Wana CCM Wajipanga Kuikomboa Moshi Mjini

Hapa mkuu tupo ukurasa mmoja, ninakumbuka siku moja jinsi nilivyomsaidia sana huyu mbunge somewhere majuu, kununua malori mawili ya Fire kwa ajili ya jimbo lake, akiwa na mtoto wake mmoja wa kike, ambaye ni jaji wa mahaka Kibaha, huyu ni lazima ashinde tu na CCM wanajua sana kuwa hilo halina ubishi na wala huwa hawajisumbui,

Unless ametokea mgombea wao mmoja asiyelewa na mwenye hela sana, huwa wanamuachia na kumchela baadaye kwenye private zao.

Mkuu,

Nakuambia CCM nao huwa wana vituko,kwa mfano 2005 nilikua kule wakati wa Kampeni.Yaani nakuambia walikufuru kwa kumwaga hela,watu wanakodisha baa nzima ni pombe na mbuzi choma tu na mziki mnene.

Kesho yake karibu na eneo hilo hilo Ndesa akaingia,akamwaga sera huku watu wakimuita Mbunge mtarajiwa.

Nikajifunza kuwa CCM humwaga hela bila back up ya hoja,unakuta watu wana-concetrate kwenye mlo tu lakini anything to do na kupigia kura hyo next month ni ajenda nyingine.Kwa kweli niliwasifu sana wapiga kura wa huko maanke that's the only way ya kuwafundisha mafisadi kuwa pesa zao ni laana siku zote
 
MBUNGE WETU MOSHI VIJIJINI ACHA KUOGOPA KIVULI CHAKO

Mh. Sana, Daktari Cyril chami, mbunge mtukufu wa jimbo la moshi vijijini, nakuandikia waraka huu nikiwa na matumaini kuwa utausoma kwa makini na kuulewa badala ya kukurupuka na kumwagiza anayeitwa msaidiizi wako maalumu kunijibu.

Ninakuandikia kukuonya mapema kuwa mwaka 2010, siyo mbali, kama ukilinganisha na safari ya kutoka moshi kwenda dare s salam mlioianza mwaka 2005, sasa mmeshafika njia panda ya segera. Hivyyo kujidanganya kuwa bado upo muda ni sawa na kumdanganya mt0to kwa pipi ili alale.

Ninakuandikia nikikkukumbusha kuwa mwaka 2005, ilibidi uongozi wote kitaiifa uhamie moshi vijijini kukunusuru, wananchi waliamua kukupa kura za huruma na kwa bahati mbaya, umeligawa jimbo kwa misingi ya ukabila.

Wakati wananchi wa uru mawela , wakilalamika kwa ngazi zote kuhusu kudhulumiwa kwa ardhi yao , na majengo waliompangisha mwekezaji aitwaye laitolya tours, kiasi kwamba mwekezaji huyu hataki kulipa kodi ya pango kwa miaka 12 sasa, huku akisaidiwa na baadhi ya viongozi kutengeneza hati miliki hivyo kuwadhulumu wananchi hawa, wewe umekaa kimyaa kabisa, na wala hutaki kujiingiza kwenye mgogoro, labda unafaidi toka kwa mwekezaji au kwako matatizo ya wananchi wa uru hayana nafasi. Huko kibosho unakotoka mgogoro mdogo wa ardhi kati ya wananchi na chuo kule mweka uliufungia safari toka dar es alam ukautatua kwa muda mfupi sana. Mweka ni kama nusu kilomita toka uru mahali ambako wananchi wanavutana na kutishiwa kuuawa na mwekezaji. Nawe ukekaa kimya hali ukijua kama mwekezaji yule angebanwa akalipa kodi anayodaiwa kama 467m, pesa hizo zingetosha kufanya maajabu kieleimu na afya kwa tarafa zima ya uru. Mwekezaji yule anavuna mamilioni kila kukicha na ukweli ni kuwa anao uwezo wa kulipa kiasi hiki, ila kiburi unampa wewe na wenzako huko serikalini.

Mwaka juzi, uliahidi wananchi wa uru mawela kuwa utamleta balozi wa japan, ambaye angesaidiana kiufadhili na wanachi kujenga kidato cha tano na sita katika shule yetu ya mawela. Kwa masikitiko makubwa ukampeleka kwako kibosho, wakati kule mawela wananchi walikuwa wanakusubiri hadi giza hukutokea! Badala yake baadaye ukawajibu kuwa eti serikali ina mpango wa kujenga shule za kidato cha tano na sita hivyo wasubiri. Ni nani asiyejua kuwa mipango ya serikali inachukua muda mrefu? Kwa nini balozi aende kujenga shule kibosho, na uru wa subiri serikali?

Mheshimiwa , labda nikukumbushe tu kuwa, barabara ya uru iliahidiwa kuwekewa lami, barabara ile ina urefu wa kilomita 20. naona utapeli umeanza wa kuweka mita 300 kila mwaka, na sasa wako pale rau kama mita 700 toka mjini, hii danganya toto haitawafanya wananchi wa uru waamini kuwa eti unatimiza ahadi. Tunachotaka ni barabara ijengwe yote kilomita 25 kabla ya mwaka 2010, la sivyo hakuna cha ngawaiya kuzunguka na wewe au yeyote kukuombea kura. Mambo ya kudanganywa na rangi za bendera za vyama vya siasa sio uru, mkajaribu mahali pengine.

Mheshimiwa sana mbunge na waziri. Wananchi wa moshi vijijini hatutaelewa somo lolote kama ahadi zako hazitatimia kuhusu hasa elimu, majji, ajira nakadhalika. Kamwe usihangaike kuandika litania za mambo uliyofanya ukidanganywa na wasaidizi wako, wananchi hawataangalia makaratasi, bali kama ni lami ionekane barabarani, na kama ni maji yaonekane yanatiririka. Ngonjera tulishazichoka

Mwisho, ni vema nikakuonya mapema, kwani kuna watu wananyemelea jimbo la moshi vijijini. Yeyote aliye tayari kufanya kazi na sisi tunamkaribisha. Hatujali wadhifa ulio nao au kipaji chako cha kufaulu darasani, tunachotaka ni maendeleo na wala siyo litania za sifa.tunazo taarifa kuwa badala ya kukazania kutimiza ahadi unatumia rasilimali ulizo nazo kupambana na wote wanaojitokeza kuwania jimbo hili. Hii haitakusadia sana, san asana itazidi kutuongezea wasiwasi tulio nao dhiidi yako, na uwezo wako wa kujibadilisha kwa siku chache zilizobaki, Ni matumaini yangu kuwa utasoma barua hii kwa makini kwani bado hujachelewa

Ahsante sana

Mwikimbi mwitori
moshi

Dr Chami, alikuwa mwana Tanzanet wa siku nyingi. Wasomi wetu wengi waliokuwa mabingwa wa kuongea kwenye vijiwe wakiwa nje, wanachemsha kweli kweli wakifika Tanzania.

Akina Mtanzania, Mkandara, Rev. Kishoka, FMES, Mzee Mwanakijiji, Kitila na wengine, jiandaeni mkirudi TZ, msije mkaishia kundi la akina Dr. Chami, Dr. Msekela, Dr. Kamala, na wengine.

Wengine tunatunza makabrasha yenu tu ili mkianza kufanya tofauti tuweze kuyafungua. Wengine yetu macho na masikio! kwi kwi kwi!!!
 
Dr Cahami, alikuwa mwana Tanzanet wa siku nyingi. Wasomi wetu wengi waliokuwa mabingwa wa kuongea kwenye vijiwe wakiwa nje, wanachemsha kweli kweli wakifika Tanzania.

Akina Mtanzania, Mkandara, Rev. Kishoka, FMES, Mzee Mwanakijiji, Kitila na wengine, jiandaeni mkirudi TZ, msije mkaishia kundi la akina Dr. Chami, Dr. Msekela, Dr. Kamala, na wengine.

Wengine tunatunza makabrasha yenu tu ili mkianza kufanya tofauti tuweze kuyafungua. Wengine yetu macho na masikio! kwi kwi kwi!!!

Mkuu Mtanzania,

Heshima nawe,more respect kwa kukumbushia hili mkuu.But my worry ni kwamba how are you going to identify them? most of us and may be be except Mr.Kitila huwa tunatumia nicknames,utawajua kweli?
 
Ben,

Hivi wewe huwajui? Kwi kwi kwi!!!

Bahati nzuri hao wote niliowataja hapo juu mimi nawajua, ila siwezi kutoa siri hata ukinipa
EPA yote.

Nikiona na wewe unakaribia kuchukua form ya CHADEMA nitakujua tu mkuu.

Any way JF hatutakiwi kutafutana kujuana majina. Vinginevyo mtafute Jasusi atakuambia Mtanzania ni nani.
 
mimini mpiga kura wa hili jimbo

napenda kuwahakikishia cyril harudi kwani hajafanya lolote. Pili mgombea yeyote atakae toka sehemu za kibosho kwa ujumla awe ccm ama chadema et.al kwani wabunge wote waliopita baada ya mrema wametoka huko na hakuna walichofanya (ngotolainyo, chami na ngawaiya)
hata kikwete aliambiwa wakati wa kampeni 2005 akishindwa watamfukuza na itakuwa zamu ya uru na old moshi kutoa mmbunge regardless ya chama.

Pia wauru na oldimoshi wanakura zaidi ya 65% ya jimbo zima so wanaouwezo wa kutoa mmbunge. Nilikua huko miezi michache iliyopita na wazee kwa vijana wamesema imetosha.

Kikwete aliwaahidi mmbunge wao atakuwa waziri hivyo atawaletea maendeleo ndio sababu kubwa ya chami kushinda jimbo hilo kwa small margin.

Ombi langu ni kwa vyama vya upinzani kuanza mchakato mapema wa kutafuta mgombe kwenye jimbo hili la moshi vijijini na awe ametoka maeneo nilioanisha. Pia ikumbukwe kwenye hili jimbo pia hawaangalii sana itikadi bali deliverance. Angalia miaka 15 vyama 3 tofauti hi hayo tu.

ukinikumbusha ngotolainyo nasikia kichefuchefu maana hata jina lake halieleweki lakini huyu ni msambaa hana neno
 
Ben,

Hivi wewe huwajui? Kwi kwi kwi!!!

Bahati nzuri hao wote niliowataja hapo juu mimi nawajua, ila siwezi kutoa siri hata ukinipa
EPA yote
.

Nikiona na wewe unakaribia kuchukua form ya CHADEMA nitakujua tu mkuu.

Any way JF hatutakiwi kutafutana kujuana majina. Vinginevyo mtafute Jasusi atakuambia Mtanzania ni nani.

Mkuu wangu,

Hata mkuu Jasusi nae atataka Chupa ya John Walker! Teh teh teh.

Ha ha ha,mkuu hapo nilipo-bold nako unaniua mkuu,unajua leo ni Jumatatu tu?
 
Upinzani usilale, hawa vijana wa CCM kina Chami et al hawana kipya chochote zaidi ya kufuata upepo dawa ni kuwang,oa wote. Kuna rafiki yangu kaniambia bosi wake ameletewa kadi ya mchango wenye lengo la kmng'oa Dk Slaa Karatu. Nilijaribu kupata moja ila sikufanikiwa, inaelekea mafisadi wameanza kijipanga mapema.
 
Kwamba Moshi Mjini wanataka kumng'oa mzee Ndesa nafikiri hiyo ni ndoto tena ya mchana. Huyu mzee amejengea uzio makaburi makubwa ya kata ya Pasua, Kata ya Kaloleni na kata ya Majengo kwa hela yake. Kanunua ambulance mbili, kawanunulia wamachinga soko la kisasa kwa TSH 160,000,000/=, alikwishawahi kuzuia wanachuo 72 wa TUmaini University waliokuwa wanadaiwa ada wasirudishwe nyumbani kwa kutoa 10,000,000/=. Ofisi yake ni kama kliniki ambako watu hawaishi kwenda kutoa shida zao binafsi na kusaidiwa. Amefungua SACCOS 8 mjini Moshi.

Ninachojua kuhusu huyu mzee ni kuwa ana uwezo wa hali ya juu wa kuwafanyia timing CCM. Huyu mzee ni mjanja sana.

CCM wasahau kumng'oa Moshi Mjini.
 
Labda jimbo lingine au Mzee NDESA asigombee,mbona hata 2005 walichanga hela za kumngoa lakini hamna kitu
 
Belo,
Do not underestimate these thugs. Kumwondoa sio lazima iwe through the ballot. Haya majambazi yamekwisha pofushwa na ulafi so they can do anything. Just think of Tarime.
 
Kwamba Moshi Mjini wanataka kumng'oa mzee Ndesa nafikiri hiyo ni ndoto tena ya mchana. Huyu mzee amejengea uzio makaburi makubwa ya kata ya Pasua, Kata ya Kaloleni na kata ya Majengo kwa hela yake. Kanunua ambulance mbili, kawanunulia wamachinga soko la kisasa kwa TSH 160,000,000/=, alikwishawahi kuzuia wanachuo 72 wa TUmaini University waliokuwa wanadaiwa ada wasirudishwe nyumbani kwa kutoa 10,000,000/=. Ofisi yake ni kama kliniki ambako watu hawaishi kwenda kutoa shida zao binafsi na kusaidiwa. Amefungua SACCOS 8 mjini Moshi.

Ninachojua kuhusu huyu mzee ni kuwa ana uwezo wa hali ya juu wa kuwafanyia timing CCM. Huyu mzee ni mjanja sana.

CCM wasahau kumng'oa Moshi Mjini.
tatizo ni kuwa amezeeka sana ana hana uwezo wa kujimudu yeye binafsi wala kazi ya ubunge.nimemuona kama mwezi mmoja ata kutembea hawezi.
 
Kwamba Moshi Mjini wanataka kumng'oa mzee Ndesa nafikiri hiyo ni ndoto tena ya mchana. Huyu mzee amejengea uzio makaburi makubwa ya kata ya Pasua, Kata ya Kaloleni na kata ya Majengo kwa hela yake. Kanunua ambulance mbili, kawanunulia wamachinga soko la kisasa kwa TSH 160,000,000/=, alikwishawahi kuzuia wanachuo 72 wa TUmaini University waliokuwa wanadaiwa ada wasirudishwe nyumbani kwa kutoa 10,000,000/=. Ofisi yake ni kama kliniki ambako watu hawaishi kwenda kutoa shida zao binafsi na kusaidiwa. Amefungua SACCOS 8 mjini Moshi.

Ninachojua kuhusu huyu mzee ni kuwa ana uwezo wa hali ya juu wa kuwafanyia timing CCM. Huyu mzee ni mjanja sana.

CCM wasahau kumng'oa Moshi Mjini.

Kumbe ubunge maana yake ni ufadhili? sikujua kuwa mbunge mzuri ni yule anaetoa pesa mfukoni mwake.
 
mimini mpiga kura wa hili Jimbo

Napenda kuwahakikishia Cyril Harudi kwani hajafanya lolote. Pili mgombea yeyote atakae toka sehemu za kibosho kwa ujumla awe ccm ama chadema et.al kwani wabunge wote waliopita baada ya Mrema wametoka huko na hakuna walichofanya (Ngotolainyo, Chami na Ngawaiya)
Hata Kikwete aliambiwa wakati wa Kampeni 2005 akishindwa watamfukuza na itakuwa zamu ya URU na Old moshi kutoa mmbunge regardless ya chama.

Pia wauru na oldimoshi wanakura zaidi ya 65% ya jimbo zima so wanaouwezo wa kutoa mmbunge. Nilikua huko miezi michache iliyopita na wazee kwa vijana wamesema imetosha.

Kikwete aliwaahidi mmbunge wao atakuwa waziri hivyo atawaletea maendeleo ndio sababu kubwa ya Chami kushinda jimbo hilo kwa small margin.

Ombi langu ni kwa vyama vya upinzani kuanza mchakato mapema wa kutafuta mgombe kwenye jimbo hili la Moshi vijijini na awe ametoka maeneo nilioanisha. Pia ikumbukwe kwenye hili jimbo pia hawaangalii sana itikadi bali deliverance. Angalia miaka 15 vyama 3 tofauti hi hayo tu.

Alisema atatoa ajira ni mmasy wa vodacom, hakuna ubaya wowote kama ataweza kummondoa cyril chami, huyu mtu ni mzigo kwa wanachi wa moshi vijijini hakuna lolote alilofanya zaidi ya kujisifu eti alikuwa na phd first class, pia ni mkabila wa kutupwa, yeye anadhani kuwa mbunge ni kutetea maslahi ya wakibosho wenzake, huku wa-uru akiwabagua wazi wazi

Leeelelelee ambaa!
 
Kumbe ubunge maana yake ni ufadhili? sikujua kuwa mbunge mzuri ni yule anaetoa pesa mfukoni mwake.

Au mbunge mzuri ni yule aliye fisadi, asiyejali maisha ya wapigakura wake?

Bw. Masatu kwa hili - kajifikirie upya!
 
lazima uwe na definition nzuri ya neno kukomboa, ukiweka jimbo chini ya himaya ya mafisadi unaita huo ni ukombozi? au wewe unatumia ukombozi hapa kwa maana ipi?
 
Back
Top Bottom