Wakuu wa Nchi za SADC kukutana kwa dharura nchini Angola tarehe 04 Novemba, 2023

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanatarajia kukutana katika mkutano wa dharura Jijini Luanda, Angola tarehe 04 Novemba, 2023.

Mkutano huo unalenga kujadili juhudi za SADC katika kuimarisha hali ya amani, ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kufuatia mapigano ya muda mrefu yanayoendelea nchini humo yakitekelezwa na vikundi vyenye silaha katika majimbo ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri.

Katika Mkutano huo ujumbe wa Tanzania unatarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ataambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) pamoja na Maafisa Waandamizi wa Serikali.

Pamoja na masuala mengine, mkutano huo unatarajiwa kusisitiza umuhimu wa utashi wa kisiasa kwa Nchi Wanachama katika kuchangia askari na vifaa vya kijeshi kwa ajili ya Misheni ya Ulinzi wa Amani ya SADC nchini DRC (SAMIDRC), ambapo hadi sasa nchi tatu pekee ndizo zimechangia askari na vifaa vya kijeshi katika misheni hiyo. Nchi hizo ni Tanzania, Afrika Kusini na Malawi.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama na Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu na Mawaziri vitakavyofanyika tarehe 3 Novemba 2023.
Screenshot 2023-11-03 at 12.52.56.png
 
Tunamupiga tu mupaka bukimbie Bana Lunda Bana Congo bana Zairee.....banayomba busisi batubezi kupiga musasi yeye Mubuambiye hii MuCongo sio ileee
 
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanatarajia kukutana katika mkutano wa dharura Jijini Luanda, Angola tarehe 04 Novemba, 2023.

Mkutano huo unalenga kujadili juhudi za SADC katika kuimarisha hali ya amani, ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kufuatia mapigano ya muda mrefu yanayoendelea nchini humo yakitekelezwa na vikundi vyenye silaha katika majimbo ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri.

Katika Mkutano huo ujumbe wa Tanzania unatarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ataambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) pamoja na Maafisa Waandamizi wa Serikali.

Pamoja na masuala mengine, mkutano huo unatarajiwa kusisitiza umuhimu wa utashi wa kisiasa kwa Nchi Wanachama katika kuchangia askari na vifaa vya kijeshi kwa ajili ya Misheni ya Ulinzi wa Amani ya SADC nchini DRC (SAMIDRC), ambapo hadi sasa nchi tatu pekee ndizo zimechangia askari na vifaa vya kijeshi katika misheni hiyo. Nchi hizo ni Tanzania, Afrika Kusini na Malawi.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama na Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu na Mawaziri vitakavyofanyika tarehe 3 Novemba 2023.
View attachment 2802360
Kaz kaz... kazi iendelee, Mama anachapa sana kazi, anapiga mzigo wa kufa mtu, kwa kweli kazi iendelee ila pia charty begins at home, namuomba tuu Mama asiwe too busy kushughulikia ya wengine, ikafika 2025 hili kubwa la kwetu ambalo bado, akashindwa kulikamilisha!. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

P
 
Back
Top Bottom