Wako wapi wanafunzi bora (Tanzania One) wa miaka ya nyuma?

Wako wapi wanafunzi bora (Tanzania One) wa miaka ya nyuma?

hata mazingira yakiwa sawa lazima awepo wa kwanza na wa mwisho.taifa libadilike vipi?!

em nipe jinsia yako,maana naweza nikawa na-argue na mtu mwenye jinsia mbili bila kujijua,au naweza nikawa naongea na mtu mwenye dafu badala ya kichwa km jk,nimesha sema NECTA z unfair waweke utaratibu mwingine sio huu wa kipuuzi wa kufanya watoto wakalili mwasali yani kucopy na kupaste ila concept ya vitu hawana.Kwa mfumo huu utamwita mtu TO?
 
Hali wakuu?

Baada ya matokeo ya form iv kumekuwa na mihemko na tafsiri mbalimbali kuhusu shule za serikali na binafsi. mimi leo najiuliza pia nawauliza wenzangu.

1. Maendeleo ya watoto ambau huwa best katika hatua zinazoendelea kwa mfano high school na vyuo? je bado wanakuwa best huko? kazini nk?

2. Ubunifu wa hawa vichwa vyetu. je matokeo haya yanatafsiri uwezo wao wa ubunifu katika maisha?

3. Value for money; kama wazazi na wandugu wa hawa vijana mbali ya lugha kuna kitu cha kujivunia kuhusu watoto wetu? Nami namsomesha wangu private but hata kama anafanya vizuri nahisi kama natumia pesa nyingi zaidi ya kile anachopewa...

Mpo huru kuongeza maswali....

Nawasilisha

==============

Wakuu nimefurahia angalau tumeweza kuwakumbuka wachache, but nahisi tumejaribu kujadili swala moja na kiasi la pili.

Katika hilo naona tumewajadili wa kwanza tu na sio angalau scope ya top ten or 20 na kadhalika. Nia ya huu mjadala ni kujaribu kuzinduka na kufuatilia records za hawa watu wetu. Huenda tukichimba kwa mbali utakuta wahadhili wengi wa vyuo vyetu wala hawakuwa top 100.

Pia tukichimba sana tunaweza kujua kama hizi shule bora zinatoa elimu bora au zinafundisha mbinu za kufaulu mitikani.

La mwisho... Tujiulize nini dhamira ya elimu? Kufaulu au kuelimika? And hapo huenda kuna mafunzo mengine mtambuka....
 
Nimesoma diploma na Tanzania one alikuja diploma baada ya kuvuruga advance. kwa kifupi wengi wakishakwenda advance husikii Tena ubest student. na hizi mbwembwe zinaishia pale advance ksb huko ndiyo Kuna shule bora za private. Huku mbele hakuna university bora ya private ndipo majanga yanapoanzia wananyakwa Sana
 
mwaka huo(2005) shule hii ilifanya vizuri sana kitaifa, nawaza vijan hawa watakuwa wapi kwa sasa
 

Attachments

  • 1456054708925.jpg
    1456054708925.jpg
    69.3 KB · Views: 320
Namfahamu martin chegere tu ambae ni mwalimu wa uchumi udsm kwa sasa.
jembe wa pugu sec....

daah wakat wote nimesoma economics pale department alikuwa masomon...
karudi huyu jammaa?
 
mwaka huo(2005) shule hii ilifanya vizuri sana kitaifa, nawaza vijan hawa watakuwa wapi kwa sasa
Mmoja nimesoma nae Tambaza, ni mtoto wa mkuu wa mkoa mmoja(kipindi hicho alikuwa naibu waziri wa elimu), alipata Div. 4, ikabidi aende india kusomea degree ya uchumi. Sijui sasa hivi yuko wapi ? Unawezakuta yupo BOT au taasisi nyingine kubwa
 
Profesa Mukandara yuko chuo kikuu Dar es salaam
Profesa Shivji yupo ni profesa
Profesa Lipumba yupo
Andrew Chenge yupo mbunge na ana nafasi kubwa tu
Profesa Sospeter Muhongo yupo ni waziri wa madini
DK harrison Mwakyembe yupo ni waziri
Dk Tulia ACKSON ni naibu Spika

Kwa ufupi wengi waliokuwa wakali kwenye masomo waliendelea kuwa vipanga na wako vyuo vya ndani na nje na wana nyadhifa nyingi tu serikalini.Mtu kama Profesa Shivji form six tabora alisoma combination ya PMM (Physcs,Pure Mathematics NA ADVANCED mathematics) Akaenda kusoma sheria akawaburuza na kuibuka kinara wa sheria kuwashinda wale waliosoma masomo ya arts kama HGL.Ni mwanasayansi aliyekuwa na akili mno kwenye sayansi na alipoingia kwenye sheria akabaki na akili zake zile zile hadi leo
 
Profesa Mukandara yuko chuo kikuu Dar es salaam
Profesa Shivji yupo ni profesa
Profesa Lipumba yupo
Andrew Chenge yupo mbunge na ana nafasi kubwa tu
Profesa Sospeter Muhongo yupo ni waziri wa madini
DK harrison Mwakyembe yupo ni waziri
Dk Tulia ACKSON ni naibu Spika

Kwa ufupi wengi waliokuwa wakali kwenye masomo waliendelea kuwa vipanga na wako vyuo vya ndani na nje na wana nyadhifa nyingi tu serikalini.

Mtu kama Profesa Shivji form six Tabora alisoma combination ya PMM (Physcs, Pure Mathematics NA ADVANCED mathematics) Akaenda kusoma sheria akawaburuza na kuibuka kinara wa sheria kuwashinda wale waliosoma masomo ya arts kama HGL.

Ni mwanasayansi aliyekuwa na akili mno kwenye sayansi na alipoingia kwenye sheria akabaki na akili zake zile zile hadi leo

Kuna Mwingine aliitwa Professor Kighoma Ally Malima akiwa Minaki Secondary 1960s Marekani walikuwa wana program ya kuchukua Vijana waliomaliza kidato cha Sita kwenda kuwaendeleza kielimu huko Marekani hivyo wali conduct mitihani ya majaribio.

Mmoja wa walimu wa kujitolea alikuwa anasomesha Minaki alimuona Kighoma kama mmoja wa Vijana wenye kipaji akamchukua aende akafanye huo Mtihani uliokuwa unafanyika Pugu Secondary. Akiwa Kidato cha Tatu alifanya Mtihan wa Majaribio na kuwa Mwanafunzi Bora.

Alichukuliwa akaenda kufanya Program ya Pre university Marekani akafaulu akaanza Degree mpaka akafikia level ya Uprofessa ndio Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikamuomba arudi nchini mwanzoni mwa Mika ya 1980s.
 
Hali wakuu?
Baada ya matokeo ya form iv kumekuwa na mihemko na tafsiri mbalimbali kuhusu shule za serikali na binafsi. mimi leo najiuliza pia nawauliza wenzangu

1. Maendeleo ya watoto ambau huwa best katika hatua zinazoendelea kwa mfano high school na vyuo? je bado wanakuwa best huko? kazini nk?

2. Ubunifu wa hawa vichwa vyetu. je matokeo haya yanatafsiri uwezo wao wa ubunifu katika maisha?
3. Value for money; kama wazazi na wandugu wa hawa vijana mbali ya lugha kuna kitu cha kujivunia kuhusu watoto wetu? nami namsomesha wangu private but hata kama anafanya vizuri nahisi kama natumia pesa nyingi zaidi ya kile anachopewa...

mpo huru kuongeza maswali.... nawasilisha

Umeleta hoja za msingi sana. HONGERA. Upo uwezekano mkubwa kabisa wizara husika wala haifahamu walipo hao vijana waliofanya vizuri miaka ya nyuma. Hata wale wa wanafunzi kwenye shule zinazoitwa za vipaji maalum kama kilakala, mzumbe, msalato na kadhalika sidhani kuwa huwa wanafuatiliwa...
 
Back
Top Bottom