DK Mweluvu
Member
- Mar 3, 2020
- 86
- 127
Nachoamini watu waliomaliza miaka hyo kwasasa wako vizuri kiuchumi
Nasema uongo?
Nasema uongo?
Hii iligharimu wengiKijijini ukishinda jina lako linauzwa kwa wenye fedha we unaingia shamba
Zilikuwa nyakati ngumu sana mkuu. Mkoa wa Arusha pia ulikuwa na shule zinahesabika. Kulikuwa na Arusha day, Arusha sec, Ilboru, Kimandolu, Makuyuni, Karatu, Irkisongo, na nyingine chache.Nimemaliza STD Seven mwaka 1997 kwenye shule mojawapo wilaya ya Kinondoni. Siku matokeo yametoka tumekwenda wilayani na marafiki zangu tumekuta watu wameshajaa kwenye ubao wa matangazo hata nafasi hakuna.
Kuna dogo mmoja namfahamu alitangulia ile kuniona tu akaniambia "Mwamba umepasua Azaboy umekwenda" akimaanisha Azania Sekondari. Aisee sikuamini nilipambana kwenye ule umati hadi nikaona jina langu, nilifurahi sana.
Kuna mwenzetu mmoja tulikuwa nae ametafuta jina halioni na alikuwa kipanga darasani, alitafuta jina lake hadi alikata tamaa. Kumbe kachaguliwa Mzumbe vipaji pekee kiakili, kuja kuona jina alishangilia kama Mwehu.
Kipinid kila Dar es salaam ilikuwa na shule za sekondari za serikali chache sana.
1. Azania- wavulana tupu
2. Jangwani- wasichana tupu
3. Kisutu- wasichana tupu
4. Zanaki- wasichana tupu
5. Forodhani- Mchanganyiko
6. Kibasira- Mchanganyiko
7. Kambangwa- Mchanganyiko.
8. Pugu
NB! Tambaza ilikuwa ni A-level tu (kuanzia mwaka 1994)
Pata picha Dar nzima wanafunzi wanagombania nafasi kwenye hizo shule ushindani wake ulikuwaje.
Asilimia kubwa tulitegemea Tuition ili kufaulu bila hivyo ni ngumu kutoboa.
Tuition maarufu za wanafunzi wa shule ya msingi wilaya ya kinondoni kipindi kile zilikuwa;
1. MT Zungu- Sinza,
2. Dani - Mburahati,
3. Boniface Ibunga- Mabibo.
😄😄😄 Jomba taratibu aisee. Ingawa wapo ambao kwa sasa ni matajiri ila Wengi wetu hatutaki kukumbuka umri wetu kabisa maana ni stress. Hakuna mtu aliyemaliza shule 2000 kurudi nyuma mwenye umri wa chini ya miaka 36.Nachoamini watu waliomaliza miaka hyo kwasasa wako vizuri kiuchumi
Nasema uongo?
tena wa kundeBora umeacha kuandika kwasababu ungeandika ushuzi.
Ndio sasa nasema wengi wao wamejipata ata kama sio matajiri ila hawategemei wazaziJomba taratibu aisee. Ingawa wapo ambao kwa sasa ni matajiri ila Wengi wetu hatutaki kukumbuka umri wetu kabisa maana ni stress. Hakuna mtu aliyemaliza shule 2000 kurudi nyuma mwenye umri wa chini ya miaka 36.
We acha tu mkuu tumesoma katika mazingira magumu sana ili kufaulu maana mzazi anakuambia kabisa ukifeli hela ya kukupeleka private sina nakupeleka gereji.Miaka hiyo mlikuwa mnasoma kwa stress tupu. Ila Mimi naona Ni Bora kwa sababu serikali ilichagua watu wachache tu walioweza kuwaajiri. Sikuhizi serikali inasema umefaulu alafu haina pa kukuajiri. Muda unaokuwa umepotezewa Ni almost miaka 15 plus
Hivi ile barabara inayopitia shighatini unatokea ngujini alafu mombasa store bado ipo ile njia imepita sehemu ambayo huwezi tegemeaNilimaliza 1998 matokeo tulikua yakitoka tunaenda Bomani Mwanga na ni Alhamisi siku ya soko.Na hapo tumetokea Usangi kwa miguu tunapitia Shighatini,Male huko mnashuka kwa ngondi.
Tukafika pale tukakuta watu kibao wanaangalia yale matoke na sisi ni wadogo inabidi upambane uangalie majina yamebanfikwa kwenye notice board.
Bahati nikaliona Jina Langu. Bi mkubwa akanipa ofa ya wali maharage hotelini na nikaanza kununuliwa vifaa sokoni.
Form Four mwaka 2002 enzi hizo matokeo yanatoka kwenye magazeti.Ina maana kila siku gazeti linatoa shule na inabidi ununue kila siku mpaka uone shule yako.
Nililipata gazeti la Nipashe nikaona nimefaulu na sasa ikawa kusubiria selection.Nazo zinatoka kwenye gazeti kila siku mpaka uone umepata post ama la.
Mimi pia nimemaliza mwaka huo...Mm nimemaliza mwaka 1997
Mambo yalikuwa ya kijima kabisa Ila watoto wa enzi Hizo na Sasa ni tofauti kabisa interms of IQ
Nakumbuka Moshi kipindi kileee ndio tabia hyo ilishamiri sn aisee, wengi waliumizwa kwa style hiiKijijini ukishinda jina lako linauzwa kwa wenye fedha we unaingia shamba
HahahaKwa Dar nadhani Azania ilikuwa maarufu zaidi.