Wakristo wenzangu, kwahiyo pamoja na kuwa na elimu zetu Bado tunaamini Nabii Yona alimezwa na nyangumi na akatapikwa akiwa Yu hai?

Wakristo wenzangu, kwahiyo pamoja na kuwa na elimu zetu Bado tunaamini Nabii Yona alimezwa na nyangumi na akatapikwa akiwa Yu hai?

Jesus Christ 🤣

Unaweza kumuacha mtu apotee hivi hivi wakati anahitaji kumpokea bwana.

I'm serious, need your help
Upoteeje? Unapinga kitu unachokijua unataka nirudie kukueleza yaleyale unayoyajua ili usipotee?

You cannever be serious!👌🏽
Excuse me 💅
 
Upoteeje? Unapinga kitu unachokijua unataka nirudie kukueleza yaleyale unayoyajua ili usipotee?

You cannever be serious!👌🏽
Excuse me 💅
Sijawahi kujua that's why I'm seeking your help maybe kama hautaki kunipa muongozo kuhusu bwana na unataka nipotee
 
Unajua bado kuna kitu huelewi mkuu.

Katika imani hakuna hoja isiyo na majibu, hoja zote zina majibu. Tatizo linaanza ukitaka majibu yawe na logic ilihali majibu ni ya kiimani.

Mfano wa hoja yako ya Misri, ukaambiwa MUNGU aliamua watange tange misri tayari umefikia ukomo wa kiimani wa kuhoji maana katika imani MUNGU habishiwi.

Na swali lolote litakalofata nje ya hapo ni kubishana na maamuzi ya MUNGU au kuwekea mashaka ya matendo yake na nadhani unaelewa maana yake ni nini kwa waamini.
Kaka nimesoma Bible Knowledge na naelewa walivyokuwa wakitangatanga, nimesoma vizuri bible knowledge 1 and Bible knowledge kuanzia form III hadi IV na nilifaulu vizuri sana. Mimi ni muumini mzuri sana, na ninayo imani imara isiyoyumbishwa. Sibishani na Mungu, hilo halipo hata kidogo, nilichoongea hapo ni kutengeneza logic na pia kuleta mawazo tofauti ili watu tujadili kujenga uwanda mpana wa fikra. Vitabu viliandikwa na binadamu, unawajua vizuri waandishi hao walikuwa akina nani.....Lakini pia binadamu tunayo mapungufu yetu, na siyo lazima wakati tukifanya vitu au tukiandika tunakuwa tumejazwa roho mtakatifu. TAFAKARI
 
Kumbuka définition ya Muujiza ni hii: an extraordinary and welcome event that is not explicable by natural or scientific laws and is therefore attributed to a divine agency.
Source: Wikipedia

Biblia yenyewe inasisitiza kuwa samaki huyo alikuwa "aliyetayarishwa na BWANA" (Yona 1:17), yaani, Mungu alimuumba au kumtuma kwa lengo maalum. Hivyo, haikuwa tukio la kawaida,

Ukilazimisha kutumia knowledge ya science kwenye kila kitu utachosha akili yako kuliko unavyostahili.
 
Apa haujasema kweli sehemu ya biblia hasa agano jipya zimekinzana kutokan na waandishi kuwa tofauti na mitazamo yao pia tofauti.

Hamna anayepinga neno la Mungu, sisi tunahoji shuhuda za hao waandishi walioshuhudia ayo na kuyaandika.

Na ndo maana vitabu vya
Deuterokanoni vilipunguzwa kwenye biblia ya baadhi ya dhehebu kama sio part ya biblia kwa maana watu walihoji uhalali wake, ivyo kama wayahudi waliweza kuhoji uhalali wake na pia sisi tunapaswa kuhoji pia.

Na kwenye kukinzan kwa waandishi wa biblia mfano kifo cha Yuda Mathayo 27:5 inasema Yuda alijinyonga na ukisoma matendo 1:8 yuda alianguka akapasuka tumbo na kufariki. Kwaivo apo tunaona maneno ya biblia Mungu aliwapa tu watu ujumbe wake ila kila binadamu aliandika kwa style yake anavojua na kuelewa maana roho wa mtakatifu aliwaongoza tu watu ila hakuondoa utu wao, akili zao wala mitazamo yao sasa kwanini sisi wasomaji na waamini tusitumie mitazamo ama utu wetu kusoma na kuhoji?.
vitabu ivyi vya kwenye biblia ni matokeo ya jamii ya mwanzo za kikristo na sio dictation ya kutoka moja kwa moja kwa Mungu na ndo maan Yesu hakuandika kitabu chchte bali wafuasi wake waliandika baadae sana miaka kama 30+ mpk 70+, na kila mwandishi alikuwa ana ajenda zake na malengo yake na ndo maana wanasisitiza mambo tofauti na wakati mwingne wanakinzana.
kwaivo kama ungekuwa ni Muongozo wa Mungu moja kwa moja basi Biblia isingekuwa na makosa aina yyte maana Mungu hakosei, ila kama ni ya mwanadamu hamna mwanadamu asiyekosea ivo ni halali kuhoji na kutumia logic kwenye kusoma tafsiri zao.
Basi naomba utumie imani yako ama logic kunielezea apa Nani aliyemchochea Daudi kufanya sensa juu ya Israel.


2 Samweli 24:1
“Hasira ya Bwana ikawaka tena juu ya Israeli, akamchochea Daudi juu yao, akisema, Nenda ukawahesabu Israeli na Yuda.”

Mambo ya Nyakati 21:1
"Shetani akasimama juu ya Israeli, akamchochea Daudi awahesabu Israeli.”

Kuliingana na maandiko aya Je Shetani ndio Mungu na Mungu ndo shetani ama Roho mtakatifu anasemaje apa tusijiulze tuamini tu chchte kinawezekana?.

Pia neno gani hasa la mwisho Yesu alisema msalabani?

Mathayo 27:46
“Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Luka 23:46
“Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.”

Yohana 19:30
"Imekwisha"

Kitabu cha 1 Wathesalonike 5:21 linatuhasa tukiskibali kila kitu bali tuchunguze kwanza.
“Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.”

Matendo ya mitume 17:11 inatuhasa pia kutumia akili zetu sio imani tu.
“… walilipokea neno kwa utayari, wakayachunguza maandiko kila siku waone kama ndivyo yalivyo.”

Ata Tomaso alimwambia Yesu yeye asipoona hatoamini na wala Yesu hakumpinga waka kuwambia Mungu kakataza.
Yohana 20:25.
Sasa mkuu, twende kama unavyotaka, tuanze kuhoji kwa kutumia Logic ili mwishoni tuone kama msingi wa Logic si kubatilisha imani.

Tuanze na swali jepesi, wewe tumia Logic kujibu kisha tuone mwelekeo wake kiimani.

Uhalali wa Israel kupewa nafasi ya upekee katika maandiko ya biblia ni upi?
 
Kaka nimesoma Bible Knowledge na naelewa walivyokuwa wakitangatanga, nimesoma vizuri bible knowledge 1 and Bible knowledge kuanzia form III hadi IV na nilifaulu vizuri sana. Mimi ni muumini mzuri sana, na ninayo imani imara isiyoyumbishwa. Sibishani na Mungu, hilo halipo hata kidogo, nilichoongea hapo ni kutengeneza logic na pia kuleta mawazo tofauti ili watu tujadili kujenga uwanda mpana wa fikra. Vitabu viliandikwa na binadamu, unawajua vizuri waandishi hao walikuwa akina nani.....Lakini pia binadamu tunayo mapungufu yetu, na siyo lazima wakati tukifanya vitu au tukiandika tunakuwa tumejazwa roho mtakatifu. TAFAKARI
Mkuu, unachosema hapa ni kuna vitabu vya biblia vimetokana na mawazo ya mwanadamu na si MUNGU. Si ndio?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom