Anayemiliki mabasi ya Kilimanjaro ni Tajiri wa ajabu kweli kweli

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
534
1,751
Hii kampuni nimewaungisha sana lakini kwa sasa nataka kuwakimbia.

Tajiri ana mabasi ambayo yana namba A yapo barabarani yamechakaa.

Hata ile ajali ya Mbeya, juzi inasemekana uchakavu wa gari nao ni chanzo kikubwa.

Tajiri hanunui gari mpya anavizia wenzake wafilisike or magari yao yachoke kisha anayanunua kwa bei rahisi kisha anayapeleka gereji yake anayachomelea na kuyapiga rangi kisha anayaweka barabarani anayaita luxury.

Mfano ni zile gari za Dar Lux kazinunua kazipiga rangi kisha akaweka engine za Scania , akazileta barabarani ila cha kushangaza yale magari yana AC juu ila ukipanda ni joto kwa kwenda mbele hamna AC mule ni janja janja.

Magari ya Kilimanjaro baadhi yameshachoka, mengine hadi ndani kuna harufu ya uvundo lakini mmiliki anajidani anatoa huduma za kisasa.

Ni muda muafaka kwa wamiliki wa hii kampuni wakiona ubahili kununua Scania mpya basi wamgeukie mchina la sivyo hii kampuni tutaikimbia soon.

Angalia matajiri wengine kama Nacharo na Sauli. Sauli alianza na gari chache juzi kanunua Marco polo mpya kaweka barabarani.

Juzi Nacharo ya Tanga baada ya kucheza na mchina kwa kipindi kifupi juzi kanunua gari mpya za marcopolo scania kweka barabarani.

Na siku hizi makampuni ya kuunda mabasi kama una kampuni kubwa unachukua magari na unalipa kwa awamu sijui anakwama wapi.

====================
====================

Nimeona watu humu wanamtetea Bwana sawaya kuwa kama vipi nipande gari lingine wengine wanasema bila ubahili wa sawaya angeshafilisika zamani so kwa biashara ya kuendelea na gari mbovu ndio atadumu sokoni

Hivi niwaulize Abood bus,Ratco,Raha leo,Tashriff,Shabiby,super feo, Dar express,Allys ambao ni wakongwe kwenye game na wana gari mpya barabarani ni wajinga?

Lengo la uzi huu ni Sawaya aache tabia ya kuwakatia watu ticket akiwadanganya kuwa gari ni luxury alafu watu wanakuja kushtukia sio luxury anafanya makosa
 
mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
625
1,237
Hii kampuni niliizika Rasmi na kuachana nayo pindi Tu TAHMEED alivoanza Arusha>Dar,,Kilimanjaro wajanja wajanja wana jina kubwaa ila kazi hamnaaa.....BM kaja na operation maalum na amelikamata soko tayari Ni Muda wa Kimanjaro Exp kujitafakarii mwenzie Dar Express kasanuka kahamia kwa wachina
 
Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
2,498
5,458
Mi bado nawaungisha maana wakati wa kula wanakusubiri umalize chakula restaurant siyo wale wengine eti kula na kuchimba dawa dk10. Abiria anahaha kwenda kukata gogo, haijakaa sawa anaambiwa chakula elfu 8 chakula chenyewe kidogo kama cha boarding halafu mbiyo kwenye gari.
 
mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
625
1,237
Afu kwanza ni Kilimanjaro yupi?
Kilimanjaro express Arusha-Dar sijawahi ona gari namba A wala B
AQN
Screenshot_2022-07-16-16-24-44-23_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
34,131
45,681
Usimpangie mleta mada

Mtaji hujampa wewe
Anajitahidi sana kwa Sisi tunaomjua

Matajiri wengi wa mabasi walishafilisika na kuondoka barabarani. Mzee Kilimanjaro yuko fit bado yuko barabarani na mabasi wenzie umri wake wengi mabasi yalishaondoka barabarani kwa kufilisika

Ukitaka kanunue na wewe yako uingie ligi na mzee kilimanjaro na mabasi yako mapya uone mziki wake ndipo utajua Mzee Kilimanjaro biashara hajajifunza jana kama wewe
 
Wewe bila mimi mteja yule hawezi kusurvive so kama mteja lazima nimwambie ukweli abadilike
 
themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
534
1,751
Mi bado nawaungisha maana wakati wa kula wanakusubiri umalize chakula restaurant siyo wale wengine eti kula na kuchimba dawa dk10. Abiria anahaha kwenda kukata gogo, haijakaa sawa anaambiwa chakula elfu 8 chakula chenyewe kidogo kama cha boarding halafu mbiyo kwenye gari.
na mimi ni mteja wao ila nawaambia ukweli gari chakavu ni hatari kuliko kusubiriwa kula
 
Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
4,599
13,914
Biashara ya ma bus inatakiwa iendeshwe kama anavyoendesha Klm ndo maana muhuni yupo kwenye game kitambo na bado analeta G7 mpya namba D
Ukikurupuka unafilisika chap tu , Darlux kaingia na wenge leo Yuko chali na michina yake ila muhuni klm xprss anakomaa na marcopolo gari zenye maisha marefu anazifanyia maborsho ya Mara kwa Mara na huduma bora ndo maana ana survive yupo kwenye game Hadi leo.

Biashara ya bus ni pasua kichwa kama huna roho ngumu huwezi kuifanya inaweza kukufilisi chap tu ukajikuta umetajirisha maajent na makondakta, kwahiyo unatakiwa ujue unae mshauri anaijua hiyo biashara vilivyo hawezi kuwekeza pesa nyingi kuliko faida anayopata huko ni kuchoma hela, wachoma hela wote sahivi wako chali japo waliingia na michina ya kisasa
 
BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
776
1,657
Hii kampuni nimewaungisha sana lakini kwa sasa nataka kuwakimbia.

Tajiri ana mabasi ambayo yana namba A yapo barabarani yamechakaa.

Hata ile ajali ya Mbeya, juzi inasemekana uchakavu wa gari nao ni chanzo kikubwa.

Tajiri hanunui gari mpya anavizia wenzake wafilisike or magari yao yachoke kisha anayanunua kwa bei rahisi kisha anayapeleka gereji yake anayachomelea na kuyapiga rangi kisha anayaweka barabarani anayaita luxury.

Mfano ni zile gari za Dar Lux kazinunua kazipiga rangi kisha akaweka engine za Scania , akazileta barabarani ila cha kushangaza yale magari yana AC juu ila ukipanda ni joto kwa kwenda mbele hamna AC mule ni janja janja.

Magari ya Kilimanjaro baadhi yameshachoka, mengine hadi ndani kuna harufu ya uvundo lakini mmiliki anajidani anatoa huduma za kisasa.

Ni muda muafaka kwa wamiliki wa hii kampuni wakiona ubahili kununua Scania mpya basi wamgeukie mchina la sivyo hii kampuni tutaikimbia soon.

Angalia matajiri wengine kama Nacharo na Sauli. Sauli alianza na gari chache juzi kanunua Marco polo mpya kaweka barabarani.

Juzi Nacharo ya Tanga baada ya kucheza na mchina kwa kipindi kifupi juzi kanunua gari mpya za marcopolo scania kweka barabarani.

Na siku hizi makampuni ya kuunda mabasi kama una kampuni kubwa unachukua magari na unalipa kwa awamu sijui anakwama wapi.
Kwani yuko peke yake Barabarani? Ukiona buduma mbaya hama nenda kwingine, acha kuchafua Biashara za watu, na oua alie kymuambia no A ndo zinaanguka ni nani? Kwa hio hakuna no D zinazo angauka?

Gari ni matunzo na Service na wala sio No, AC za nini kwani Madirisha ni Seald?
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
34,131
45,681
Biashara ya ma bus inatakiwa iendeshwe kama anavyoendesha Klm ndo maana muhuni yupo kwenye game kitambo na bado analeta G7 mpya namba D
Ukikurupuka unafilisika chap tu , Darlux kaingia na wenge leo Yuko chali na michina yake ila muhuni klm xprss anakomaa na marcopolo gari zenye maisha marefu anazifanyia maborsho ya Mara kwa Mara na huduma bora ndo maana ana survive yupo kwenye game Hadi leo.

Biashara ya bus ni pasua kichwa kama huna roho ngumu huwezi kuifanya inaweza kukufilisi chap tu ukajikuta umetajirisha maajent na makondakta, kwahiyo unatakiwa ujue unae mshauri anaijua hiyo biashara vilivyo hawezi kuwekeza pesa nyingi kuliko faida anayopata huko ni kuchoma hela, wachoma hela wote sahivi wako chali japo waliingia na michina ya kisasa
Uko sahihi sumry alikuwa na mabasi 80 brand ya kisasa aliuza yote kukimbia ushindani akaenda kulima sumbawanga

Akina Kilimanjaro aliwakuta akaondoka kwenye biashara na mabasi yake Classic akina Kilimanjaro bado wanaenda

Anayebisha aingie YouTube a search kwa kuandika milionea Sumry amsikie mwenyewe alichoongea kuhusu hiyo biashara ya mabasi
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
65,586
73,013
Biashara ya ma bus inatakiwa iendeshwe kama anavyoendesha Klm ndo maana muhuni yupo kwenye game kitambo na bado analeta G7 mpya namba D
Ukikurupuka unafilisika chap tu , Darlux kaingia na wenge leo Yuko chali na michina yake ila muhuni klm xprss anakomaa na marcopolo gari zenye maisha marefu anazifanyia maborsho ya Mara kwa Mara na huduma bora ndo maana ana survive yupo kwenye game Hadi leo.

Biashara ya bus ni pasua kichwa kama huna roho ngumu huwezi kuifanya inaweza kukufilisi chap tu ukajikuta umetajirisha maajent na makondakta, kwahiyo unatakiwa ujue unae mshauri anaijua hiyo biashara vilivyo hawezi kuwekeza pesa nyingi kuliko faida anayopata huko ni kuchoma hela, wachoma hela wote sahivi wako chali japo waliingia na michina ya kisasa
Hii biashara inabidi uwe bahiri kweri kweri

Ova
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

39 Reactions
Reply
Top Bottom