Hii post nataka ibaki hapa hapa jukwaa la siasa maana inahusu mustakabali wa vijana wetu ambao wapo vyuoni
Nimeliona hili bandiko
Kesho nitakunywa sumu
Nimeshangazwa na kitendo cha bodi ya mikopo kuwapunja wanafunzi pesa yao ya kujikimu kwa madai ya muda wa masomo vyuoni ni mdogo kinyume na mkataba huu ni upumbavu wa hali ya juu.
Nitashangaa sana kusikia kwamba bodi ya mikopo wametumwa na Rais au hata waziri kufanya hilo kwa wanafunzi.
Pesa ya kujikimu vyuoni huwa ni laki 530000 wanapewa, lakini wamepewa laki mbili tu huku marejesho wakija kutakiwa kurejesha laki 530000 hiyo hiyo.
Loan board wamegeuka wabinafsi, watu wenye mihemko na wasiojali wanafunzi ambao wengi ni maskini.
Inashangaza sana na kusikitisha sana kwamba mpaka dakika hii wahusika wapo ofisini na wameachwa tu na hapo ndo naanza kuamini kwamba hii ni amri kutoka ngazi za juu.
Inasikitisha sana kuona hili limetokea na nikumbushe kwamba wanafunzi wa toka mwaka 2019 November hawajapewa laki mbili ya books and stationery ambayo hutolewa.
Swali hizi pesa kwani ni za bure?Jibu ni kuwa wanazilipia,na kinachoshangaza ni kuwa ijapo wamepewa laki 2 na mkataba umesema ni laki 5 watakuja kulipia hiyo laki 5 yote japo walipewa laki 2.
Nitashangaa sana kama loan board wanaweza kufanya maamuzi ya ajabu namna hii bila kuzingatia utashi na kanuni na wahusika wapo tu ofisini.