menny terry
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 509
- 667
Wakuu hii system ni ya muda sana hapa Tanzania. Anatajwa kijana ambae ameongoza Tanzania nzima kidato cha nne au kidato cha sita wanapelekwa bungeni na zawadi kibao wanapewa lakini hadi leo hii hawa vipanga wa mitihani hawajulikani walipo.
Je, kuna unayemjua na unajua anajishughulisha na nini?
Je, kuna unayemjua na unajua anajishughulisha na nini?
Hali wakuu?
Baada ya matokeo ya form IV kumekuwa na mihemko na tafsiri mbalimbali kuhusu shule za serikali na binafsi. Mimi leo najiuliza pia nawauliza wenzangu.
1. Maendeleo ya watoto ambao huwa best katika hatua zinazoendelea kwa mfano high school na vyuo? Je bado wanakuwa best huko? kazini nk?
2. Ubunifu wa hawa vichwa vyetu. Je matokeo haya yanatafsiri uwezo wao wa ubunifu katika maisha?
3. Value for money; kama wazazi na wandugu wa hawa vijana mbali ya lugha kuna kitu cha kujivunia kuhusu watoto wetu? Nami namsomesha wangu private but hata kama anafanya vizuri nahisi kama natumia pesa nyingi zaidi ya kile anachopewa...
Mpo huru kuongeza maswali....
Nawasilisha
==============
Wakuu nimefurahia angalau tumeweza kuwakumbuka wachache, but nahisi tumejaribu kujadili swala moja na kiasi la pili.
Katika hilo naona tumewajadili wa kwanza tu na sio angalau scope ya top ten or 20 na kadhalika. Nia ya huu mjadala ni kujaribu kuzinduka na kufuatilia records za hawa watu wetu. Huenda tukichimba kwa mbali utakuta wahadhili wengi wa vyuo vyetu wala hawakuwa top 100.
Pia tukichimba sana tunaweza kujua kama hizi shule bora zinatoa elimu bora au zinafundisha mbinu za kufaulu mitikani.
La mwisho... Tujiulize nini dhamira ya elimu? Kufaulu au kuelimika? And hapo huenda kuna mafunzo mengine mtambuka....