Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses
By Waandishi wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.



Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?
humo kuna vilaza watoto wa vigogo wenye d mbili. hao ndio lazima kutemwa na wahusika kuwadahili wawajibishwe. programu ibakie na div i&ii wa sayansi tu ndio waendelee na ikibidi wsfidiwe usumbufu. wanaopiga kelele wanataka kutubabaisha ili taifa liendelee kubeba makapi kama ndio waalimu wa sayansi.
 
Tatizo mnaongea sanaaaaa ila maamuzi ya Magufuli hayarudi nyuma
Haiwezekani serikali ibebe mzigo wakati wangeweza enda soka A level
Hivi watu kama nyie mlienda shule kufanyaje, kama kitu kidogo kama hiki unashindwa kukielewa, maisha yako unayaendeshaje?
 
JPM wangu weeee kalishwa kasa! Kama kweli hakuna Kilaza.....ni hatari kwa nchi kumdanganya President! Isije kutokea kumbe Kilaza ni Jesca pekee alieko UDOM! Naendelea kula pop corn movie ikiendelea!! Aje aombe radhi kwa lugha ya kuudhi!
Una hakika gani kwamba waliosema waliofukuzwa ni ya kweli, tuwe watulivu serikali imeahidi kwamba watarejeshwa kuendelea na masomo wasio na sifa hawataruhusiwa.
 
JPM hana analolijua kuhusu hao wanafunzi wa UDOM
 
Hahahahaha ungemuuliza kuwa alirisiti lini, Matokeo yakatoka lini, akadahiliwa lini, akaanza masomo lini, na admission akapata lini hadi Leo awe Mwaka wa Pili....
Bahat mbaya uyu mtu anaweza kuwa hajui hata nacte na tcu ni kitu gani
So msimlaumu
 
Kwa huu utofauti wa kauli,mh Ndalichako,msemaji wa chuo na mwakilishi wa wanafunzi wanaongea kauli sawa.Mh JPM anasema walikuwa ni vilaza.Sasa tuanzie hapa kujua ukweli uko wapi.Kisha tutafute suluhu.Pia napata mashaka kuwa Mh Raisi anaweza kuwa anadanganywa
Ninachokifahamu mimi ni kwamba, baada ya mpango huo kukubaliwa na bunge kusaini sheria, JK aliishawishi Benki ya Dunia kugharamia sehemu ya mpango huo, kuna taarifa benki ya dunia, ambayo ndio ilikuwa ikitoa fedha za kuwalipa walimu, imesitisha mpango huo; haijaeleweka kama kusitishwa huko kuna uhusiano na kusitishwa kwa misaada mingine kama ile ya MCC na nchi nyingine wahisani kutokana na kusinginwa kwa demokrasia au lau. Ila hili halizungumzwi!
 
Kwa huu utofauti wa kauli,mh Ndalichako,msemaji wa chuo na mwakilishi wa wanafunzi wanaongea kauli sawa.Mh JPM anasema walikuwa ni vilaza.Sasa tuanzie hapa kujua ukweli uko wapi.Kisha tutafute suluhu.Pia napata mashaka kuwa Mh Raisi anaweza kuwa anadanganywa
Jpm alivyoona mwanawe kapokelewa udom kwa shinikizo basi akajua udom ni chuo kinachopokea vilaza. Basi akakurupuka kusema wale 7000 ni vilaza warudi nyumbani. Kumbe anayestahili kuondolewa ni jeska.
 
Watanzani wanahoji kwanini Jesca ambaye ni KILAZA namba moja anayesomea degree ya Rasilimali watu hapo hapo UDOM asifukuzwe ilhali ana ufaulu wa division FOUR?
Baba jesca katia pamba masikioni na miwani ya mbao kabisaa labda uharamu wa jesca haumuhusu kwa sababu jesca anasomea kuwait kwa gadafi na sadam.
 
Huyo msemaji wa udom nae anatuchanganya.anawezaje kusema kuwa wanafunzi walofukuzwa wana ufaulu mzuri wa grade 1,2and 3.!!! inamaana hajui kama jesca John yupo UDOM?
km jesca amedahiliwa UDOM,uwezekano wa kwepo kwa wanafunzi wa aina yake upo.cha msingi UDOM waweke file zima la wanafunzi hao tuone matokeo yao.
Hao ni special program. Sio wa degree.

Tatizo kubwa la serikali nadhani ni pesa na vipaumbele. Mababa humu JF wanajua wanavyokuwa wakali majumbani wanapokuwa hawana kitu mfukoni.

Kitu umuhimu ni serikali ku retreat na kuangalia vipaumbele vyake na kuona pesa kidogo inayopatikana inagawanywaje. Waangalie elimu msingi, wazazi tuchangie angalau kidogo. Wote tunajua gharama kubwa iko kwenye elimu ya juu na huko ndio majority tunahitaji msaada.
 
Rais kwenye hili alikurupuka kama kawaida yake haiwezekani mwanafunzi anayesoma diploma miaka 3 akiwa na ufaulu mzuri wa kidato cha nne umfukuze chuo.
Mpaka sasa nimeshindwa kujua mantiki ya rais kwamba ukiwa form 4 huuruhusiwi kusoma chuo kikuu hata kama ni diploma kwa miaka 3? Mbona huu ni mfumo wa kawaida kabisa, rais anashindwa kujua hata vyuo vikuu wanatoa diploma na cheti.
 
Ndio ni Vilaza hivi huwa nashangaa kweli MTU unapataje daraja LA tatu katika matokeo ya kidato cha NNE.....si ukilaza huu
 
Kwenye hili sakata la Dart mfalme yuko uchi!
Wana propaganda magogoni inabidi wabuni propaganda ya kuhamisha upepo huku hili jambo likishughulikiwa fasta.
Hahahaha inabidi magufuli afanye ziara kiwanda cha sukari mtibwa, maana siku hizi simskii kabisa akigusia sukari na bei yake mtaani ni 4500 kwa kilo..... Kaz ipo
 
Sheria ya mtandao inatubana sana,Mimi ninachotaka kuandika nashindwa kwa sababu ya sheria .

Ila huyo aliyempa taarifa mh. rais wetu mpendwa kuwa wanafunzi 7000 ni vilaza inabisi afukuzwe kazi kwa sababu atakuwa kilaza .
 
Tatizo mnaongea sanaaaaa ila maamuzi ya Magufuli hayarudi nyuma
Haiwezekani serikali ibebe mzigo wakati wangeweza enda soka A level
mzigo?
kumbe wangeenda advance then wakarudi makwao kuuza mbege? kwasababu kama wataenda chuo mzigo si uleule tu?
 
Kama waliowadahili walifanya makosa kuchukua vilaza,mimi naona tungeanzia pale. kama yale yaliyowakuta wale waliodahili wanafunzi wa st.Joseph. lakini watu waliowadahili wanapeta ila wanamsulubu mdahiliwa hapo hapako sawa.mbaya zaidi hawa watoto hawakuomba hii kozi ila NACTE wao ndio waliwachagua tena baada ya kusema kutokana na ufaulu kuwa mkubwa wa wanafunzi wa kidato cha nne kunapelekea kuna wengine wamefaulu ila hawatapata nafasi.serikali ikawataka wanafunzi hao kutokata tamaa badala yake watapangwa kwenye vyuo vingine ili kuhakikisha wote waliofaulu wanaendelea na masomo. kundi la kwanza lilipelekwa UDOM na kundi lingine lilipelekwa katika vyuo vya afya. haikutokea kwa bahati mbaya ni mikakati na sera ya serikali yetu wenyewe.
Magufuli angalia jinsi gani utawasaidia hawa watoto waweze kuendelea na masomo kwasababu kuwatimua pekee kwa makosa ambayo sio ya kwao hamuwatendei haki na mmeshawapotezea muda na matumaini katika maisha yao.
 
Sheria ya mtandao inatubana sana,Mimi ninachotaka kuandika nashindwa kwa sababu ya sheria .

Ila huyo aliyempa taarifa mh. rais wetu mpendwa kuwa wanafunzi 7000 ni vilaza inabisi afukuzwe kazi kwa sababu atakuwa kilaza .
 
Huyo msemaji wa udom nae anatuchanganya.anawezaje kusema kuwa wanafunzi walofukuzwa wana ufaulu mzuri wa grade 1,2and 3.!!! inamaana hajui kama jesca John yupo UDOM?
km jesca amedahiliwa UDOM,uwezekano wa kwepo kwa wanafunzi wa aina yake upo.cha msingi UDOM waweke file zima la wanafunzi hao tuone matokeo yao.
Mkuu kumbuka Jesca John Magufuli hajafukuzwa ana division 4.30. Yuko Udom anasoma degree. Huyo msemaji anaongelea kwamba wanafunzi waliofukuzwa walikuwa na Sifa, narudia tena, wanafunzi waliofukuzwa, sio Jesca aliyeko Chuoni.
 
Kwa huu utofauti wa kauli,mh Ndalichako,msemaji wa chuo na mwakilishi wa wanafunzi wanaongea kauli sawa.Mh JPM anasema walikuwa ni vilaza.Sasa tuanzie hapa kujua ukweli uko wapi.Kisha tutafute suluhu.Pia napata mashaka kuwa Mh Raisi anaweza kuwa anadanganywa
Hakuna hata anayemdanganya yeye mwenyewe hafuatilii taarifa mbalimbali,kitu kibaya zaidi anapenda kuhutubia bila kusoma hotuba kwahiyo anaenda chaka vibaya mno.
 
Back
Top Bottom