BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Bubu, Asante kwa kuwaelimisha watu humu.
Wanaosema Mwalimu alifanyamakosa kwa kufuata siasa ya ujamaa ni 'wavivu wa kufikiri'! Siku zote mie huwaambia bila siasa za Mwalimu Nyerere wengi leo wasingelikuwa huko waliko na wasingelikuwa wanatamba kwenye internet badala yake wangelikuwa vijijini wakichunga mbuzi na ng'ombe! Washukuru elimu ya bure waliyopewa baba, mama, shangazi, wajomba zao n.k. iliyotokana na siasa za Mwalimu Nyerere. Leo hii watu bado tunatembea barabarani bila hofu kwa kuwa bado kuna ile chembe ya 'udugu' uliotokana na siasa za Ujamaa.
Ahsante sana Bibi Ntilie, Mwalimu kafanya mengi sana lakini watu wanataka kukumbuka yale mabaya tu ambayo mengi yalikuwa nje ya uwezo wake. Tulipiga hatua kubwa kimaendeleo wakati wa Mwalimu kuliko kipindi kingine chochote cha uhuru wetu wa miaka 47 hasa ukitilia maanani tulikuwa hatuna hata chuo chochote wala kiwanda. Siku zote tutamtetea kwamba alikuwa ni kiongozi mzuri pamoja na kuwa tulimpa majina mengi kama ya Mussa, Mchonga, Mzee haambiliki n.k. lakini alikuwa na mapenzi ya kweli na nchi yetu na maamuzi mengi aliyoyafanya yalilenga katima maslahi ya Watanzania. Hakuwa mroho wa utajiri, mwizi au fisadi ukilinganisha na wale waliokuja baada yake. Na hata wenzetu wa nchi nyingine za Afrika wakijua unatoka Tanzania wengi watakuuliza kuhusu Mwalimu na kuanza kummwagia sifa tele. Hakuwa perfect lakini lazima ukweli usemwe kwamba alifanya kazi nzuri sana na matunda yake yamesambaa karibu kila kona ya dunia.