WAMAMA PUNGUZEN HIZI KAULI KWENYE NDOA ZENU WANAUME WENGI WAMEPINDA NA MAISHA SIKUHIZI USIONE ANACHEKA NYUMBAN

WAMAMA PUNGUZEN HIZI KAULI KWENYE NDOA ZENU WANAUME WENGI WAMEPINDA NA MAISHA SIKUHIZI USIONE ANACHEKA NYUMBAN

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,023
Reaction score
36,865
WAMAMA PUNGUZENI KAULI HIZI KWA WAUME ZENU 🙏

Kila mzazi ana haki ya kumlea mtoto wake.
Malezi si jukumu la mama peke yake wala baba peke yake… ni ushirikiano 🤝

Lakini kuna kauli ambazo zinaumiza, zinadhoofisha mamlaka ya baba, na zina changanya watoto😔

Epuka kauli hizi mbele ya watoto👇
“Usinipigie wanangu kama mbwa!”
“Huyo ni mwanangu, wewe usimfokee!”
“Wewe huna haki ya kumkanya mtoto wangu!”
“Watoto ni wangu, wewe hujui uchungu wa leba”
“Nitaongea na wewe peke yako, usimguse mwanangu!”

🚫 Kauli hizi zinafanya baba ajisikie hana nafasi kwenye malezi
🚫 Zinamfanya mtoto aone mama na baba wako vitani
🚫 Zinavunja heshima na mipaka ndani ya familia

Mama kumbuka
✔ Baba ana haki ya kumkanya mtoto wake
✔ Nidhamu ya mtoto inahitaji sauti ya wazazi wote wawili
✔ Kutofautiana mbele ya watoto kuna wachanganya na kuwapa kiburi

Njia sahihi ni ipi?
👉 Kama hujaridhika na namna baba alivyo mkanya mtoto, zungumza naye faraghani
👉 Toeni maamuzi ya malezi kwa pamoja
👉 Mjenge umoja ili mtoto aone upendo na mshikamano, siyo ugomvi
Familia imara hujengwa na wazazi wanao shirikiana, si wanaopingana.
Tuwalee watoto wetu kwa upendo, heshima na umoja 🤍
 
DADA, GIZA LIMEINGIA… 🌙
Achana kidogo na mawazo ya vikoba na majukumu ya mchana, vaa tabasamu na mkaribishe mume wako kwa upendo wa dhati.

Kila mwanaume hutamani kurudi nyumbani apate:
✨ Amani ya moyo
✨ Maneno ya faraja
✨ Hisia za kuthaminiwa

Usimkaribishe kwa lawama na maswali ya shinikizo,
mkaribishe kwa upendo, heshima na utulivu.

Ndoa nzuri huanza na mwanamke anayejua kubadili mazingira ya nyumbani kuwa sehemu ya furaha💞

Leo jioni, chagua kuwa sababu ya mume wako kutabasamu😊

Share 🔁 kwa wanawake wanaojenga ndoa zao kwa hekima.
 
Back
Top Bottom