backbenchers
Member
- May 9, 2024
- 59
- 30
Kero hizi zinazidi kila siku kwasababu mbili kubwa:
1. Wafanyabiashara wadogowadogo kuweka bidhaa zao sehemu zilizotengwa kwa maegesho ya magari. Hii ipo sana kwenye soko la Manyema, kwenye soko la M'buyuni kuna barabara ya magari imefungwa kabisa na wafanyabiashara wadogowadogo ambayo haiwezi kupitika hata kwa pikipiki kirahisi.
2. Madereva wa bajaji hususani bajaji zinazoelekea eneo linaloitwa Shabaha kubadili eneo ya maegesho kuwa stendi bubu ya bajaji zao. Hii ipo sana kwenye soko la M'buyuni.
Swali langu nalielekeza kwa viongozi wa masoko ya M'buyuni na Manyema, mkurugenzi wa manispaa ya Moshi mjini, hvi jamani hii kero nyie hamuioni au labda kwenu nyie hii sio kero? Watu tutaegesha wapi magari yetu wakati wa.kwenda masokoni kama maeneo yakuegesha magari kumevamiwa na wafanyabiashara wadogowadogo na madereva wa bajaji?