Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Umekuja na wazo zuri sana. Mm nawashauri kwanza wasiwe karib n wanasiasa. Pili wale wenye vigezo waangalie utaratib wa kwenda A level. Wengine kama wakiwez waende NACTE wanaweza saidiwa kupata vyuo.
 
Habari zenu wakuu,

Ni hakika kuwa mtu anapopatwa na msiba huhitaji faraja na ushauri wa maana utakaomsaidia mbele ya maisha yake kwani katika wakati huo huwa katika hali ya huzuni na mfadhaiko mkubwa.

Huu ni msiba kwa ndugu zetu,kwa kuwa hawakuwahi kuwaza kuwa itakuwa hivyo ilivyokuwa. Tamko limetoka kuwa wenye div one na two watatafutiwa namna,na wenye three wakatafute vyuo vingine.

Makundi haya yote yanahitaji ushauri wako.

Binafsi nawashauri wale wenye div three wawahi kufanya application za kozi za diploma au certificate nacte kabla muda haujafungwa ili kuwahi mwaka wa masomo 2016/2017.

Hata hao wenye one na two pia wanaweza fanya application kwa kuwa maamuzi ya serikali hayajawa wazi juu yao then baada ya maamuzi watapima wapi waende.

Pia wasikate tamaa, wana ufaulu mzuri tu,wana fursa nyingi za kufanya.

Wewe unawawashauri nini? Watu 8000 sio kidogo,toa mawazo yako,kwani kwa kukosa information juu ya fursa mbalimbali watu wengi wenye ufaulu wa wastani wamekata tamaa katika jamii yetu ya Tz na wale wa wakubwa na matajiri hata wapate ziro watatimiza tu,kwa kuwa wanajua njia na fursa.

Ahsanteni

Ushauri mzuri tu

Hata hivyo, ushauri wako umeangalia upande mmoja tu wa sifa, kwamba wana qualifications za kuwafanya wakasomee diploma ya ualimu au fani zingine zozote

Upande wa pili ambao haukuuangalia ni;

1. Gharama za kwenda kusomea diploma ambazo zina range kati ya 1,000,000 hadi 3,000,000 kwa mwaka. Tukumbuke kuwa hii special diploma in education for science teachers kwa UDOM ilikuwa inafadhiliwa na serikali kwa kuwapa mikopo hawa vijana 100% na ndiyo maana kuna vijana wengine walishachaguliwa kwenda High Schools lakini kwa kuvutiwa na programu hii ambayo ilikuwa wakimaliza wana ajiriwa moja kwa moja waliacha na kuamua kujiunga nayo. Hawa walikuwa ndo wazalendo wa kweli!!

2. Uchache/uhaba wa nafasi katika vyuo vya serikali vinavyotoa Stashahada ya ualimu especially ktk masomo ya sayansi ambako huko ingalau hata watoto wa maskini walala hoi wanaweza kumudu gharama za kusomesha watoto wao.

Option pekee ya nafasi inabakia kwenye vyuo vya binafsi ambako ndiko kuliko na gharama unbearable kwa watoto wa maskini ya kati ya milioni moja hadi milioni tatu au hata zaidi!!

.....Ndo kusema kuwa hoja sio sifa na muda kuruhusu kufanya application bali vikwazo vikubwa ni hivyo hapo juu!!
 
Mi nafikiri tatizo ni form 4 kuingia chuo kikuu kusomea bachelor. Kama ufaulu wa o' level wamefanya vyema, ila shida ni huo mfumo wa kubypass advanced level kuelekea degree ya kwanza. Wengi wana diploma then degree, kama hiyo special program award yake ni diploma then sijaona kosa lao
 
mkuu so wewe unategemea mheshimiwa alipewa zile taarifa! Think twice...
Sheria ya mtandao inatubana sana,Mimi ninachotaka kuandika nashindwa kwa sababu ya sheria .

Ila huyo aliyempa taarifa mh. rais wetu mpendwa kuwa wanafunzi 7000 ni vilaza inabisi afukuzwe kazi kwa sababu atakuwa kilaza .
 
Huyo mtoto alireseat akaendelea acheni ushambenga matokeo ya kureseat hamna mnaongea kishiranga kishambenga kikunanku kishombondokoloko kitawaponza
Muda wa kureset na muda aliyojiunga Udom vinapishana kama ile CV ya Agness Marwa.
Inahitaji unywe viroba Vingi sana ili utoe aibu uweze kutetea kauli ya Pombe kwenye hili sakata la Udom.
 
Umekuja na wazo zuri sana. Mm nawashauri kwanza wasiwe karib n wanasiasa. Pili wale wenye vigezo waangalie utaratib wa kwenda A level. Wengine kama wakiwez waende NACTE wanaweza saidiwa kupata vyuo.
Waende mahakamani kudai haki yao.
Muda waliopotezewa ni mkubwa sana.
 
Huyo mtoto alireseat akaendelea acheni ushambenga matokeo ya kureseat hamna mnaongea kishiranga kishambenga kikunanku kishombondokoloko kitawaponza
naona unafikiri kwa kutumia tumbo,kama alirisiti akaendelea mana yake alisoma five na six maana yake alidahiliwa kupitia tcu,iweje adahiliwe kupitia nacte


tusifayane wapumbavu kwa kuita watoto wa masikini vilaza huku wa ccm hata walifeli wanaendelea na shule
 
Watanzani wanahoji kwanini Jesca ambaye ni KILAZA namba moja anayesomea degree ya Rasilimali watu hapo hapo UDOM asifukuzwe ilhali ana ufaulu wa division FOUR?
Huyo yujo juu ya sheria hakuna wa kumgusa, mkuu wa chuo anamwogopa sasa anafanyiwa mipango ahamie chuo Fulani kule Marekani.
 
Magufuli ni dikteta. Hasikilizi watu. Anajifanya anajua kila kitu kwa sababu anajua boiling point ya silver. Hata hotuba anazoandikiwa baada ya watu kufanya uchunguzi hazisomi anasema tofauti.
Mtanyooka tu. Mlishazoea viongozi warasimu, wanaozungumza kwa kuwaonea aibu wale waliokaa pembeni yao, badilikeni kifkra ili maumivu ya moyoni na hasira, vipungue kama sio kuwatoka kabisa.
 
Mtanyooka tu. Mlishazoea viongozi warasimu, wanaozungumza kwa kuwaonea aibu wale waliokaa pembeni yao, badilikeni kifkra ili maumivu ya moyoni na hasira, vipungue kama sio kuwatoka kabisa.
Nani anyooke mbona Lugumi kawaweka Mfukoni? Mabehewa feki ya Mwakyembe yamewashinda hata NSSF mnapaogopa? Siku mkimaliza hivi vimeo vya Escrow, NIDA, IPTL, ATC, TTCL, Chenji ya Rada, chenji ya Bunge la katiba, kivuko nk ndipo uje na hilo neno kunyooka.
 
Nani anyooke mbona Lugumi kawaweka Mfukoni? Mabehewa feki ya Mwakyembe yamewashinda hata NSSF mnapaogopa? Siku mkimaliza hivi vimeo vya Escrow, NIDA, IPTL, ATC, TTCL, Chenji ya Rada, chenji ya Bunge la katiba, kivuko nk ndipo uje na hilo neno kunyooka.
Umesahau kuweka kimeo cha richmond, ambacho kilibadilisha kabisa maisha ya mgombea urais wa UKAWA mwaka jana.
 
Movie inanoga....mpaka ofisa wa chini kabisa....msemaji wa UDOM amepingana na magufuli bila woga kabisa.....kuna mahali nchi hii haiko sawa,nampongeza sana msemaji wa UDOM ....siyo Yale mazee yanayosema yanaogopa kufukuzwa kazi
...

....yah bila woga ni Haki tu
 
Kama baba Jesca kashindwa kutofautisha Division one two three na four na kuzichanganya na kuziita vilaza,pia kashindwa kutofautisha diploma na degree kisha kuwatimua Udom na kusahau kuwa wakati huo huo mwanae Jesca Division 4.30 yupo pale anasoma degree huku nae ni Kilaza, Je ataweza kweli kulielewa hili neno "Double Standard"? Si unamchanganya tu mkuu.

Hahaha nmejikua nacheka kwa sauti pekee yangu
 
Kihongwe wewe. Yalete hayo matokeo ya kureseat!! Kama hauna funga hilo bakuli lako.Watu tumechoshwa na mambo ya kipuuzi ndani ya nchi hii wewe unaleta upuuzi wako.
Ameenda kusali kwa mzee wa upako kabla ya kuifuta hii laana ya UDOM
 
Itoshe kusema kwamba Rais Magufuli ambaye ni baba Jesca John Magufuli, ambaye alipata division 4 ya 30, ambaye bado yupo Chuoni Udom anasoma degree muda huu licha ya wenzake kutimuliwa wakiwa na Division one two na three, ambaye kwa mujibu wa baba yake nae ni Kilaza (Jesca), basi yeye Magufuli nae ni Kilaza kwa sababu anakurupuka na kuropokaropoka bila mpangilio.

Mbona hapa unamsema vibaya Mh wetu?
 
Ahsante sana Mkuu, juzi niliandika hapa kuna kila dalili upstairs ya huyu mtu haiko sawa.

Unahitaji saikolojia ya juu kugundua tatizo la ugonjwa wa akili alionao mtu mzima. Kuna mambo yanaendelea naona kabisa huyu mtu hayuko sawa!
 
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
View attachment 353745
Wawa ni wanafunzi Miongoni mwao wapo walioweza kuathirika na timua hiyo, wamelazimika kukutana na vyombo vya habari katia kujadili suala hilo ambalo mpaka sasa hakuna mwenye tamko la mwisho zaidi ya mheshimiwa Rais wa jamhuri wa Tanzania

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.



Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?

=========================

Tamko la Wanafunzi waliofukuzwa

=========================

Ndugu Waandishi wa habari,

Awali yayote tunapenda kupongeza jitihada kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha inaboresha mfumo wa Elimu nchini.

Pamoja na ukweli kwamba, kumekuwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Elimu haswa katika awamu hii ya Uongozi wa Mh. Raisi, John Pombe Makufuli. Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unasikitishwa na kulaani baadhi ya maamuzi yaliyokwishafanyika na kukiuka utu, haki za Wanafunzi na vile vile taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.

Kuhusu Sakata la Kufukuzwa Wanafunzi UDOM

Mumesikia hoja za viongozi mbalimbali juu ya sakata la Wanafunzi Waliosimamishwa UDOM, mmesikia hotuba ya Mh. Joyce Ndelichako, Waziri mwenye dhamana katika wizara ya Elimu, lakini vile vile mmesikia hotuba ya Mh. Raisi, John Pombe Makufuli aliyoitoa akiwa chuo kikuu cha taifa (UDSM) tar. 02.06.2016

Tangu tar. 28 mei 2016, mara baada ya agizo la Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (MoEST) la kuwarejesha nyumbani Wanafunzi takribani 7802 Mtandao huu umekua ukifanya tafiti za kina kupitia idara yake (Reseach& Training Department) na kupata taarifa za pande zote mbili kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa “Wahanga(Wanafunzi waliofukuzwa) na Watawala(Wizara ya Elimu) ”.

Tumejiridhisha kwamba kitendo kilichofanywa dhidi ya Wanafunzi wa UDOM ni ukiukwaji mkubwa wa haki za Wanafunzi ambacho kilikuwa kwanza cha kimabavu na hakikuzingatia kabisa utu wa Wanafunzi husika.

Taarifa zilizotufikia ni kwamba Wanafunzi walifukuzwa kama Wakimbizi ndani ya nchi yao, Polisi walizagaa kila kona na bunduki zao kama wanafukuza majambazi, hofu ilitanda na wanafunzi wengine kuogopa kurudi chuoni kwa hali ilivyokuwa. Mtandao huu unasikitishwa kwa matumizi makubwa ya vyombo vya dola lakini vile vile madhara yaliyowakumba Wanafunzi husika wakati wa zoezi la kuwaondoa chuoni.

Chimbuko la Mgogoro:

Ikumbukwe, wakati wa uongozi wa Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu kama vile Mamlaka ya Elimu (TEA), Tume ya vyuo vikuu (TCU), Mamlaka ya vyuo vya Ufundi (NACTE) na wadau mbali mbali a Elimu, waliadhimia na kuzindua program maalumu ya kusomesha waalimu wa masomo ya Sayansi katika shule za sekondari nchini ili kutatua changamoto za uhaba wa waalimu wa masomo ya sayansi.

Lakini ili kupata waalimu wenye sifa Serikali ikaweka sifa za Udahili kwamba itakuwa kwa wahitimu wa kidato cha nne tu waliopata daraja la 1,2 na 3 pia wawe na ufaulu wa alama A” au B” kutoka masomo ya sayansi. Na serikali ikawashawishi kwa ahadi ya kuwapa mkopo kwa 100%.

Tumeshangazwa kwamba, Sababu za kusimamishwa masomo wanafunzi hawa zimeendelea kubadilika badilika, sababu ya kwanza kabisa, ambayo ilisemwa na Prof. Joyce Ndelichako Bungeni ni Mgomo wa Wahadhiri uliotokana na kukosa posho za kuwafundisha Wanafunzi husika, Sababu ya pili ni wanafunzi kukosa sifa.

Mtandao huu umejiuliza, Kama suala kuu ni vigezo kwanini serikali isingeweka utaratibu maalumu wa kuwaondoa wanafunzi wasio na sifa na kuwawajibisha wale waliowadahili kinyume na standard zilizowekwa na serikali?

1. Tunapenda Kutumia fursA hii kukanusha taarifa zote za uongo zilizotolewa na watawala/Viongozi dhidi ya wanafunzi husika. Na kumekuwa na utamaduni wa Watawala kutumia Vyombo vya habari(Media coverage) kama silaha ya kupotosha taarifa kwa umma(Taarifa hii itasomwa na muwakilishi wa wahanga wa Wanafunzi (UDOM)

Ombi letu.
1. Tunaiomba serikali kupitia wizara yake ya Elimu ifanye hima kuwarudisha Wanafunzi husika ili kutoendelea kupoteza rasilimali muda wa wanafunzi husika

2. Kama hotuba ya Mh. Raisi hapo juzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, akikiri kwamba kunawanafunzi wasio na vigezo walidahiliwa. Mtandao huu unaomba waliohusika kuwadahili wawajibishwe haraka iwezeanavyo lakini vile vile wanafunzi wafidiwe Rasilimali fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni.

Hatma ya Wanafunzi (UDOM)
Kama itatokea, kunamwanafunzi au kundi Fulani la Wanafunzi, halitopewa haki zake, Mtandao huu utashirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu zikiwemo azaki zinazojihusisha na masuala ya utetezi kisheria kutafuta haki za Wanafunzi husika mahakamani

Chanzo cha Migogoro katika Sekta ya Elimu Nchini.

v Kutokuwa na Muafaka wa Kitaifa katika Mfumo wa Elimu.

Mtandao huu unaamini kwamba haya yote ni madhara ya kutokuwa na muafaka wa kitaifa/Msimamo wa itaifa katia Sekta ya Elimu nchini. Kwa mda mrefu, mfumo wetu wa Elimu, Sekta ya Elimu nchini imekuwa inaendeshwa na kiwango cha utashi wa Waziri wa Elimu aliyepo madarakani na sio kuongozwa na dira/Muafaka/Msimamo wa kitaifa katika sekta ya Elimu.

Tumeshuhudia, Mawaziri wa Elimu tofauti tofauti, katika awamu tofauti tofauti za uongozi tangu uhuru wa nchi hii (Mh.Jumanne Maghembe, Mh, Joseph Mongai, Mh. Shukuru Kawambwa na sasa Mh. Joyce Ndalichako), wakifanya maamuzi kutokana na kiwango cha utashi wao na mapenzi yao. Hii ni hatari katika taifa letu na imesababishwa na ukweli kwamba taifa limekosa dira/Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.

Hitimisho.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unaamini kwamba kilichotokea Chuo Kikuu cha DODOMA kitakuwa msingi wa Serikali kupitia Wizara ya Elimu kuanza harakati rasmi za kimapinduzi za kuunganisha wadau wote wa Elimu nchini ili kuwa na mjadala mpana wa kitaifa wa namna ya kufikia Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.

Vile vile Mtandao huu umeshaandaa waraka maalumu kwa Waziri wa Elimu unaotoa muongozo wa namna taifa litakavyofanikisha kuwa na Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini ambao tutauwasilisha wizarani mapema wiki ijayo.

Mwisho kabisa, tunaomba viongozi wote wa dini na wale wanaoamini, kuendelea kumwombea Mh. Raisi n a viongozi wengine ili waongoze taifa hili kwa hekima na busara na kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.
Mungu wabariki vilaza wote wa Tanzania .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom