Walokole, tuache kujitenga na wenye dhambi

Walokole, tuache kujitenga na wenye dhambi

Walokole tuache kujitennga na wenye dhambi... hii ina tofauti gani na yule aliyemsema Yesu ambaye alikuwa anasali huku akimnanga mwenzake. Walokole bwana
walokole ndio kina nani hao ?
 
mbinguni hakuna wanaofanya ibada kwa kupiga makelele na kulia🤣😅😆😁😄😃😀
ukuta wa Yeriko ulianguka kwa Kelele au minong'ono ?
Mbingu sio ya mjomba wako kaa kimya.
 
Ukisoma Luka 7:37

Hapa kuna habari za Mariamu Magdalena mwanamke ambaye aliyehisishwa na dhambi...

Lakini Yesu alikuwa karibu naye na hakumtenga...
Hivi mifano yote ,ndio umeiona HUO na Huyo,
 
Umenena vema
Habari wakuu,

Husika na kichwa habari hapo juu,

Kama kuna kitu ambacho ndugu zangu walokole tunakosea ni hapo pa kujitenga na wenye dhambi.

Wokovu tunaupata kwa neema ya YESU mwenyewe, na hata kabla ya kuokoka wewe ulikuwa na dhambi.

Iweje Leo umeokoka unajitenga na wengine na kijiona Mtakatifu.

Yesu mwenyewe alikula na alikaa na wenye dhambi, hata wale waliotaka kumuua alikuwa nao.

Pia aliwajua, hilo halikuwa kawaida ila alikaa nao na kuongea nao.

Sasa iweje wewe uliyeokoka unashindwa kukaa na mwenye dhambi ikiwa tu huyo unayemuamini alikaa nao.

Kumbuka umepata neema ya kuokoka wewe ili uokoe na wengine na sio kujitenga nao.

Sasa wewe umeokoka unajiita mlokole wakati sio mwanafunzi wake, ukiokoka ndio ushakuwa mwanafunzi unatakiwa na wewe utangaze neno watu waokoke.

Kuokoka kwanza lazima uwe na Upendo, sasa umeokoka unachukia wenye dhambi umeokoka au unajidanganya.

Unasengenya watu, badala ya kuwaeleza kwa upendo namna ya wewe ulivyopata neema na wao wajue kuwa Yesu ni Bwana.

Kama walokole wangekuwa na Upendo wa kweli wa kukaa na wenye dhambi na kuwapa elimu ya kuwa hata wao walikuwa na dhambi ila Sasa wameokoka.

Hakika watu wangemjua Yesu Kristo kwa wepesi sana, ila majungu, masengenyo na kujitenga, ndio kunafanya watu waone Wokovu hauna faida.

Walokole tuache ubinafsi na tupende wenye dhambi.
 
wapi kwenye biblia watu walijiita wameokoka...?? ....na nini maana ya dhambi...? maana navyoona inawezekana walokole hawajui maana ya dhambi labda nijibu kwa kutumia biblia tafadhali ndugu.
1.Kuuokoka kunatoka hapa
Warumi 10: 9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

2. Dhambi ni uasi juu ya Mungu
1Yohana 3:4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
 
Yeah ni kweli kwenye msafara wa mamba ya kenge wapo, tena ndio huwa wanakuwa kihere here kweli kweli.
Ila bado uwepo wa kenge kwenye msafara hauzuii uwepo wa mamba.
Asilimia kubwa ya walokole ni matapeli. Kama yule ''prophet'' Malisa unasema ni mlokole? Gwajima naye? Mzee wa upako? Yaani list ni ndefu...
 
Back
Top Bottom