Wakuu nimeitwa TRA. Usalama upo kweli?

Wakuu nimeitwa TRA. Usalama upo kweli?

Usiwe na wasiwasi, ila ilipaswa wauliza Kwa Nini wanakuita eneo ambao sio lako la Kodi, ila hakuna shida, kabla hujaenda huko pita kwanza eneo lako la Kodi uwaulize kuhusu huo wito, only and only then ndo uamue kwenda huko.

Kama ni TRA kweli, then wala usiwe na wasiwasi, ila shida ni kama ni chambo na umeshawapa mademu walko wa Jamii forums number ambao ni madume jike kama wale walioingia mahakamani Jana!
Asante sana mkuu
 
Ahaa Asante sana mkuu, so nikienda what will happen? Ntatakiwa kulipa hapo hapo au nitapewa muda wa kulipa?
Hulazimiki kulipa hapo hapo. Unaweza hata kukataa mahesabu yao ukawaambia hali halisi maanake kama hujalipa siku nyingi watakupugia hesabu na mapenati yao ya kipuuzi.
 
Nimepigiwa simu TRA wananiita. Namba ya simu ni ya kawaida. Je uzima upo? Sehemu niliyo itwa ni tofauti na kituo changu cha Kodi..

Usalama upo kweli?

N. B : Mimi sio mfanyabiashara mkubwa wala wa Kati.
Nenda hata kama ni IKULU hakuna kumwogopa mtu hata kama una makosa, hii nchi sisi ndio mabosi, hao waliopo huko ofisini ni watumishi wetu.
 
Nimepigiwa simu TRA wananiita. Namba ya simu ni ya kawaida. Je uzima upo? Sehemu niliyo itwa ni tofauti na kituo changu cha Kodi..

Usalama upo kweli?

N. B : Mimi sio mfanyabiashara mkubwa wala wa Kati.
Mimi hua nawashangaa watu unapigiwa tu simu unakurupuka kwendaukiona hivo jua unatatizo ama la akili au kazi zako ni chafu.Huwezi kuwa makini ukawa na wasiswasi. Sasa kwa nini hukuwauliza mawali hayo huko huko?
Navyofahamu tra mpaka wakute utakuta kwanza walishafanya makadirio hujalipa au ulikuwa na adhabu na walikuandikia hukulipa au hukwenda .Ndiyo maana watu kama wewe matapeli wanawapenda mno yaani myu anapiga simu tenanunaema na namba huijui unakubali tu kichwa kichwa je ulimuuliza jina ni nani na ofisi ipi ya tra? na unasema siju ni ofisi tofauti na unayolipia kodi uoni kabisa unatapeliwa na watu wanaojifanya tra? mimi mtu hata awe wa bank akipiga namwambia naenda bank ambay ndiyo tawi langu .
 
Back
Top Bottom