Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

thesym

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
3,866
Reaction score
4,854
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
IMG_20160604_122714.jpg

Wawa ni wanafunzi Miongoni mwao wapo walioweza kuathirika na timua hiyo, wamelazimika kukutana na vyombo vya habari katia kujadili suala hilo ambalo mpaka sasa hakuna mwenye tamko la mwisho zaidi ya mheshimiwa Rais wa jamhuri wa Tanzania

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.

Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?

=========================

Tamko la Wanafunzi waliofukuzwa

=========================

Ndugu Waandishi wa habari,

Awali yayote tunapenda kupongeza jitihada kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha inaboresha mfumo wa Elimu nchini.

Pamoja na ukweli kwamba, kumekuwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Elimu haswa katika awamu hii ya Uongozi wa Mh. Raisi, John Pombe Makufuli. Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unasikitishwa na kulaani baadhi ya maamuzi yaliyokwishafanyika na kukiuka utu, haki za Wanafunzi na vile vile taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.

Kuhusu Sakata la Kufukuzwa Wanafunzi UDOM

Mumesikia hoja za viongozi mbalimbali juu ya sakata la Wanafunzi Waliosimamishwa UDOM, mmesikia hotuba ya Mh. Joyce Ndelichako, Waziri mwenye dhamana katika wizara ya Elimu, lakini vile vile mmesikia hotuba ya Mh. Raisi, John Pombe Makufuli aliyoitoa akiwa chuo kikuu cha taifa (UDSM) tar. 02.06.2016

Tangu tar. 28 mei 2016, mara baada ya agizo la Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (MoEST) la kuwarejesha nyumbani Wanafunzi takribani 7802 Mtandao huu umekua ukifanya tafiti za kina kupitia idara yake (Reseach& Training Department) na kupata taarifa za pande zote mbili kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa “Wahanga(Wanafunzi waliofukuzwa) na Watawala(Wizara ya Elimu) ”.

Tumejiridhisha kwamba kitendo kilichofanywa dhidi ya Wanafunzi wa UDOM ni ukiukwaji mkubwa wa haki za Wanafunzi ambacho kilikuwa kwanza cha kimabavu na hakikuzingatia kabisa utu wa Wanafunzi husika.

Taarifa zilizotufikia ni kwamba Wanafunzi walifukuzwa kama Wakimbizi ndani ya nchi yao, Polisi walizagaa kila kona na bunduki zao kama wanafukuza majambazi, hofu ilitanda na wanafunzi wengine kuogopa kurudi chuoni kwa hali ilivyokuwa. Mtandao huu unasikitishwa kwa matumizi makubwa ya vyombo vya dola lakini vile vile madhara yaliyowakumba Wanafunzi husika wakati wa zoezi la kuwaondoa chuoni.

Chimbuko la Mgogoro:

Ikumbukwe, wakati wa uongozi wa Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu kama vile Mamlaka ya Elimu (TEA), Tume ya vyuo vikuu (TCU), Mamlaka ya vyuo vya Ufundi (NACTE) na wadau mbali mbali a Elimu, waliadhimia na kuzindua program maalumu ya kusomesha waalimu wa masomo ya Sayansi katika shule za sekondari nchini ili kutatua changamoto za uhaba wa waalimu wa masomo ya sayansi.

Lakini ili kupata waalimu wenye sifa Serikali ikaweka sifa za Udahili kwamba itakuwa kwa wahitimu wa kidato cha nne tu waliopata daraja la 1,2 na 3 pia wawe na ufaulu wa alama A” au B” kutoka masomo ya sayansi. Na serikali ikawashawishi kwa ahadi ya kuwapa mkopo kwa 100%.

Tumeshangazwa kwamba, Sababu za kusimamishwa masomo wanafunzi hawa zimeendelea kubadilika badilika, sababu ya kwanza kabisa, ambayo ilisemwa na Prof. Joyce Ndelichako Bungeni ni Mgomo wa Wahadhiri uliotokana na kukosa posho za kuwafundisha Wanafunzi husika, Sababu ya pili ni wanafunzi kukosa sifa.

Mtandao huu umejiuliza, Kama suala kuu ni vigezo kwanini serikali isingeweka utaratibu maalumu wa kuwaondoa wanafunzi wasio na sifa na kuwawajibisha wale waliowadahili kinyume na standard zilizowekwa na serikali?

1. Tunapenda Kutumia fursA hii kukanusha taarifa zote za uongo zilizotolewa na watawala/Viongozi dhidi ya wanafunzi husika. Na kumekuwa na utamaduni wa Watawala kutumia Vyombo vya habari(Media coverage) kama silaha ya kupotosha taarifa kwa umma(Taarifa hii itasomwa na muwakilishi wa wahanga wa Wanafunzi (UDOM)

Ombi letu.
1. Tunaiomba serikali kupitia wizara yake ya Elimu ifanye hima kuwarudisha Wanafunzi husika ili kutoendelea kupoteza rasilimali muda wa wanafunzi husika

2. Kama hotuba ya Mh. Raisi hapo juzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, akikiri kwamba kunawanafunzi wasio na vigezo walidahiliwa. Mtandao huu unaomba waliohusika kuwadahili wawajibishwe haraka iwezeanavyo lakini vile vile wanafunzi wafidiwe Rasilimali fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni.

Hatma ya Wanafunzi (UDOM)
Kama itatokea, kunamwanafunzi au kundi Fulani la Wanafunzi, halitopewa haki zake, Mtandao huu utashirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu zikiwemo azaki zinazojihusisha na masuala ya utetezi kisheria kutafuta haki za Wanafunzi husika mahakamani

Chanzo cha Migogoro katika Sekta ya Elimu Nchini.

v Kutokuwa na Muafaka wa Kitaifa katika Mfumo wa Elimu.

Mtandao huu unaamini kwamba haya yote ni madhara ya kutokuwa na muafaka wa kitaifa/Msimamo wa itaifa katia Sekta ya Elimu nchini. Kwa mda mrefu, mfumo wetu wa Elimu, Sekta ya Elimu nchini imekuwa inaendeshwa na kiwango cha utashi wa Waziri wa Elimu aliyepo madarakani na sio kuongozwa na dira/Muafaka/Msimamo wa kitaifa katika sekta ya Elimu.

Tumeshuhudia, Mawaziri wa Elimu tofauti tofauti, katika awamu tofauti tofauti za uongozi tangu uhuru wa nchi hii (Mh.Jumanne Maghembe, Mh, Joseph Mongai, Mh. Shukuru Kawambwa na sasa Mh. Joyce Ndalichako), wakifanya maamuzi kutokana na kiwango cha utashi wao na mapenzi yao. Hii ni hatari katika taifa letu na imesababishwa na ukweli kwamba taifa limekosa dira/Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.

Hitimisho.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unaamini kwamba kilichotokea Chuo Kikuu cha DODOMA kitakuwa msingi wa Serikali kupitia Wizara ya Elimu kuanza harakati rasmi za kimapinduzi za kuunganisha wadau wote wa Elimu nchini ili kuwa na mjadala mpana wa kitaifa wa namna ya kufikia Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.

Vile vile Mtandao huu umeshaandaa waraka maalumu kwa Waziri wa Elimu unaotoa muongozo wa namna taifa litakavyofanikisha kuwa na Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini ambao tutauwasilisha wizarani mapema wiki ijayo.

Mwisho kabisa, tunaomba viongozi wote wa dini na wale wanaoamini, kuendelea kumwombea Mh. Raisi n a viongozi wengine ili waongoze taifa hili kwa hekima na busara na kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.
 
JPM wangu weeee kalishwa kasa! Kama kweli hakuna Kilaza.....ni hatari kwa nchi kumdanganya President! Isije kutokea kumbe Kilaza ni Jesca pekee alieko UDOM! Naendelea kula pop corn movie ikiendelea!! Aje aombe radhi kwa lugha ya kuudhi!
 
Nakumbuka Magufuli alisema

'wachina ndio marafiki wa kweli wengine ni wanafiki'

huku tz ikitegemea na kupokea misaada toka US na UK na Kikwete akasema misaada kwa sasa ni muhimu
'wanaopita mwendokasi chomoeni matairi muuze'

alisema hivyo kwa tone ya kusisitiza wala sio ya utani kwenye tv ya taifa na mbele ya balozi wa China

'wanaficha sukari ndio maana inapanda bei, na tutakamata sukari yao tutagawa bure, serikali ya magufuli haishindwi'

mpaka leo hii nyie wote ni mashahidi juu ya hili swala la sukari lilivyo

'sukari inayoagizwa nje ni ya bei nafuu kwa kuwa inakuwa imekwisha expire na haifai kwa matumizi ya binadamu'

huyu mkulu hii kauli hana uhakika nayo, na ni ya kukurupuka pia

'tulishindwa kesi ya samaki kwa kuwa DPP alikuwa amewapunguzia mashitaka'

huku akiwa hana uelewa mzuri juu ya sheria na hakuwa na uhakika walishindwa kwa sababu gani.

' migomo mingine inamalizwa kwa kufukuza tu, nilikuwa nasubiria na wanafunzi wengine wa Dodoma wagome, wangeondoka wote!!'

list ya kauli tata ni nyingi hapa ni chache tu.......

gazeti la Economist liliandika Huyu rais ni mzuri lakini ni mkurupukaji, ikulu ikatoa taarifa rasmi ya kupinga......
 
Sasa kama msemaji wa UDOM anasema hao walioitwa vilaza walikuwa na ufaulu wa division one,two,na wachache three,mh rais atawaambia nini watanzania anapodai walikuwa na division four? Hii si ushahidi kwamba rais hapati taarifa sahihi na mwisho wa siku anafanya maamuzi ya kuumiza watu? Ni nani alimpelekea rais taarifa hizo? Mbona UDOM kupitia msemaji wao na bi ndalichako kauli zao zinafanana? Za rais zinatoka wapi na ni naani mpasha habari wake? Wangapi wameshaumia kwa staili hii tangu aingie madarakani? Hawa watoto wakienda mahakamani watashinda kwa hakika,serikali itachukua kodi za nani kuwalipa fidia? Hiyo fidia na kuwaacha waendelee kusoma kipi cha busara?
 
Itoshe kusema kwamba Rais Magufuli ambaye ni baba Jesca John Magufuli, ambaye alipata division 4 ya 30, ambaye bado yupo Chuoni Udom anasoma degree muda huu licha ya wenzake kutimuliwa wakiwa na Division one two na three, ambaye kwa mujibu wa baba yake nae ni Kilaza (Jesca), basi yeye Magufuli nae ni Kilaza kwa sababu anakurupuka na kuropokaropoka bila mpangilio.
 
JPM wangu weeee kalishwa kasa! Kama kweli hakuna Kilaza.....ni hatari kwa nchi kumdanganya President! Isije kutokea kumbe Kilaza ni Jesca pekee alieko UDOM! Naendelea kula pop corn movie ikiendelea!! Aje aombe radhi kwa lugha ya kuudhi!
Movie inanoga....mpaka ofisa wa chini kabisa....msemaji wa UDOM amepingana na magufuli bila woga kabisa.....kuna mahali nchi hii haiko sawa,nampongeza sana msemaji wa UDOM ....siyo Yale mazee yanayosema yanaogopa kufukuzwa kazi
 
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses
By Waandishi wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.

Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?[/QUOTE

Kumbe ni kweli wanakubali Kuwa hawana qualification Za kujiunga Na chuo kikuu. Hawajasoma high school wamekubalije kuingia chuo Kwa kucheza Na system. Nani akiyewadanganya Kuwa Hilo Jambo linawezekana? Hatuwezi Kuwa Na makomandoo Kwa mafunzo ya mgambo. You are not qualified mrudishwe wapi? Mlikubaliana Na wavunjautaratibu matapeli wa Karme illuminatas, Devils wakina kikwete Na Udini wake, he has destroyed our nation kabisa, NSSF Kupitia Dau alitoa hela zetu Chungu nzima zikiwemo Za watu wa Duni mbalimbali kumfurahisha kikwete, wakapeana kazi Kwa Udini wakina prof kikula wakina dr mlacha kwenda kujifunzia kazi huko. Na Nyie mkakubali mkijiona you are priviledged Wakati wenzenu wanasoma form 5 eti Nyie mliambiwa Muwahi Kupata kazi how about wenzenu? Hili ni jini Na shetani, mmekua initiated, Leo mnasema wafadhiliwe waliowaingiza huko Na Nyie mpone NO WAY, you are in it together, Kama mlivyofaidi pamoja, hivi kuna adhabu Kubwa Kwa your ring leader kikwete Kama kufikishwa h apo? Kwa nini Yeye Ndio asiwe mbele kutetea Kama hakubaliani kuwa akiwachezea? Mfuateni Yeye Hizi press conference zielekezwe Kwake Yeye Ndio wakuwajibu sio Magufuli. Hongera Magufuli Na Ndalichako Kwa kutumbua huu mjipu. Hakuna sympathy fanyeni kazi. Hakuna degree ya shortcut Ndio maana graduates wao wanachekesha,
 
Watanzani wanahoji kwanini Jesca ambaye ni KILAZA namba moja anayesomea degree ya Rasilimali watu hapo hapo UDOM asifukuzwe ilhali ana ufaulu wa division FOUR?
Kwa sababu baba yake ambaye ni Rais wa Tanzania ni Kilaza pia, na amezungukwa na washauri vilaza ambao hawajui kutofautisha Diploma na degree, hawajui kutofautisha Division one two three na four. Yaani vilaza wamekutana Ikulu.
 
Nimegunduwa hata ikulu nayo Ina vilaza wengi tu
Wasiwasi wangu ni kwamba inawezekana hili jambo halikujadiliwa hata kwenye Baraza la mawaziri...kama lingepita basi wasingepishana kauli,ndalichako na msemaji wa UDOM wana kauli moja,rais ana kauli nyingine, lingepita kwenye Baraza la mawaziri lazima wangeitisha ufaulu/matokea ya hao vijana,hii ingeuwa hoja kwamba hao vijana ni vilaza,hukohuko kwenye vikao vyao vya ndani, Pili lingefuata suala la milioni 800 wanazodai walimu,hili nalo si kubwa kwa serikali inayojigamba kuwa na makusanyo makubwa,wangebana huku na kule walipe waalim vijana wamalize shule,hizo hela walizobana kwenye semina na safari za nje wanapeleka wapi? Mbona Huduma za afya ziko vilevile?tunachoona ni ukosefu wa uongozi wa pamoja kati ya mawaziri na mwenyekiti wao rais..
Kuna mmoja anawavuruga
 
Huyo mtoto alireseat akaendelea acheni ushambenga matokeo ya kureseat hamna mnaongea kishiranga kishambenga kikunanku kishombondokoloko kitawaponza
 
Kwa sababu baba yake ambaye ni Rais wa Tanzania ni Kilaza pia, na amezungukwa na washauri vilaza ambao hawajui kutofautisha Diploma na degree, hawajui kutofautisha Division one two three na four. Yaani vilaza wamekutana Ikulu.
Dahh aisee we noma nenda shop upate nyota uvute khaaaa
 
Nakumbuka Magufuli alisema ' migomo mingine inamalizwa kwa kufukuza tu, nilikuwa nasubiria na wanafunzi wengine wa Dodoma wagome, wangeondoka wote!!'

Huyu rais noma
Wale watoto wa watu wanapakaziwa kwamba waligoma wakati waliogoma ni waalimu wao. Baba Jesca alitaka kufukuza Wanafunzi wa UDOM anajisahaulisha kwamba pale pale alipokuwa kuna wanafunzi walikuwa wamegoma na hakupenda kukemea wala kuchukua hatua yeyote yeye pamoja na Joyce wake, mbona wanakuwa na "Double Standards"!?.
 
Back
Top Bottom