Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC Ngazi ya Wataalamu waanza Nchini Angola

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Tanzania inashiriki Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa Agosti 08, 2023 Jijini Luanda, Angola kwa ngazi ya Maafisa Waandamizi.

Wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, imeshuhudiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ikikabidhi uenyekiti wa ngazi hiyo kwa Angola ambayo itashikilia wadhifa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Agosti 2024.
22ac8e4f-9e0b-4b92-976f-8e4ac3cc5bda.jpg

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaban (mwenye mtandio) akiwa na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ulioanza Agosti 8, 2023 katika ngazi ya maafisa waandamizi Jijini Luanda, Angola.

Tanzania ambayo ni moja ya nchi waasisi wa SADC inashiriki kikamilifu Mkutano huo na kwa ngazi ya maafisa waandamizi, ujumbe wake unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaban.

Wakati wa makabidhiano ya uenyekiti, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Balozi Songhu Kayumba alisema kwa mwaka mmoja wa uenyekiti wa DRC, Nchi wanachama ziliunganisha nguvu kuhakikiasha kuwa wanafikia malengo waliyojiwekea kupitia kaulimbiu “Kuhamasisha Uwekezaji katika viwanda kupitia usindikaji wa mazao ya kilimo, madini, kuendeleza mnyororo wa thamani wa kikanda kwa nia ya kufikia uakuaji wa uchumi jumuishi na endelevu” (Promoting Industrialization through Agro-Processing, beneficiation of minerals and the development of regional value chains with a view to achieving inclusive and sustainable economic growth).
10c7377c-f09f-4bc5-bf6b-a6eb97975024.jpg

Mwenyekiti wa ngazi ya maafisa waandamizi aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Balozi Songhu Kayumba (kulia) akikabidhi uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya wa maafisa waandamizi kutoka Angola, Balozi Nazare Salvador ambaye ni Mkurugenzi wa Ofisi ya SADC Nchini Angola katika Wizara ya Uhusiano wa Nje ya nchi hiyo.

Balozi Kayumba alisema kupitia kaulimbiu hiyo, mengi yamefikiwa na cha muhimu zaidi eneo la SADC limeendelea kuwa salama na tulivu. “Hatujashuhudia kuibuka kwa migogoro mipya, migoro mikubwa ya matumizi ya silaha au matendo ya ugaidi katika nchi wanachama tofauti na ile ambayo imekuwepo tokea zamani” Balozi Kayumba alisema.

Mkutano huo utakaofanyika takribani kwa siku 10 umegawayika katika makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Kamati ya Fedha tarehe 10 Agosti 2023; Mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 13 na 14 Agosti 2023; Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ushirikiano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 16 Agosti 2023 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC tarehe 17 Agosti 2023.

Masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta ustawi wa jamii, kuimarisha uchumi na usalama katika Kanda ya SADC yatajadiliwa katika ngazi tofauti za Mkutano huo. Masuala hayo ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya pamoja ambayo imeainishwa katika Mpango Elekezi wa Maendeleo ya Kikanda; utekelezaji wa Bajeti na hali ya michango ya nchi wanachama na Maendeleo ya Viwanda na Mtangamano wa Masoko.
 
Tanzania inashiriki Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa Agosti 08, 2023 Jijini Luanda, Angola kwa ngazi ya Maafisa Waandamizi.

Wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, imeshuhudiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ikikabidhi uenyekiti wa ngazi hiyo kwa Angola ambayo itashikilia wadhifa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Agosti 2024.
View attachment 2712350
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaban (mwenye mtandio) akiwa na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ulioanza Agosti 8, 2023 katika ngazi ya maafisa waandamizi Jijini Luanda, Angola.

Tanzania ambayo ni moja ya nchi waasisi wa SADC inashiriki kikamilifu Mkutano huo na kwa ngazi ya maafisa waandamizi, ujumbe wake unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaban.

Wakati wa makabidhiano ya uenyekiti, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Balozi Songhu Kayumba alisema kwa mwaka mmoja wa uenyekiti wa DRC, Nchi wanachama ziliunganisha nguvu kuhakikiasha kuwa wanafikia malengo waliyojiwekea kupitia kaulimbiu “Kuhamasisha Uwekezaji katika viwanda kupitia usindikaji wa mazao ya kilimo, madini, kuendeleza mnyororo wa thamani wa kikanda kwa nia ya kufikia uakuaji wa uchumi jumuishi na endelevu” (Promoting Industrialization through Agro-Processing, beneficiation of minerals and the development of regional value chains with a view to achieving inclusive and sustainable economic growth).
View attachment 2712351
Mwenyekiti wa ngazi ya maafisa waandamizi aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Balozi Songhu Kayumba (kulia) akikabidhi uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya wa maafisa waandamizi kutoka Angola, Balozi Nazare Salvador ambaye ni Mkurugenzi wa Ofisi ya SADC Nchini Angola katika Wizara ya Uhusiano wa Nje ya nchi hiyo.

Balozi Kayumba alisema kupitia kaulimbiu hiyo, mengi yamefikiwa na cha muhimu zaidi eneo la SADC limeendelea kuwa salama na tulivu. “Hatujashuhudia kuibuka kwa migogoro mipya, migoro mikubwa ya matumizi ya silaha au matendo ya ugaidi katika nchi wanachama tofauti na ile ambayo imekuwepo tokea zamani” Balozi Kayumba alisema.

Mkutano huo utakaofanyika takribani kwa siku 10 umegawayika katika makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Kamati ya Fedha tarehe 10 Agosti 2023; Mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 13 na 14 Agosti 2023; Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ushirikiano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 16 Agosti 2023 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC tarehe 17 Agosti 2023.

Masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta ustawi wa jamii, kuimarisha uchumi na usalama katika Kanda ya SADC yatajadiliwa katika ngazi tofauti za Mkutano huo. Masuala hayo ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya pamoja ambayo imeainishwa katika Mpango Elekezi wa Maendeleo ya Kikanda; utekelezaji wa Bajeti na hali ya michango ya nchi wanachama na Maendeleo ya Viwanda na Mtangamano wa Masoko.
Hayawezi kufanikisha lolote duniani kwa watu wao haya madikiteita. sana sana yanaangalia how to consolidte power
 
Back
Top Bottom