Wamiliki wa Mabasi na mafuso hutoa wapi hela?

Wamiliki wa Mabasi na mafuso hutoa wapi hela?

Hakuna wizi wala uchawi, Bank zinahusika hapo, Mabenk mengi yana pesa na yanahitaji wakopaji, watu mnalilia tuu uchawi, lakini usiende Bank kama hata kampuni huna maana hakuna mtu atapoteza muda na wewe, anza kidogo onyesha satements zako na documents za kibiashara na kodi unayolipa, cha maana anzisha kampuni onyesha cash flow zako, taxes etc kitu ambacho ni rahisi sana, ukienda bank watakuwa more than happy kuongea na wewe ili wakupe mkopo, tatizo weng wavivu hamtaki kufanya kazi na kufuata sheria ili muonekane wafanyabiashara wa kweli, hata eka 5 za mahindi na kampuni na ukionyesha ulichouza kihalali bank watakupa mkopo mkubwa tuu, usitake mkopo wa milioni 300 wakati huna hata kampuni ya biashara inayoingiza kipato, bank hawatazungumza na wewe
Umeamua kutugombeza Broo!!!
 
Imagine, kuna haya mabasi

Ester Luxury
Tilisho
Happy Nation
Sauli
New Force
Arusha Express
Shabiby
Abood
Machame Express
Kapricon
Kilimanjaro Express
Dar Express
Zube
Saratoga
Mgamba
Kimbinyiko
Abc
Ally's
Saibaba
etc etc

Malori ndo usiseme.
Unakuta mtu ana basi 10, 20 au 60. Basi moja bei yake ni Milion 300, 400 hadi 500. Jamaa wanapata wapi hela aisee?
Hujafika songea stendi kuu ya mabasi ukamuona mwamba Super feo anavyopanga scania zake dadeki..Tz hii hakuna anayemfikia super feo katika hii biashara ya mabasi ya usafirishaji
 
Kuna jamaa yangu ana mabasi ya mkoa 42, arejesha milion 60 kwa mwezi CRDB
Inamlipa kwan ukipiga hesabu kwa mwezi kila gari linarejesho la mil 1.43 ,kwa mwezi magari yote anavuna sio chini ya Tshs 420 mil,other factors remain constant,kwa mwaka ana vuna 5bill ,akitoa rejesho na other running costs anaweka 4bill kibindon,biashara ya transportation inalipa tized
 
Imagine, kuna haya mabasi

Ester Luxury
Tilisho
Happy Nation
Sauli
New Force
Arusha Express
Shabiby
Abood
Machame Express
Kapricon
Kilimanjaro Express
Dar Express
Zube
Saratoga
Mgamba
Kimbinyiko
Abc
Ally's
Saibaba
etc etc

Malori ndo usiseme.
Unakuta mtu ana basi 10, 20 au 60. Basi moja bei yake ni Milion 300, 400 hadi 500. Jamaa wanapata wapi hela aisee?
Nanunua rinda kwa milion 500 Kama uko tayari
 
Fisadi ni mpambanaji. Hukai kwenye channel ya hela bila kupambana otherwise hata vichaa wangekua mafisadi.
Pia fisadi ni mtu ambaye shule anayo ya kutosha. Wale kuwafunga ni ngumu mno kwasababu wizi wao ni wa kisomi. Utakuta zimeibwa hela nyingi lakini wanaokamatwa ni vidagaa. Fisadi liko tu ila ushahidi wa kumtia hatiani hauonekani.
 
Watu wengi ni masikini kwa sababu kuu tatu

1-Ujinga - kutokujua jinsi gani ulimwengu wa pesa unavyofanya kazi. Wengi tumekuzwa katika mfumo wa "shule"...soma nursery, mpaka A-level then omba mkopo go to UNIVERSITY ...ukimaliza tembeza bahasha kuomba ajira serikalini, ukishapata unaanza kulipa mkopo kwa miaka zaidi ya 15 huku ukiishi maisha ya mshahara mwezi mpaka mwezi..ukija kustuka umri wa kustaafu ushafika huna cha maana ulichokifanya. Leo hii tajiri akipaki ndinga lake hutasikia masikini wakisema kuwa jamaa kasoma sana yule ndio maana kafika pale alipo,maneno utakayoyasikia ni jamaa ni drug dealer, fisadi,jambazi, amewatoa kafara wazee wake, freemasoj n.k

2-Uvivu - hapa unatakiwa uelewe kuwa ili ufike kwenye utajiri basi jua kuwa unashindana na kundi kubwa la watu katika kuisaka pesa, matajiri huwa hawalali, muda wote wanaisaka pesa ilipo tofauti na wafanyakazi wa serikalini unaingia kazini saa 2 na nusu unatoka saa 9 ukitoka unakwenda kulala nyumbani, ukisubiri kesho ifike.Matajiri muda wote wapo macho tembea barabarani usiku uone malori yao yanavyoingiza pesa, miradi yao inaingiza pesa masaa 24 bila kupumzika ila masikini hufanya kazi kwa muda mchache tu .

3-Kiburi - ujuaji unafanya watu wengi kubaki katika umasikini. Ili uwe dereva mzuri ni lazima ufundishwe na mkufunzi mzuri...mfano mtu utakwenda VETA au NIT ili uive katika fani ya udereva, vivyo hivyo huwezi kuwa tajiri kama upo mbali na matajiri, huwezi kuwa tajiri kama hujakaa chini na waliokutangulia katika utajiri ukapata misingi ya nini ufanye kuelekea katika njia ya utajiri. Masikini wengi ni wajuaji, wanaridhika kuwa wao wanajua nini wafanye matokeo yake wanaendelea kubaki katika umasikini. Kaa karibu na uwaridi ili upate kunukia au fuata nyuki upate asali. Tusiwe viburi kujifunza kwa matajiri.
 
Ufisadi, connection na biashara haramu ndio asilimia kubwa ya chanzo cha mitaji.

Mafisadi wakipiga hela huko serikalini huwa wanawatafuta wafanyabiashara "smart" ili wawazungushie kwenye biashara zao. Zingatia neno "smart"

Connection hasa kwenye tenda serikalini, kukwepa kodi na pia connection kwenye kupata mikopo bank hasa crdb bank, wachaga wengi walipata mikopo na kukua enzi za Dr kimei. Pia connection ya kupata viwanja kwenye prime areas zinazofaa kwa ajili ya kuchukulia mikopo connection inachezwa na watu watatu (benki, watu wa ardhi na watu wa Tanroads) ili kupata maeneo yenye ukubwa kuanzia 1000 sqm mpaka 5000sqm yanayofaa kwa mikopo bank.


Ndumba/uchawi. Hizo ndumba ni za kufanya biashara iwe na wateja wengi sana na iwe na mzunguko mkubwa. Mshana Jr utaongezea 😂

Kudhurumu watu pia inaleta utajiri sana 😂. Sanasana viwanja vilivyo kwenye prime areas. Pia kudhurumu watu mali/hela/bidhaa feki. Kuna Matajiri wengi maarufu ila siri ya utajiri wao ni kudhurumu watu.

Kurithi na kujua kuendeleza biashara, + nidhamu kubwa ya hela.


NB: Matajiri wengi wana nidhamu kubwa ya hela. Pia wana connection, wapo smart, wanatunza SIRI. Wana viwanja vikubwa vya 5000sqm + prime areas ( kuna tajiri anazo hati za 5000sqm kama 50+ sehemu mbalimbali Tanzania kwa ajili ya hoteli,sheli, godown, viwanda, magorofa )


Hivi punde
 
Moja ya kiburi cha masikini ni kujifanya wajuaji wakati hawajui, utakuta mtu anasema Matajiri wamepata utajiri kupitia mikopo ya mabenki ila ukimuuliza ni vigezo gani anatakiwa avikamilishe ili nae akopesheke atakwambia hajui na wala hana mpango wa kuwafata wanaojua ili wamuelekeze ili nae ajue. Usitegemee kuwa na pesa kama hukai karibu kujifunza kwa wale walio kwenye chaneli ya pesa.

Mfano unaweza kukaa na tajiri ambae tayari anamiliki mabasi na kampuni kubwa tu ila ukimdadavua atakwambia tu usione nimefika hapa nilianza kwanza na biashara ya kununua nafaka vijijini huko ,nikapanda mtaji ,nikaja kuanzisha biashara fulani, then biashara fulani mpaka nimefikia hapa unaponiona...tayari hapo kashakupa ABC zake alipotokea na jua kuwa haikuwa kazi ya siku moja ila ilimchukua miaka ya ku-hustle
 
Back
Top Bottom