Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Kama hujawahi kutoka nje ya nchi na unataka kuona dunia ya kwanza ikoje nenda Dubai. Gharama hazitishi na visa yake inapatikana kirahisi. Nauli kwenda na kurudi around $500, hotel siku 3/4 around $200, maana yake ukiwa na $1,000 unapata na pocket money $300.

Au Airbnb badala ya hoteli
 
IMG_6573.jpeg

mtu aliyefika kwenye kuangalia dolphin Znz anipe rougly budget. 😋
Kuna dolphin Zanzibar?
 
Mkoa wa Mbeya mtu atembelee wapi na wapi
Kuna maeneo kadhaa mazuri ya kutembelea mkoani Mbeya, jumlisha na mkoa wa Songwe
  1. Kawetire view point - Njia ya kwenda Chunya. Pale utaona bonde la ufa kwa ukubwa wake, yaani ile trough (beseni) la bonde la ufa, ni sehemu nzuri sana. Iko njia kuu ya kwenda Singida na Tabora eneo la Kawetire
  2. Daraja la Mungu, likpo Rungwe Mbeya. Ni mwamba mgumu (jiwe) ambao umevuka mto na pana mandhari nzuri sana ya kuvutia. Jirani na hapo pana kijungu (maji ya mto yanapotelea ardhini)
  3. Tembelea Matema, fukwe za ziwa Nyasa. Kuna fukwe nzuri sana na utapata nafasi ya kuogelea ziwani, maji baridi burudani kabisa na utapata nafasi ya kula samaki wa ziwa Nyasa
  4. Eneo la Songwe (Majimoto) kuna majimoto (geysers) yanayotoka ardhini. Maji ni ya moto kiasi unaweka yai linaiva na unakula. Kijiji kipo kilometa 8 kutoka uwanja wa Ndege wa Songwe, kama unaelekea Tunduma
  5. Ukipata nafasi temebelea kimondo cha Mbozi, eneo la Ndolezi, nao ni utalii tosha.
  6. Mwisho, tembele mbuga ya maua ya Kitulo, ni mwendo wa saa 2 kutoka Mbeya mjini, uelekeo wa Makete Njombe kupitia Igoma.
 
Back
Top Bottom