Wale tuliomaliza darasa la 7 mwaka 2000 kurudi nyuma tujikumbushe ilivyokua siku matokeo ya la 7 yanatangazwa

Nimemaliza STD Seven mwaka 1997 kwenye shule mojawapo wilaya ya Kinondoni. Siku matokeo yametoka tumekwenda wilayani na marafiki zangu tumekuta watu wameshajaa kwenye ubao wa matangazo hata nafasi hakuna.
Kuna dogo mmoja namfahamu alitangulia ile kuniona tu akaniambia "Mwamba umepasua Azaboy umekwenda" akimaanisha Azania Sekondari. Aisee sikuamini nilipambana kwenye ule umati hadi nikaona jina langu, nilifurahi sana.
Kuna mwenzetu mmoja tulikuwa nae ametafuta jina halioni na alikuwa kipanga darasani, alitafuta jina lake hadi alikata tamaa. Kumbe kachaguliwa Mzumbe vipaji pekee kiakili, kuja kuona jina alishangilia kama Mwehu.
Kipinid kila Dar es salaam ilikuwa na shule za sekondari za serikali chache sana.
1. Azania- wavulana tupu
2. Jangwani- wasichana tupu
3. Kisutu- wasichana tupu
4. Zanaki- wasichana tupu
5. Forodhani- Mchanganyiko
6. Kibasira- Mchanganyiko
7. Kambangwa- Mchanganyiko.
8. Pugu
NB! Tambaza ilikuwa ni A-level tu (kuanzia mwaka 1994)
Pata picha Dar nzima wanafunzi wanagombania nafasi kwenye hizo shule ushindani wake ulikuwaje.
Asilimia kubwa tulitegemea Tuition ili kufaulu bila hivyo ni ngumu kutoboa.
Tuition maarufu za wanafunzi wa shule ya msingi wilaya ya kinondoni kipindi kile zilikuwa;
1. MT Zungu- Sinza,
2. Dani - Mburahati,
3. Boniface Ibunga- Mabibo.
 
Zilikuwa nyakati ngumu sana mkuu. Mkoa wa Arusha pia ulikuwa na shule zinahesabika. Kulikuwa na Arusha day, Arusha sec, Ilboru, Kimandolu, Makuyuni, Karatu, Irkisongo, na nyingine chache.
 
Nachoamini watu waliomaliza miaka hyo kwasasa wako vizuri kiuchumi

Nasema uongo?
😄😄😄 Jomba taratibu aisee. Ingawa wapo ambao kwa sasa ni matajiri ila Wengi wetu hatutaki kukumbuka umri wetu kabisa maana ni stress. Hakuna mtu aliyemaliza shule 2000 kurudi nyuma mwenye umri wa chini ya miaka 36.
 
1998 dah asubuhi naamka taarifa matokeo yametoka baada ya chai mbio magomeni wilayani watu kama wote tafuta tafuta na Wewe hadi saa 7 hola mtu nyomi. Tetesi gazeti la Dar Leo na Alasiri wametoa majina ya waliochaguliwa. dah mbio kkoo shule ya uhuru kulisaka gazeti. Pekua hola. Nikarudi home kinyongeee sana. Wamefaulu watu 16 mimi siko na nakuwaga top 10. Hata chakula sikula siku hiyo.
Kumbe bana Mungu ana mipango yake bana. Nikaja kusoma shule iliyobadilisha mengi sana maishani mwangu na watu niliokutana nao. The rest is history.
Wale walioenda Azania Forodhani Kibasila sijui Kambangwa Jangwani Kisutu waliotoboa hadi huku juu hata watatu hawafiki.
 
Jomba taratibu aisee. Ingawa wapo ambao kwa sasa ni matajiri ila Wengi wetu hatutaki kukumbuka umri wetu kabisa maana ni stress. Hakuna mtu aliyemaliza shule 2000 kurudi nyuma mwenye umri wa chini ya miaka 36.
Ndio sasa nasema wengi wao wamejipata ata kama sio matajiri ila hawategemei wazazi
 
Miaka hiyo mlikuwa mnasoma kwa stress tupu. Ila Mimi naona Ni Bora kwa sababu serikali ilichagua watu wachache tu walioweza kuwaajiri. Sikuhizi serikali inasema umefaulu alafu haina pa kukuajiri. Muda unaokuwa umepotezewa Ni almost miaka 15 plus
 
Heri yenu mliooma mijijini. Sisi tuliosoma bush ilikuwa kawaida shule kutoa sifur bin sifur. Mwaka wangu tulifauku 5 tu na mmoja hakuenda. Nashukuru kati ya wanne tulioenda wenzangu watatu ni maticha. Moja Secondari, wawili Msingi. Mimi napambana na maisha yangu katika tasnia nyingine.
 
Miaka hiyo mlikuwa mnasoma kwa stress tupu. Ila Mimi naona Ni Bora kwa sababu serikali ilichagua watu wachache tu walioweza kuwaajiri. Sikuhizi serikali inasema umefaulu alafu haina pa kukuajiri. Muda unaokuwa umepotezewa Ni almost miaka 15 plus
We acha tu mkuu tumesoma katika mazingira magumu sana ili kufaulu maana mzazi anakuambia kabisa ukifeli hela ya kukupeleka private sina nakupeleka gereji.
Na pia kipindi kama haujafulu kwenda shule ya serikali unaonekana hauna akili hivyo kila mtu alipambana atoboe. Ni bora ufaulu halafu mzazi aamue tu akupeleke private school lakini usifeli.
Tumelala sana kwenye majumba ya watu kwenye group discussion, full mbu na kunguni ili kutafuta heshima ya kwenda Azania sekondari.(ndio ilikuwa shule pendwa kwa wavulana mkoani Dar enzi hizo)
Ukifaulu mtaa mzima wanakujua full heshima....
 
Nilimaliza 1998 matokeo tulikua yakitoka tunaenda Bomani Mwanga na ni Alhamisi siku ya soko.Na hapo tumetokea Usangi kwa miguu tunapitia Shighatini,Male huko mnashuka kwa ngondi.
Tukafika pale tukakuta watu kibao wanaangalia yale matoke na sisi ni wadogo inabidi upambane uangalie majina yamebanfikwa kwenye notice board.
Bahati nikaliona Jina Langu. Bi mkubwa akanipa ofa ya wali maharage hotelini na nikaanza kununuliwa vifaa sokoni.
Form Four mwaka 2002 enzi hizo matokeo yanatoka kwenye magazeti.Ina maana kila siku gazeti linatoa shule na inabidi ununue kila siku mpaka uone shule yako.
Nililipata gazeti la Nipashe nikaona nimefaulu na sasa ikawa kusubiria selection.Nazo zinatoka kwenye gazeti kila siku mpaka uone umepata post ama la.
Hivi ile barabara inayopitia shighatini unatokea ngujini alafu mombasa store bado ipo ile njia imepita sehemu ambayo huwezi tegemea
 
Back
Top Bottom