Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Habari zenu wakuu,

Ni hakika kuwa mtu anapopatwa na msiba huhitaji faraja na ushauri wa maana utakaomsaidia mbele ya maisha yake kwani katika wakati huo huwa katika hali ya huzuni na mfadhaiko mkubwa.

Huu ni msiba kwa ndugu zetu,kwa kuwa hawakuwahi kuwaza kuwa itakuwa hivyo ilivyokuwa. Tamko limetoka kuwa wenye div one na two watatafutiwa namna,na wenye three wakatafute vyuo vingine.

Makundi haya yote yanahitaji ushauri wako.

Binafsi nawashauri wale wenye div three wawahi kufanya application za kozi za diploma au certificate nacte kabla muda haujafungwa ili kuwahi mwaka wa masomo 2016/2017.

Hata hao wenye one na two pia wanaweza fanya application kwa kuwa maamuzi ya serikali hayajawa wazi juu yao then baada ya maamuzi watapima wapi waende.

Pia wasikate tamaa, wana ufaulu mzuri tu,wana fursa nyingi za kufanya.

Wewe unawawashauri nini? Watu 8000 sio kidogo,toa mawazo yako,kwani kwa kukosa information juu ya fursa mbalimbali watu wengi wenye ufaulu wa wastani wamekata tamaa katika jamii yetu ya Tz na wale wa wakubwa na matajiri hata wapate ziro watatimiza tu,kwa kuwa wanajua njia na fursa.

Ahsanteni
 
Mm ni moja wahanga hao yaani mtoto wangu amepata matatizo hakika nimekata tamaa ikiwa serikali iliwaahidi tena kupitia bunge sasa nani atawasaidia nishida
 
Nakumbuka Magufuli alisema

'wachina ndio marafiki wa kweli wengine ni wanafiki'

huku tz ikitegemea na kupokea misaada toka US na UK na Kikwete akasema misaada kwa sasa ni muhimu
'wanaopita mwendokasi chomoeni matairi muuze'

alisema hivyo kwa tone ya kusisitiza wala sio ya utani kwenye tv ya taifa na mbele ya balozi wa China

'wanaficha sukari ndio maana inapanda bei, na tutakamata sukari yao tutagawa bure, serikali ya magufuli haishindwi'

mpaka leo hii nyie wote ni mashahidi juu ya hili swala la sukari lilivyo

'sukari inayoagizwa nje ni ya bei nafuu kwa kuwa inakuwa imekwisha expire na haifai kwa matumizi ya binadamu'

huyu mkulu hii kauli hana uhakika nayo, na ni ya kukurupuka pia

'tulishindwa kesi ya samaki kwa kuwa DPP alikuwa amewapunguzia mashitaka'

huku akiwa hana uelewa mzuri juu ya sheria na hakuwa na uhakika walishindwa kwa sababu gani.

' migomo mingine inamalizwa kwa kufukuza tu, nilikuwa nasubiria na wanafunzi wengine wa Dodoma wagome, wangeondoka wote!!'

list ya kauli tata ni nyingi hapa ni chache tu.......

gazeti la Economist liliandika Huyu rais ni mzuri lakini ni mkurupukaji, ikulu ikatoa taarifa rasmi ya kupinga......

" mahakama zipo, ila hawataki kwenda mahakamani wanataka Magufuli aingile kati.... mimi siingirii na ore wao watakao leta fyokofyoko" kumbe katiba hairuhusu mahakama yeyote Tz kusikiliza/pinga maamuzi ya Tume kwenye nafasi za uraisi .....
 
Inawezekanaje wanafunzi wooote 7000 wakawa hawafai. Hakukuwapo hata 200, hata 100, hata 19 wazuri???!!!! Nina wasiwasi Mkubwa. Inawezekana kabisa mkuu wa nchi akawa na allergy ya kulipa madeni makubwa has a yanapofika mezani kwake kama wazuri wa fedha no2. Hiki ni kisingizio tu na ndio maana anasema nilikuwa natafuta sababu tu ili niwafukuze. Si jambo jema mlezi wa taifa kutafuta sababu za kuadhibu watu wake. Ajitafakari na laweza kuja tatizo kubwa badala ya kulitatua akaliongeza zaidi. Mfano mzuri ni sukari.
Tatizo ni malipo ya wahadhiri.

Hizi habari za qualifications za wanafunzi ni uongo tu.

Ni jambo la aibu sana kuona rais aliyejinadi kama mtetezi wa wanyonge anakuja kuwafukuza wanafunzi chuoni kama mbwa na kutoa sababu za uongo.
 
kuna division three ambazo combination zipo vizuei na pia huwa kuna division three wenye point kumzidi div one au two!

Div three sio failure wapo wachache huwa failure
 
Ushauri wangu kwao wasikubali tu kutumiwa na wanasiasa matukio kwa faida za kisiasa kwani watakuja kuachwa solemba ikifikia swala lao so habari kubwa tena.
 
Waungane wapambane kwa pamoja watafanikiwa...wasigawanyike..
..wahakikishe wanateua wawakilishi kwenda kumuona waziri Mkuu bungeni na ikibidi viongozi wa kambi ya upinzani, hii hoja iingie bungeni na ijadiliwe,waende taasisi za haki za binadamu,wawasiliane na serikali yao ya wanafunzi na serikali nyingine za wanafunzi zitoe matamko kutoka kila kona ya nchi
 
mchezo wa huu hauhitJi nguvu msubilie serikali iwapangie
 
Prof. Kitila Mkumbo aliiambia jamii kupitia kipindi cha saa 3 usiku cha ITV cha Kipima Joto kuwa kuna vilaza 80, hao wamemshangaza kwa nini seneti na mgt ya UDOM haikuliona hilo.

Alienda mbali kwa kusema Div 1&2 ni wachache sana kama 15% na Div 3&4 ni 80%. Sasa Prof. Mkumbo aje hapa atueleze kuwa kati yake na hao wanafunzi nani muongo.

Kitila, Professor mbobezi hii issue lazima ikushushe heshima kama ulisema kwa unazi. Njoo hapa nawe ulete yale uliyoyatapika juzi usiku.
 
ni kweli umoja ni nguvu, na natumai watapita hapa na watafanyia kazi ushauri.
 
kuna division three ambazo combination zipo vizuei na pia huwa kuna division three wenye point kumzidi div one au two!

Div three sio failure wapo wachache huwa failure
ni sawia kabisa, unawashauri wenye comb zilizobalance waombe shule za advance?
 
kwani shida nn wenye vigezo washaambiwa wanaandaliwa utaratibu ikiwa ni pamoja na kutaftiwa wakufunzi sasa wanaweweseka nn?
Sijui kama tunaelewana!! Wale wote wana sifa kuwafukuza ni kosa kubwa na JPM amedanganywa...aibu!!
 
wamechelewa Muda wa application usha isha tangu tarehe 3 mwez wa 6
 
Sijui kama tunaelewana!! Wale wote wana sifa kuwafukuza ni kosa kubwa na JPM amedanganywa...aibu!!
sio wote wenye sifa mbona unalazimisha upuuzi wake uwe na maaana rudia kusikiliza ile hotuba kama kasema wenye sifa anawaandalia utaratibu shida kwako ipo wapi ?Anna Kilango alisema hakuna watumishi hewa yeye akakuta sasa hofu yako nn?

Naakasema prof kikula nimemuuliza kwann umechukua hawa wengine hawana sifa akasema alilazimishwa .

Kama kasema wenye sifa watarudi hata kama ni wote kwa msemo wako shida ipo wapi ?
 
Mhhhh hili tamko la wanafunzi wa UDOM ni taabu kweli kweli, utafikri limeandikwa na mtoto wa kidato cha nne shule za Kata. Yaani mtu uko Chuo Kikuu hata jina la Rais hulijui? Eti Makufuli (huyu ni Rais wa wapi?), jina la waziri wa elimu hulijui? Eti Ndelichako! Mara eti Mongai. Huyu aliyeandika hili tamko hastahili kuwepo hapo chuoni, arudi kidato cha pili kwanza.
 
Habari zenu wakuu,

Ni hakika kuwa mtu anapopatwa na msiba huhitaji faraja na ushauri wa maana utakaomsaidia mbele ya maisha yake kwani katika wakati huo huwa katika hali ya huzuni na mfadhaiko mkubwa.

Huu ni msiba kwa ndugu zetu,kwa kuwa hawakuwahi kuwaza kuwa itakuwa hivyo ilivyokuwa. Tamko limetoka kuwa wenye div one na two watatafutiwa namna,na wenye three wakatafute vyuo vingine.

Makundi haya yote yanahitaji ushauri wako.

Binafsi nawashauri wale wenye div three wawahi kufanya application za kozi za diploma au certificate nacte kabla muda haujafungwa ili kuwahi mwaka wa masomo 2016/2017.

Hata hao wenye one na two pia wanaweza fanya application kwa kuwa maamuzi ya serikali hayajawa wazi juu yao then baada ya maamuzi watapima wapi waende.

Pia wasikate tamaa, wana ufaulu mzuri tu,wana fursa nyingi za kufanya.

Wewe unawawashauri nini? Watu 8000 sio kidogo,toa mawazo yako,kwani kwa kukosa information juu ya fursa mbalimbali watu wengi wenye ufaulu wa wastani wamekata tamaa katika jamii yetu ya Tz na wale wa wakubwa na matajiri hata wapate ziro watatimiza tu,kwa kuwa wanajua njia na fursa.

Ahsanteni
 
Awa watoto wamekosea sana kwenda kwenye media itawagharimu mno.. Siasa ni kitu kibaya sana hapa wanalazimisha mafahali wawili wapambane ila watakaoumia ni wao.
 
Mm ni moja wahanga hao yaani mtoto wangu amepata matatizo hakika nimekata tamaa ikiwa serikali iliwaahidi tena kupitia bunge sasa nani atawasaidia nishida
Pole sana ndugu ila najiuliza wewe na wazazi wengine wenye watoto hao sijui mlimachagua nani mwaka jana maana watanzania ni wepesi wa kulaumu na kulalamika alafu uchaguzi ukija kuanzia diwani,mbunge mpaka raisi wote mtu anachagua kutoka CCM.
 
Back
Top Bottom