Hamna haja ya kusema nafasi ya mwanafunzi darasani kama darasa lina wanafunzi chini ya 50 darasani

Ultimate

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
713
1,738
Leo siku ya tatu rafiki yangu ananisumbua kutimiza ahadi niliyompa mtoto wake

Ipo hivi mapema mwaka huu, nilikutana na huyo mtoto sasa kwenye story za hapa na pale, akaniambia mwaka huu anaingia darasa la nne.

Kiroho safi nikamwambia akiwa kwenye top 10 aniambie kuna zawadi yake. Sasa juzi hapa nimetumiwa matokea yake ya mitihani. Kijana amekua wa 4 kati ya wananfunzi 28

Kitu amacho nimegoma kufanya ni kitimiza hii ahadi maoni yangu ni kwamba

1. Darasa halina ushindani, kama darasa lina wanafunzi ni 28 ni rahisi kufanya vizuri.

2. Shule nyingi hasa hizi private watoto wanafaulu sana hadi inatia wasiwasi

3. Kama ni kutoa zawadi nitatoa kama ataweza kufanya test za kwenye vitabu na kupata angalau 70%+ (baba ake amekataa)
 
Bamdogo na ma uncle janja janja wapo wengi sana. Wewe uliahidi zawadi toa zawadi acha siasa sijui mambo ya ushindani, mara private school na blah blah nyingine.

Toa zawadi babuu
 
Kuna formula ya kupima matokeo na maendeleo ya mtoto isotumia nafasi.

Maana mfano kusema mtoto alikuwa wa 12 sasa hivi ni wa 7 basi amepanda inaweza kupotosha. Je kama darasa zima wameongezeka kufaulu? Na je kama wamefeli zaidi ila yeye akafeli kidogo utajuaje!???.

Yaani inatakiwa iwe ni yeye VS juhudi zake tu. Wastani wake uliopita VS wastani wake wa baadaye.

Na kama unafuatilia somo mojamoja basi alama ndio ziamue kuwa amepanda au ameshuka. Mfano mzazi anataka kupima effectiveness ya tuisheni mpya ya hisabati aliyompeleka.
Screenshot_20231218-135358_Chrome.jpg


Badala ya parasitemia weka ufaulu wake wa kwanza Po na wa Mwisho Pt.

Anyway kama una maswali zaidi, niwhatsapp kwa 0734189022
 
Acha janja janja timiza ahadi, hata kama darasani wangekuwa 11 na amekuwa wa 10 lazima utoe zawadi kama ulivyoahidi
 
Shida ulipotoa zawadi masharti hayo hayakuwepo, ungeuliza wapo wangapi darasani kabla hujatoa ahadi, kwa sasa huna namna, toa tu zawad
 
Back
Top Bottom