Walokole, tuache kujitenga na wenye dhambi

Habari wakuu,

Husika na kichwa habari hapo juu,

Kama kuna kitu ambacho ndugu zangu walokole tunakosea ni hapo pa kujitenga na wenye dhambi.

Wokovu tunaupata kwa neema ya YESU mwenyewe, na hata kabla ya kuokoka wewe ulikuwa na dhambi.

Iweje Leo umeokoka unajitenga na wengine na kijiona Mtakatifu.

Yesu mwenyewe alikula na alikaa na wenye dhambi, hata wale waliotaka kumuua alikuwa nao.

Pia aliwajua, hilo halikuwa kawaida ila alikaa nao na kuongea nao.

Sasa iweje wewe uliyeokoka unashindwa kukaa na mwenye dhambi ikiwa tu huyo unayemuamini alikaa nao.

Kumbuka umepata neema ya kuokoka wewe ili uokoe na wengine na sio kujitenga nao.

Sasa wewe umeokoka unajiita mlokole wakati sio mwanafunzi wake, ukiokoka ndio ushakuwa mwanafunzi unatakiwa na wewe utangaze neno watu waokoke.

Kuokoka kwanza lazima uwe na Upendo, sasa umeokoka unachukia wenye dhambi umeokoka au unajidanganya.

Unasengenya watu, badala ya kuwaeleza kwa upendo namna ya wewe ulivyopata neema na wao wajue kuwa Yesu ni Bwana.

Kama walokole wangekuwa na Upendo wa kweli wa kukaa na wenye dhambi na kuwapa elimu ya kuwa hata wao walikuwa na dhambi ila Sasa wameokoka.

Hakika watu wangemjua Yesu Kristo kwa wepesi sana, ila majungu, masengenyo na kujitenga, ndio kunafanya watu waone Wokovu hauna faida.

Walokole tuache ubinafsi na tupende wenye dhambi..
kama uneokoka izo ndo dalili za kuanza rudi nyuma jitenge nao
 
kwenye hii thread Umeongea kitu sahihi, ila kwa thread na comment zako nyingi za humu jf ni dhahiri kuwa wewe ni mlokole jina, sio mlokole halisi, hata mchawi akikuangalia kwa macho ya rohoni anajua hamna mlokole hapa, mlokole gani unashinda jf kuchambana na kina mzabzab Donatila
 
Mkuu umenikumbusha mtu mmoja anaitwa Martin Luther king jr anasema “ Giza halipunguzwi kwa giza, nuru ndiyo inapunguza giza ukitaka kuleta mabadiliko kuwa mwanga.

Huwa siamini hizi stori za miungu ila umemjibu vzuri huyo jamaa.
Asante.
Hiyo ni Yohana 1.
Yesu anasema Nuru yang'aa gizani wala Giza halikuiweza.

Mwanga hauna sifa ya kuogopa au kilikimbia giza. Giza (dhambi) ni dhaifu sana kwa mwanga.
 
Laiti ungejua kuwa hao walokole wengi wao wana roho mmbaya, ni wasengenyaji, wachoyo,
Kwa hiyo Makonda naye ni mlokole? Vipi mabosi wake nao ni walokole?

Acha kuuchafua ulokole kwa sifa ulizotaja ambazo zimebebwa na chama tawala kuanzia kiongozi wa shina hadi taifa wanahizo sifa na wanazitendea haki kabisa 😂
 
Walokole wanatumia vigezo gani kuwaita binadamu wenzao wenye zambi ,hizo mnazoziita zambi ni side effect za existence na haziepukiki
 
Back
Top Bottom