Kiatu cha udongo
JF-Expert Member
- Jun 28, 2022
- 443
- 1,158
Mikopo mikubwa + nidhamu ya hela
Mchango wako una hadhi ya nyota tanoWatu wengi ni masikini kwa sababu kuu tatu
1-Ujinga - kutokujua jinsi gani ulimwengu wa pesa unavyofanya kazi. Wengi tumekuzwa katika mfumo wa "shule"...soma nursery, mpaka A-level then omba mkopo go to UNIVERSITY ...ukimaliza tembeza bahasha kuomba ajira serikalini, ukishapata unaanza kulipa mkopo kwa miaka zaidi ya 15 huku ukiishi maisha ya mshahara mwezi mpaka mwezi..ukija kustuka umri wa kustaafu ushafika huna cha maana ulichokifanya. Leo hii tajiri akipaki ndinga lake hutasikia masikini wakisema kuwa jamaa kasoma sana yule ndio maana kafika pale alipo,maneno utakayoyasikia ni jamaa ni drug dealer, fisadi,jambazi, amewatoa kafara wazee wake, freemasoj n.k
2-Uvivu - hapa unatakiwa uelewe kuwa ili ufike kwenye utajiri basi jua kuwa unashindana na kundi kubwa la watu katika kuisaka pesa, matajiri huwa hawalali, muda wote wanaisaka pesa ilipo tofauti na wafanyakazi wa serikalini unaingia kazini saa 2 na nusu unatoka saa 9 ukitoka unakwenda kulala nyumbani, ukisubiri kesho ifike.Matajiri muda wote wapo macho tembea barabarani usiku uone malori yao yanavyoingiza pesa, miradi yao inaingiza pesa masaa 24 bila kupumzika ila masikini hufanya kazi kwa muda mchache tu .
3-Kiburi - ujuaji unafanya watu wengi kubaki katika umasikini. Ili uwe dereva mzuri ni lazima ufundishwe na mkufunzi mzuri...mfano mtu utakwenda VETA au NIT ili uive katika fani ya udereva, vivyo hivyo huwezi kuwa tajiri kama upo mbali na matajiri, huwezi kuwa tajiri kama hujakaa chini na waliokutangulia katika utajiri ukapata misingi ya nini ufanye kuelekea katika njia ya utajiri. Masikini wengi ni wajuaji, wanaridhika kuwa wao wanajua nini wafanye matokeo yake wanaendelea kubaki katika umasikini. Kaa karibu na uwaridi ili upate kunukia au fuata nyuki upate asali. Tusiwe viburi kujifunza kwa matajiri.
Pia fisadi ni mtu ambaye shule anayo ya kutosha. Wale kuwafunga ni ngumu mno kwasababu wizi wao ni wa kisomi. Utakuta zimeibwa hela nyingi lakini wanaokamatwa ni vidagaa. Fisadi liko tu ila ushahidi wa kumtia hatiani hauonekani.
Kuwa fisadi inabidi uwe very smart na uwe kwenye inner circle ya CCM na uwe na very heavy connection na watu wazito. Na ujue kutunza SIRIExactly. Watu wanadhani kuwa fisadi ni ngekewa, inabidi uwe smart to be in that position.
Jah man?Kama yule Mbunge wa Makambako nasikia ana Malori kama 300 hivi
Jipe moyo tu mkuuWachache wamezipata kihalali. Jiulize haya mabilioni yanayopigwa serikalini huwa yanaenda wapi? Mfano mabilioni ya ndege yaliyopigwa yamepelekwa wapi... mimi kwa upande wangu naona ufisadi huwa unawanufaisha sana hawa watu.
Hata wewe mchumi mwenzangu unahoji hivi?...Yani hill swali kila siku nikipita hapa maeneo ta shekilango huwa najiuliza nakosa jibu,Jana nimeona Haya mabasi ya BM kama 20 hivi-hawa watu walifanya kitu gani hadi wakapata hizo hela.
Hamna pesa za uchawi... ndo mnavyojidanganyaga?... pesa inapatikana kwa kufanya kazi, hayo mengine ni mboyoyo....Kuna pesa za majini, kafara, wizi,magendo,zari mfano kwenye madini, ufsadi serikalini
Mkuu unaweza kukubaliana nawe kwa sehemu Fulani but in reality sio kweli watu wengi kwenye pesa ni hawa politician na wengi 99% sio waaminifu hata punje.Pambana,Pambana anza na kujenga uaminifu kwa waliokuzunguka.
Baba yangu hakunipa mtaji (pesa) wa maisha zaidi ya ELIMU.
na kingine siku 1 aliniambia,Unaenda huko duniani Mtaji wako mkubwa ili ufanikiwe ni UAMINIFU kwa waliokuzunguka.
KUWA MWAMINIFU hata kama huna kitu sasa,epuka kuchukua cha mtu fanya kazi kwa bidiii ukipewa 10,000 ukatumwa kitu cha 1000 ukaenda ukakuta kile kitu kinauzwa 500 usibanie ile 500 rudisha chenchi 9500 kisha mwambie aliekutuma Bidhaaa imeshuka bei chenchi hii hapa.
Kweli yako iwe Kweli na Hapana yako iwe Hapana.
Ukiaminika na waliokuzunguka, Ni sifa namba 1 ya kutoka kimaisha huitaji kuwa na kipande cha Ardhi, huitaji kuwa na Pesa.
UKIAMINIKA wewe ni Tajiri hata kama unajiona huna kitu sasa lakini kama kuna mtu akiwaza kumtuma mtu kitu mahali akili yake inakufikiria wewe ndie mtu sahihi (Umemaliza mwaisa).
Mkuu I know its about saving,credit & investment but kila nikipiga hesabu hazi tally kabisa.Hata wewe mchumi mwenzangu unahoji hivi?...
Ina maana umesahau wealth creation inavyofanya kazi
Ah aha a ha a safi Sana Kwa kuwaza hilo bwana Hivi punde .Imagine, kuna haya mabasi
Ester Luxury
Tilisho
Happy Nation
Sauli
New Force
Arusha Express
Shabiby
Abood
Machame Express
Kapricon
Kilimanjaro Express
Dar Express
Zube
Saratoga
Mgamba
Kimbinyiko
Abc
Ally's
Saibaba
etc etc
Malori ndo usiseme.
Unakuta mtu ana basi 10, 20 au 60. Basi moja bei yake ni Milion 300, 400 hadi 500. Jamaa wanapata wapi hela aisee?
[emoji3][emoji3][emoji3]Mbona hao wa viwango vya juu?...Mimi hapa nawaza nitapata hata ist wapi, au nitaanzaje biashara ya kunipatia 10,000 kwa siku....na type hii sms nikiwa kigoma vijijini.
Siyo kuliona tu hadi video tulirekodi Kama hazitaleta shida nizipost humu, hili tukio lilitokea Mata ninaoishi na huyo mzee anajulikana kwa makafaraHilo joka wewe uliliona na uliona police wanazuia watu wasiliue? au story tuu, dogo hakuna shortcut ya mafanikio zaidi ya hardwork na kama unataka kufa maskini amini huo upuuzi
Akili ya mtanzania itaishia hapa tu akiona mtu ana pesa mingiKuna pesa za majini, kafara, wizi,magendo,zari mfano kwenye madini, ufsadi serikalini
Kuwa fisadi inabidi uwe very smart na uwe kwenye inner circle ya CCM na uwe na very heavy connection na watu wazito. Na ujue kutunza SIRI
Kuna siri kubwa sana nyuma ya umiliki wa mali ktk hizi nchi zetu masikini. Sehemu kubwa ya fedha zimewekwa na wanasiasa walioiba pesa za kodi tunazolipa sisi raia wa kawaida. Baadhi ya hao wafanyabiashara wao ni figurehead tu.Kwa kweli Mimi nimepanga kwenda kumuuliza tajiri mmoja yani yeye alifanyaje hadi akaweza kumiliki kuanzia Milioni 500.
Nimeamua nitumie njia yoyote ile kupata hela kwa kweli.