Walokole, tuache kujitenga na wenye dhambi

Walokole, tuache kujitenga na wenye dhambi

Unazunguka tu...

Hatujasema awe rafiki yako, ila usimtenge, mwambie namna Wokovu ulioupata na yeye aokolewe...
Ndiyo Mlokole aliyeokoka hata Kwa maongezi yake utamtambua.

Huyu Mlokole alikuwa na rafiki msengenyaji Mungu akamuokoa kutoka kwenye usengenyaji.

Sasa huyu rafiki akirudi Kwa rafiki yake itatakiwa kazi yake iwe kumhubiria au kumsaidia kibinadamu.

Huyu rafiki akihubiriwa na rafikiye akakataa kuokoka lazima rafiki aendelee kumpenda ila ajitenge naye Ili ajilinde asiingie kwenye dhambi.

Urafiki baina Yao hauwezi kuendelea sababu huyo amengangania kwenye Giza na rafiki yake yupo kwenye mwanga.
 
tunawaambia kila siku mbona. maana ndio kazi yetu kuzishuhudia habari za Bwana wetu Yesu Kristo. Tulipewa agizo la kuihubiri Injili kwa kila kiumbe. "na kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu.
Amina Mtumishi wa Bwana [emoji120]
 
Hii amri kuisema ni rahisi ila unatakiwa umpende hata adui yako...
Ingekuwa hivyo Hamas na Israel wasingezijapa. Sikupingi ila nataka tuweke sawa mizani, Yesu alikuwa ni Mungu mwenye nguvu kila alipopita alitenda mema, wenye njaa walikula, viwete walitembea, viziwi walisikia.

Yesu huyo huyo aliwaonya wale 'wasioamini kwamba wasiingie katika kazi ikiwa hawajapewa nguvu.

Sasa wewe unakuja na hili bandiko ambalo hata mtume Paulo kama angelisoma hili bandiko angekukemea hakika.

Maana ipo hivi sio kila mlokole anayo nguvu kama ulivyoainisha kwa uzi wako.

Ikiwa wewe unazo nguvu (upako) wa kukaa na wenye dhambi sawa kaa nao ila usitake hata wale walokole wachanga wafanye kama wewe.

Ni hivyo tu mama mchungaji
We jamaa unajua ukweli ila unapenda kupinga tuu...
 
Tulipewa agizo la kuihubiri Injili kwa kila kiumbe. "na kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu.
Hilo agizo liliambatana na Angalizo...." mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu.... "

Sasa wewe umeombewa hadi pepo la uzinzi likatoka halafu baada ya siku tatu unarudi kwa yule aliyekuwa anakukatia uno kabla hujafunguliwa, unanwendea eti ukamhubiri ilhali hujapokea nguvu 😂😂😂

Acheni mizaha katika wokovu jamani
 
Ingekuwa hivyo Hamas na Israel wasingezijapa. Sikupingi ila nataka tuweke sawa mizani, Yesu alikuwa ni Mungu mwenye nguvu kila alipopita alitenda mema, wenye njaa walikula, viwete walitembea, viziwi walisikia.

Yesu huyo huyo aliwaonya wale 'wasioamini kwamba wasiingie katika kazi ikiwa hawajapewa nguvu.

Sasa wewe unakuja na hili bandiko ambalo hata mtume Paulo kama angelisoma hili bandiko angekukemea hakika.

Maana ipo hivi sio kila mlokole anayo nguvu kama ulivyoainisha kwa uzi wako.

Ikiwa wewe unazo nguvu (upako) wa kukaa na wenye dhambi sawa kaa nao ila usitake hata wale walokole wachanga wafanye kama wewe.

Ni hivyo tu mama mchungaji
Hapa Sasa tumeelewana..

Ni hivi, ukiwa umeokoka kweli nasema kweli utapokea nguvu za Roho Mtakatifu...

Ukishasipokea hizo nguvu utakuwa inauwezo wa kuona yaani macho ya Rohoni na nguvu za Rohoni..

Hapa ukiwa na mtu hata yule mtenda mabaya hawezi kukubadili maana unauwezo...

Ambaye umeokoka alafu huna nguvu za Rohoni ni rahisi kutekwa maana umemkataa shetani ila nguvu za kumshinda Bado huna..

Kuokoka na kuishi wokovu ni vitu viwili tofauti...
 
Hapa ukiwa na mtu hata yule mtenda mabaya hawezi kukubadili maana unauwezo...
Mtume Paulo aliweka wazi kwa hili ".... Nilipokuwa kwa myunani nalikuwa kama myunani ili nimpate myunani....." Paulo alikuwa na nguvu hiyo
Ambaye umeokoka alafu huna nguvu za Rohoni ni rahisi kutekwa maana umemkataa shetani ila nguvu za kumshinda Bado huna..
Hao wasio na nguvu ni wakurupukaji sana na ndio wanaiharibu ile maana ya agizo kuu la Yesu
 
Hapa Sasa tumeelewana..

Ni hivi, ukiwa umeokoka kweli nasema kweli utapokea nguvu za Roho Mtakatifu...

Ukishasipokea hizo nguvu utakuwa inauwezo wa kuona yaani macho ya Rohoni na nguvu za Rohoni..

Hapa ukiwa na mtu hata yule mtenda mabaya hawezi kukubadili maana unauwezo...

Ambaye umeokoka alafu huna nguvu za Rohoni ni rahisi kutekwa maana umemkataa shetani ila nguvu za kumshinda Bado huna..

Kuokoka na kuishi wokovu ni vitu viwili tofauti...
Bado Mungu atakutaka ujitenge nao hata kama hizo nguvu unazo huwezi kuokoka alafu ukarudi Kwa marafiki zako wanaotukana na kuongea maongezi machafu na wamekataa kubadilika ukashiriki maongezi yao.Huo sio mpango wa Mungu.
 
Yesu mwenyewe alikula na alikaa na wenye dhambi, hata wale waliotaka kumuua alikuwa nao.
Tuko katika nyakati ambazo watu tunapenda uongo sana na kweli ni kitu tusichopenda kusikia.

Yes hakukaa na wenye dhambi kwa namna unavyoiweka, Yesu alikuwa hapo kuleta kuleta badliko na sio kupiga soga.

Siku utakayokaa na rafiki zako ukawa unasema kweli ya wokovu na si ya dini au dhehebu marafiki zako watakukimbia.

Ila wapo around na wewe kwasababu hawaoni hilo badliko unalosema unalo.
 
Ukienda kichwa kichwa utakutana na hii "Paulo namjua na Yesu namjua, na wewe ni nani?"

Hapo kabla hujajibu swali unapokea ngumi za uso, hujakaa sawa unapigwa ngwala....

Kuhubiri injili bila nguvu ya Roho Mtakatifu mtapigwa sana na wenye mapepo [emoji23][emoji23]
Paulo alitumia sana sana neno Upendo...

Hata sasa tulitumia upendo tutaweza
 
Mtu akigundua kuwa anapaswa kumwabudu Mungu na sio dini basi hakutakuwa na kujiona bora kuliko wengine,nadhani wanaofanya hivyo akili zao zimefunganishwa na dini.
 
Ukienda kichwa kichwa utakutana na hii "Paulo namjua na Yesu namjua, na wewe ni nani?"

Hapo kabla hujajibu swali unapokea ngumi za uso, hujakaa sawa unapigwa ngwala....

Kuhubiri injili bila nguvu ya Roho Mtakatifu mtapigwa sana na wenye mapepo [emoji23][emoji23]
Injili yenyewe ni uweza wa Mungu uletao wokovu.
Ngumi ipi ya kupambana na uweza wa Mungu?
Ingawa tunaenenda katika mwili,hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili.
 
Uko sahihi Mkuu! Lakini nachojua Walokole wanapaswa kujitenga na dhambi lakini SIYO kuwatenga wenye Dhambi.
 
Injili yenyewe ni uweza wa Mungu uletao wokovu.
Ngumi ipi ya kupambana na uweza wa Mungu?
Ingawa tunaenenda katika mwili,hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili.
Kuna injili za mihemko kama za wale wana wa Sewa wqliojipeleka kwenda Kuhubiri pasipo kutambuliwa hata na mapepo.

Ni kweli injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu, ila wapo wanaojipachika kazi pasipo kungoja nguvu za Mungu ziwe pamoja nao. Hakuagiza tufanye kazi bila kupokea nguvu
 
Back
Top Bottom