 , Pale Karibu na TRA kuna mtu mmoja alikuwa Meya kachukkua kile Kiambusa, na mengine mengi, wacha Moshi if kabisa maana wenye akili wameamua kuwa machawa.
 
Hivyo hata sisi kilwa pamepazidi Moshi usafi
Usilinganishe Kilwa na Moshi, Ukiambiwa pahala pachafu elewa mji umekuwa kama Banda la nguruwe.
Kilwa ni safi sana, mitaa ya Kisiwani, Magomeni,Kilwa ,Masoko,Somanga,Kipatimu,Kibata,Nanjirinji,Miguruwe,Mandawa,Njinjo,Songosongo,Chumo ni kusafi sana.
 
Hii hali ya uchafu iliyo pitiliza ni mbaya kwakweli Yan kama huku kuanzia njianpanda Hadi himo ni kuchafu sana
 
Ninaamini huko baadaye watabadilika la sivyo wataishia kuwa Wantam. Maana Moshi ni ngumu sana kuvumilia watendaji wabovu. Cha msingi wabadilike wairudishe Moshi ilipokuwa. Moshi kwa sasa imezidiwa hata na Bunda kwa usafi na mpangilio wa vitu.
 
Back
Top Bottom