Wamarekani na Watanzania

Wamarekani kama wasipomchaguwa Obama..Basi uwezekano kuwa tutaingia kwenye vita ya TATU YA DUNIA ni mkubwa...Hili naomba muweke kwenye rekodi kabisa.

Nasema hivyo kwasababu yeye anawakilisha wale wanausalama wenye intelligence zinazoonyesha kuwa bila mazungumzo Taifa hili kubwa liko hatarini kuanguka.

Na hatari hiyo inaweza kuanzia hata marekani kwenyewe...Juzi tu kuna mtu ameingia na machine gun yake na kuuuwa watu hovyo kanisani kwa madai kuwa wao ni liberals...Na liberals ndio hao kina Obama.

Kimtizamo...Kuna mgawanyiko mkubwa sana...Ndani ya wamarekani wenyewe na vyombo vyao vya usalama...Ndugu zangu tuombe Mungu tu.

Kwani mmarekani anapambana na mchina na mrussia...Na mwarabu mwenyewe keshakabidhi UHURU WOTE kwa hao watu ili wapewe ulinzi.

Kwanza hata Irani wenyewe nahisi tayari wana Nyuklia...!

Maneno ya kiongozi msomi kama Ahmedinejad kuwa ataifutilia mbali Israel kutoka kwenye ramani ya dunia si maneno ya debe tupu!

Na hata Olmert alikiri juzi kuwa Muafaka wa Israel na Palestine uko karibuni kufikiwa.

Mgogoro uko kwenye mji wa JERUSALEM..Hapo Mc Cain mwenyewe keshasema patakuwa makao makuu ya Israel siku akiapishwa kuwa Rais..Makao makuu ya Israel sasa yako Tel Aviv.

JERUSALEM NI MJI WANAOUPIGANIA NA KAMA HAWATAWEZA KUISHI PAMOJA KAMA OBAMA ANAVYOWATAKA WAFANYE..BASI TUTARUDI KWENYE HADITHI ZILE ZILE ZA VITA...TATIZO NI IRAN.

Mimi nahisi kuna intelligence za siri na inawezekana kabisa kuwa Iran tayari wana atomic bomb.

Balaa hili linaweza kuepushwa...Ila kwasababu demokrasia ni upigaji wa kura...Basi wanatakiwa wasiangalie weusi wa Obama kwani hapo ndio kipimo chenyewe!

Na hakika niko radhi kusema kuwa Obama asipochaguliwa...Basi mambo yanaweza yasiwe mambo kwani viongozi wasiopenda siasa za kidiplomasia..Wanaokumbatia vita tu...Hii ni hatari kwa dunia yetu!

Marekani ni wa kuombewa Mungu watanzania hilo mjuwe.
 
Mushi wanaweza kabisa wasimchague. Jana nilikuwa nawasikiliza political analysts na wengi wanadai Obama anashindwa kuweka gap kubwa kwenye opinion polls kati yake na McSame kwa sababu ya ngozi yake, wanadai inamcost kati ya 6 points to 10 points. Inasikitisha sana kwamba pamoja na sera za Kichaka kushindwa vibaya sana na kusababisha matumizi ya $700 billioni katika vita ambayo haikustahili kupiganwa, Record budget deficit ya $500 billions, reputation mbovu ya US karibu kila kona ya dunia, uchumi ulioporomoka vibaya sana, deni la nje la $9.5 Trillioni bado wanataka kumchagua Mcsame pamoja na kuwa sera zake zinashabihiana sana na za Kichaka!!! Dunia nzima inataka Obama ashinde, lakini kwa jinsi inavyoelekea inaweza isiwe hivyo na hii itakuwa ni habari mbaya siyo kwa US pekee yake bali kwa dunia nzima. Obama kama bado atakuwa hafanyi vizuri kwenye opinion polls basi itakuwa vizuri kama akimchagua Hillary kama VP wake ili aongeze nguvu katika campaign.
 
...babu acha pressure,Obama will be the next president by landslide....kama unataka weka bet niko tayari!
 
Mushi wanaweza kabisa wasimchague. Jana nilikuwa nawasikiliza political analysts na wengi wanadai Obama anashindwa kuweka gap kubwa kwenye opinion polls kati yake na McSame kwa sababu ya ngozi yake, wanadai inamcost kati ya 6 points to 10 points. Inasikitisha sana kwamba pamoja na sera za Kichaka kushindwa vibaya sana na kusababisha matumizi ya $700 billioni katika vita ambayo haikustahili kupiganwa, Record budget deficit ya $500 billions, reputation mbovu ya US karibu kila kona ya dunia, uchumi ulioporomoka vibaya sana, deni la nje la $9.5 Trillioni bado wanataka kumchagua Mcsame pamoja na kuwa sera zake zinashabihiana sana na za Kichaka!!! Dunia nzima inataka Obama ashinde, lakini kwa jinsi inavyoelekea inaweza isiwe hivyo na hii itakuwa ni habari mbaya siyo kwa US pekee yake bali kwa dunia nzima. Obama kama bado atakuwa hafanyi vizuri kwenye opinion polls basi itakuwa vizuri kama akimchagua Hillary kama VP wake ili aongeze nguvu katika campaign.

Kuna MOVEMENT MBILI...Nilishawahi kusema nyuma sana kwenye ile thread ya Obama wakati nikichangia kabla na pia nilisema itabidi nihamie kwenye politics za bongo kwani muda si muda nitaonyesha connection ya wazi ya namna chaguzi zetu zinavyoingiliana.
 
...babu acha pressure,Obama will be the next president by landslide....kama unataka weka bet niko tayari!

Usisahau njemba za Republicans zinaiba kura pia na walifanya hivyo katika chaguzi za 2000 na 2004, na pia sehemu wanazoishi weusi wengi huweka matangazo ya kuwadanganya kwamba uchaguzi umeahirishwa mpaka wiki moja baada ya tarehe ya kweli ya kupiga kura na kuwatisha wale wenye criminal records kwamba wakienda kupiga kura watakamatwa. Weusi wengi hawasikilizi kabisa habari za kila siku hivyo ni rahisi kuamini chochote wanachosikia na matokeo yake yanaweza kuwa si mazuri.

Napenda sana Obama ashinde maana wengi wetu hatukutegemea katika uhai wetu kumuona Rais wa kwanza mweusi wa Marekani, lakini baada ya miaka 232 ya uhuru wa US tunakaribia kuiona history ikabadilika kwa hatua kubwa sana, lakini wakati huo huo tusisahau vizingiti mbali mbali vinavyomkabili Obama. Na haya niliyoyandika sikuyatunga toka kichwani bali ni kutoka vinywani mwa kwa political analysts wa vipindi mbali mbali ambavyo huwa naangalia

I don't know what is your definition of a 'landslide' but FYI America is so divided right now, almost 50/50. The last president who won by landslide was Ronald Reagan 28 years (1980's elections) ago by 18 points. Kama una pesa ya mchezo na kutaka kubet basi ni bora ukatoe zaka kanisani mimi siko tayari kuchukua pesa yako, lakini nakuhakikishia uchaguzi huu unaokuja hakuna atakayeshinda kwa landslide. Na wote tutafurahia kushuhudia history ya Mweusi wa kwanza Marekani kutinga WH.
 
Obama yuko very arrogant kwasababu movement yake ilijipanga miaka nenda rudi!

Ni movement inayoonekana imekuja kuipindua movement ya kina Bush,Clinton, na kina Andrew Young...Hao walilitumia jina la MLK kwa maslahi yao kama wengine wanavyojinufaisha kwenye vifo vya watu wengine.

Wenye kuthubutu kusema eti weusi ni idadi ya wanawake uliotembea nao.

Movement ya kina Young ni CORRUPT...IKISAIDIWA SANA NA CLINTONS.

Hiyo mikataba mibovu si ni wao wako behind?

Hata CANADA si walithubutu kabisa kumponda OBAMA na kumkumbatia CLINTON kwa style iliyokuwa inasikitisha?

Fuatilia ile debate ya primaries na utagundua kwenye ile issue ya NAFTA...Na vituko vilivyofuatia.

Movement ya OBAMA ni ya matajiri ambao wameona sasa mwisho wa kumyonya masikini umekwisha...Na movement nyingine ni ile ya wale walafi wasioridhika na faida.

Kuna watu kama kina Bill Gates,George Soros na hata binti wa tycoon la FOX NEWS anayeishi huko Uingereza...OBAMA ana MOVEMENT..Na ndiyo maana huwa kila kwenye kampeni yake humalizia kwa kuwaaambia wamarekani wamsaidie ili aibadilishe dunia.

Watu wazito waliodhamiria kuwanywesha wamarekani mabadiliko muhimu ili waweze kuingiliana na mataifa mengine bila matatizo...Watu kama familia ya JFK...Wote mnajuwa conspiracies za kifo chake...Hivi kweli wewe unadhani kuwa FAMILIA KUBWA KAMA YA JFK HAIKO BEHIND HII MOVEMENT?
Familia ya JFK NDIYO MOVEMENT HALISI YA MLK...Hao mamluki kina Young na Jackson walishanunuliwa na wazungu waliotumwa kuwalaghai weusi.

HII NI COME BACK YA MOVEMENT YA MIAKA YA 60'S NA TRUST...WAMEDHAMIRIA KWA KILA HALI...KUIBADILI DUNIA!

Nchi gani eti timu yao ikishinda ubingwa wa nchi yao wanasema eti ni WORLD CHAMPIONS?
Hata kama ni boxing..Kuna mabondia kibwena..Ukija kwenye hiyo football yao ni wao tu na hakuna mwingine anaujuwa mchezo nje ya US...nA WAKIBEBA UBINGWA..Eti unasikia ni FOOTBAL WORLD CHAMPIONSHIP!

Wamarekani hawajui siasa..Siasa wanazojuwa wao ni za kibaguzi tu! UBAGUZI NI MKUBWA SANA! Na kama wanataka wapate credibility ya kuyasema mataifa mengine basi waangalie pia na nyumbani kwani charity begins at home.

Inanishangaza sana kuona eti wamarekani wanasema mtu asiwachagulie rais wao..Hivi wao wanajuwa ni mara ngapi maraisi wao wameshawachagulia mataifa mengine maraisi wanaowataka?

Maneno kama hayo ya Obama ya kuzungumzia mabadiliko... yanawatisha Israel na Wale very conservatives.

Kimtizamo...Mchina naye alikuwa akipiga vita ya chini kwa chini...Mchina yeye hapigi kelele...Anatambaa kama nyoka!

Sasa hata hivi majuzi...Walionyesha mbwembwe kwa kuzindua kombora lao jipya..Kombora ambalo kwa kweli lilimrusha roho mmarekani...Waliitungua satellite yao moja...HILO LILIWASHTUWA SANA WAMAREKANI..KWANI ILIKUWA WAZI KUWA MCHINA HUYO HUYO ANAWEZA KUZITUNGUA HATA SATELLITE ZA USA...Na akifanya hivyo...Mmarekani atakuwa ni kama kipofu kabisa...HII NI HATARI!

Mchina amekuwa hasemi kitu..na wala hana mikogo...Lakini ana vijembe vibaya sana....Na halafu yuko kila mahali ikimwemo marekani yenyewe!

Kama mchina ni mbaya...Mmarekani atakubali vipi aandae olympic na tena Bush mwenyewe kuudhuria?

Ni wazi watu wa namna hiyo wanatakiwa kuongea nao kwani ni watu hao hao kina Putin na sasa kamweka Medved...Sasa Mwarabu naye katumia karata ya Israel na kumpa uhuru wote mrusi na mchina...Sasa kwasababu ya siasa mbovu za kichaka...Mambo duniani kote yamewageukia wamarekani...Na ni OBAMA tu anayeweza kwenda mezani na kunegotiate...Na keshasema wazi.

Na hata sasa Bush anaonekana kuzikumbatia idea zake kwani keshaanza mazungumzo na Iran na pia kutoa kauli maarufu ya HORIZON TIMETABLE...Kauli ambayo ni ya kujishebedua tu kwani ni sawa na kukubaliana na sera za Obama..Hapo hata Babu wa watu amejikuta hawezi kabisa kuchaguwa ni pande gani na ikabidi hata aende kwa Bush mkubwa kuomba ushauri...Kama kuna wenye picha wazilete hapa...Bush mkubwa si ndiye huyo mwenye share BARRICK?
 
Kama Bush MKUBWA ANA SHARE BARRICK..Halafu JK ana MASLAHI NA NI SWAHIBA WA SINCLAIR...Basi hata mimi nahisi hatari hapa nilipo na itabidi niombe ulinzi.

Kwani kama tunaipinga Barrick na Bush ni Barrick...Sisi hatuko matatani kweli?

Na JK mwenyewe hata sijuwi sera zake ni zipi...Ila naona anamtingishia kiberiti Mmarekani.

Kama hatatetereka..Basi hatujali kama ni mchina ama mmarekani..Hata wote wanaweza wakashindana kwa bei na si kwa nani mwenye nguvu za kijeshi..Kwani huo utakuwa ni ukandamizaji na haki ya Raia hakuna...Hapo ndio kazi ya Zitto kwenye bunge lake inapokuja...Hilo bunge la dunia...Ili kukwepa vita ni lazima mambo kama haya yazingatiwe.

Kwasababu Taifa moja kuwa na influnce moja kwa moja bila ya uwezo wa taia jingine kuweza na wao kupanda dau ni sawa na ukoloni na imperialism tu.

Tunataka uhuru wa kusikiliza dili kutoka kwenye kampuni base on how much they are willing to help the people na si kikundi kidogo cha watawala na familia zao.
 
Hii linki hapo chini inaonyesha ni kwa kiasi gani hawa watu hawataki kukaa pamoja na kukubaliana...Yani kila Taifa kubwa linataka UBABE..Akiwa mchina...Anataka awe yeye tu..Akiwa Mmarekani..Muindi naye ndiyo kama mabwana wa wabongo wengine bila kusahau waarabu..Mambo yako Hivyo hivyo..Sasa Afrika itafikia mahali tugome kabisaa!
Lakini ni baada ya kuwaondoa viongozi CORRUPT wanaotegemea nguvu za mataifa makubwa ili kuendeleza ufisadi.
http://news.bbc.co.uk/1/hi/business/7531099.stm
 
Lol Kweli JF kiboko mshashift kwa jaluo....sasa hivi inabidi tualign na US maana ndio super power iliyobaki inaeleweka...Wachina, ukitoka Shanghai ukaingia ndani ni msoto kama bongo tu...

Hii ya kusafiri kwa kibali cha Ikulu ni kweli? mie nina ndugu kadhaa wamesafiri wakati wa Nyerere na hakuna anayemention mambo ya kupata kibali cha Ikulu lol.

NN naona babu yako McCain bado yuko stuck kwenye late 60s anatoa ads zenye nyimbo za Frankie Valli.
 
Na hao waliokuwa right kuhusu ubepari ukiwauliza je Tanzania katika kipindi cha ujamaa na katika kipindi cha ubepari ni kipindi kipi ambacho Watanzania walifaidika zaidi? Jibu tunalijua. Wengi tuliona maendeleo makubwa ya Tanzania wakati wa ujamaa pamoja na kuwa nchi za magharibi zilimpiga vita kubwa Mwalimu ukilinganisha na kipindi cha ubepari pamoja na kuwa na marafiki kama US n.k. waliotumwagia "misaada" ya kutununua. Chini ya Mwalimu uchumi ulikuwa mikononi mwa Watanzania, aliweza kusomesha Watanzania hadi chuo kikuu bila kujali uwezo wao na hao ndiyo leo hii wanatamba katika kona mbali mbali za dunia kutokana na uongozi wa Mwalimu.
Sasa hivi kuna mafisadi tu ambao wanaiuza nchi yetu kila kukicha kwa mikataba isiyo na maslahi yoyote kwa Watanzania. Bado naamini kauli ya Mwalimu kwamba UBEPARI NI UNYAMA!!! Na unyama huo unashamiri sasa ndani ya nchi yetu.
Nyerere labda alikua tu na wazo la kuweka uchumi chini ya umma lakini hakufanikisha kuunda/kukuza ama kuimarisha huo uchumi na kidogo kilichokuwepo alikipelekesha mpaka kuanguka. Mwisho alikiri makosa. Tokea kwenye misingi ya siasa zake ikaonekana hatutafika mbali na mabadiliko ikawa ni dhahiri na ndio matokeo ya kufika tulipo, dudu CCM limeshakua FISADI. Hivyo hamna afadhali yeyote chini ya Mwalimu.
 
Tuambieni na kwingineko Africa ambako UJAMAA wa Mwalimu haukuwepo wamefika wapi kiuchumi, kiusalama, kiumoja kama TAIFA, mtoto wa masikini alisoma hadi chuo kikuu,....
 
being wrong or right is not real in any how just ur perseption

tumainin

Kitu ambacho mimi sipendi ni hii tabia ya "Mwalimu alisma" as if chochote asemacho Mwalimu Nyerere was then Cast in Stone as the Gospel truth... I agree Mwalimu has done some good things but lets not be subjective and be objective and also learn to acknowledge that he also did alot of Wrong things that put us in a very compromising position kimaendeleo... Ubaya wa waTanzania nikwamba because of huyu Mwalimu sasa hivi majority ya waTanzania wamekaa mkao wa kutawaliwa au kuongozwa na mtu tumesahau kabisa kuchukua destiny in our own hands... And we are suprised the brainchild of Mwalimu by way of hawa mafisadi, nk wanatu-hold ransom??????
 
Kitu ambacho mimi sipendi ni hii tabia ya "Mwalimu alisma" as if chochote asemacho Mwalimu Nyerere was then Cast in Stone as the Gospel truth... I agree Mwalimu has done some good things but lets not be subjective and be objective and also learn to acknowledge that he also did alot of Wrong things that put us in a very compromising position kimaendeleo... Ubaya wa waTanzania nikwamba because of huyu Mwalimu sasa hivi majority ya waTanzania wamekaa mkao wa kutawalwa au kuongozwa na mtu tumesahau kabisa kuchukua destiny in our own hands... And we are suprised the brainchild of Mwalimu by way of hawa mafisadi, nk wanatu-hold ransom??????
Na pia hata hii tamaduni ambayo imeendelea Tanzania ya watu kuiogopa Serikali kupita kiasi mpaka kufikia hatua ya kuogopa kudai haki zao ni legacy ya sera za mwalimu Nyerere ambaye aliwabana kwa kuwaweka vizuizini wale wote waliokuwa wanapinga sera zake. Leo hii pamoja na uchafu wote unaofanywa na MAFISADI watanzania bado wako kimya kama hakuna baya lolote linalofanyika, watu wanaogopa hata kuandamana kuhakikisha MAFISADI wanafikishwa mbele ya sheria. Huu ndio uchafu wa ujamaa ambao hautakiwi sehemu yeyote duniani. Kwa sera hizi hizi Mwalimu Nyerere alichemsha.
 
Na pia hata hii tamaduni ambayo imeendelea Tanzania ya watu kuiogopa Serikali kupita kiasi mpaka kufikia hatua ya kuogopa kudai haki zao ni legacy ya sera za mwalimu Nyerere ambaye aliwabana kwa kuwaweka vizuizini wale wote waliokuwa wanapinga sera zake. Leo hii pamoja na uchafu wote unaofanywa na MAFISADI watanzania bado wako kimya kama hakuna baya lolote linalofanyika, watu wanaogopa hata kuandamana kuhakikisha MAFISADI wanafikishwa mbele ya sheria. Huu ndio uchafu wa ujamaa ambao hautakiwi sehemu yeyote duniani. Kwa sera hizi hizi Mwalimu Nyerere alichemsha.

Mwanakijiji atakuambia hao walivunja sheria na kwa mujibu wa sheria, Mwalimu hakukosea....Lol
 
Na pia hata hii tamaduni ambayo imeendelea Tanzania ya watu kuiogopa Serikali kupita kiasi mpaka kufikia hatua ya kuogopa kudai haki zao ni legacy ya sera za mwalimu Nyerere ambaye aliwabana kwa kuwaweka vizuizini wale wote waliokuwa wanapinga sera zake. Leo hii pamoja na uchafu wote unaofanywa na MAFISADI watanzania bado wako kimya kama hakuna baya lolote linalofanyika, watu wanaogopa hata kuandamana kuhakikisha MAFISADI wanafikishwa mbele ya sheria. Huu ndio uchafu wa ujamaa ambao hautakiwi sehemu yeyote duniani. Kwa sera hizi hizi Mwalimu Nyerere alichemsha.

Wanajuwa hilo wazi ndio maana wanatumia saikolojia ya usalama wa Taifa kwani kumbu kumbu za usalama wa Taifa za watanzania chini ya Mwalimu ni kizuizini.
 
Back
Top Bottom