Ninachojua ni kuwa Chama anampira wa taratibu sana na hana mbio ila ana akili na utulivu mkubwa sana wa mpira na muda wowote anakupa matokeo yeye binafsi au anasababisha timu ipate matokeo na ameshafanya hivyo mara kadhaa wala hili halina ubishi. Mafundi wa mpira kama Zidane, Pilo,Ronaldo Delima, Ronaldinho, Xavi wala hawakuwa na mbio kama za Mpape.
Mchezaji kama Kibu au Sakho ni wachezaji wenye kasi sana na papara muda mwingi hawana utulivu hivyo kutokuwa na impact kubwa uwanjani mda mwingi ni kukumbia kumbia na mpira bila sababu.
Binafsi mimi nimeshuhudia mechi nyingi za Simba kama Chama hayupo tumekuwa tukipata ushindi kwa tabu sana na mpira tunaocheza huwa ni wabutua butua. Kifupi Simba mbadala wa Chama kwa sasa hayupo, hata kama kuna siku atacheza chini ya kiwango mashabiki sio wajinga wampende mchezaji bila sababu kwani kawapa rushwa?