Walokole, tuache kujitenga na wenye dhambi

Walokole, tuache kujitenga na wenye dhambi

Mafundisho haya yaliwafanya wayahudi wamuone Yesu kama mwenye dhambi maana mara zote alikuwa anashinda na wale ambao hawakuonekana wenye haki..Ila mwisho wa siku alikuja kuwambia huwezi washa taa then ukaiweka uvunguni na mifano mingi sana alijaribu kuiweka wazi ili watu waelewe kwamba hakuja kwa ajili ya wenye kujiona safi bali wale ambao ni wadhambi.
Ukisoma Luka 7:37

Hapa kuna habari za Mariamu Magdalena mwanamke ambaye aliyehisishwa na dhambi...

Lakini Yesu alikuwa karibu naye na hakumtenga...
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa habari hapo juu,

Kama kuna kitu ambacho ndugu zangu walokole tunakosea ni hapo pa kujitenga na wenye dhambi.

Wokovu tunaupata kwa neema ya YESU mwenyewe, na hata kabla ya kuokoka wewe ulikuwa na dhambi.

Iweje Leo umeokoka unajitenga na wengine na kijiona Mtakatifu.

Yesu mwenyewe alikula na alikaa na wenye dhambi, hata wale waliotaka kumuua alikuwa nao.

Pia aliwajua, hilo halikuwa kawaida ila alikaa nao na kuongea nao.

Sasa iweje wewe uliyeokoka unashindwa kukaa na mwenye dhambi ikiwa tu huyo unayemuamini alikaa nao.

Kumbuka umepata neema ya kuokoka wewe ili uokoe na wengine na sio kujitenga nao.

Sasa wewe umeokoka unajiita mlokole wakati sio mwanafunzi wake, ukiokoka ndio ushakuwa mwanafunzi unatakiwa na wewe utangaze neno watu waokoke.

Kuokoka kwanza lazima uwe na Upendo, sasa umeokoka unachukia wenye dhambi umeokoka au unajidanganya.

Unasengenya watu, badala ya kuwaeleza kwa upendo namna ya wewe ulivyopata neema na wao wajue kuwa Yesu ni Bwana.

Kama walokole wangekuwa na Upendo wa kweli wa kukaa na wenye dhambi na kuwapa elimu ya kuwa hata wao walikuwa na dhambi ila Sasa wameokoka.

Hakika watu wangemjua Yesu Kristo kwa wepesi sana, ila majungu, masengenyo na kujitenga, ndio kunafanya watu waone Wokovu hauna faida.

Walokole tuache ubinafsi na tupende wenye dhambi..
mkuu nilikuwa sijui kama walokole hawana dhambi! hiv dhambi ni nini ebu nisaidie hapa kwanza
 
Back
Top Bottom