MWALIMU J.K.Nyerere alishatuasa kuwa ni vyema kukaa mbali sana na Mmarekani. Katika miaka ya hivi karibuni tumeona juhudi kubwa za kuikurubisha Tanzania kwa Marekani na uongozi ulioko madarakani.
Ninachojiuliza ni, je, hofu za Babu sasa hazina msingi? Hata mwanae Benjamin Mkapa naye aliwaogopa sana jamaa hawa. Vipi awamu ya nne inajipeleka mzobamzoba miguuni mwa jamaa hawa ambao hawatabiriki-leo rafiki, kesho ukimuudhi kama Saddam alivyofanya adui mkubwa na anaishia kukuangamiza!
Hofu ninayo bado mie labda akija madarakani Mjalua Obama tunaweza kuonewa huruma. Lakini hata hili naona kama ndoto maana kuna asiyejua kuwa Marekani inaendeshwa na Wayahudi? Na hakuna Obama analoweza kupinga pindi akiamrishwa na wakubwa wake.
Historia inatuonesha nini Wamarekani walichowafanyia ndugu zao huko Marekani ya Kati na Kusini; kisha Vietnam, Korea na Mashariki ya mbali kwa ujumla; na kwa hivi sasa wanachoendeleza Afghanistan na Iraq.
Hili ni taifa linaloishi kwa kukopa miaka nenda rudi. Na linapotishika kuishiwa kama ilivyo sasa basi linageuka jijambawazi kuu na kuzinyonga nchi za kinyonge ili kukwapua chao na kujipatia tena fedha za kuendesha maisha yao aghali. Wana-Jamii, je, sio muhimu kuzungumza hatima ya Tanzania na urafiki wake wa karibu na Marekani bila kujali tuna ndugu zetu na jamaa zetu na pengine wazazi wetu wanaoishi Marekani?
Nia sio kuvunja uhusiano na Marekani. Bali kujilinda kwa hasira na jazba zisizo na mipaka za jamaa hawa pindi wakiona mambo sivyo kwa upande wetu kulingana na maslahi yao. Na ikiwezekana tushawishi kuwepo kwa uongozi wa Marekani na dunia unaojali maisha ya wote; unaowatetea wanyonge badala ya kuwadidimiza; na ulio tayari kushiriki katika ubia maridhawa wa kibiashara na ulinzi wa mazingira na usalama wa dunia!