Wako wapi wanafunzi bora (Tanzania One) wa miaka ya nyuma?

menny terry

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
509
667
Wakuu hii system ni ya muda sana hapa Tanzania. Anatajwa kijana ambae ameongoza Tanzania nzima kidato cha nne au kidato cha sita wanapelekwa bungeni na zawadi kibao wanapewa lakini hadi leo hii hawa vipanga wa mitihani hawajulikani walipo.

Je, kuna unayemjua na unajua anajishughulisha na nini?

Hali wakuu?

Baada ya matokeo ya form IV kumekuwa na mihemko na tafsiri mbalimbali kuhusu shule za serikali na binafsi. Mimi leo najiuliza pia nawauliza wenzangu.

1. Maendeleo ya watoto ambao huwa best katika hatua zinazoendelea kwa mfano high school na vyuo? Je bado wanakuwa best huko? kazini nk?

2. Ubunifu wa hawa vichwa vyetu. Je matokeo haya yanatafsiri uwezo wao wa ubunifu katika maisha?

3. Value for money; kama wazazi na wandugu wa hawa vijana mbali ya lugha kuna kitu cha kujivunia kuhusu watoto wetu? Nami namsomesha wangu private but hata kama anafanya vizuri nahisi kama natumia pesa nyingi zaidi ya kile anachopewa...

Mpo huru kuongeza maswali....

Nawasilisha

==============

Wakuu nimefurahia angalau tumeweza kuwakumbuka wachache, but nahisi tumejaribu kujadili swala moja na kiasi la pili.

Katika hilo naona tumewajadili wa kwanza tu na sio angalau scope ya top ten or 20 na kadhalika. Nia ya huu mjadala ni kujaribu kuzinduka na kufuatilia records za hawa watu wetu. Huenda tukichimba kwa mbali utakuta wahadhili wengi wa vyuo vyetu wala hawakuwa top 100.

Pia tukichimba sana tunaweza kujua kama hizi shule bora zinatoa elimu bora au zinafundisha mbinu za kufaulu mitikani.

La mwisho... Tujiulize nini dhamira ya elimu? Kufaulu au kuelimika? And hapo huenda kuna mafunzo mengine mtambuka....
 
Wengi wao wanapigishwa kazi ngumu tu.Na hii thread by the way haina maana kabisa, kwa sababu huwezi kutoa mawazo ya kujadili watu waliofanya vizuri kwenye mitihani, naona huu ni utoto,inabidi ujitofautishe na watoto maana hizi ndio stori zao.

Kingine wanafunzi wanasoma katika mazingira tofauti na kuwapa mtihani mmoja wafanye na kuwapongeza waliofaulu sio haki kabisa,Taifa libadilike.
 
Tupo mbona..wengi wetu ni ma CEO kwenye coy mbalimbali! Nature haipotei
***** wewe asiyejua nani kuwa ulichagulia second selection shule ya kata! Form IV ukapata 4,ukatiwa moyo ukajikunja ukarisit ukapa credit ukaingia A level.Napo ukaambulia div three ukatupwa UDOM chuo cha kata.Alafu eti unajishaua wewe ni CEO.LABDA WA MILEMBE!
 
Umeuliza swali umejibiwa! Period.
 
Peleka huko mada za kitoto ndo walewale tu Nimesoma na TO namba 5 TZ na nimelala nae rum moja chuo lakini ile shule ni ya kujibu mitihani sio kutoka ki lyf. Mpaka leo wenye bongo kichwani nikimaanisha uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo husani ya kimaendeleo ndo wamewin interviews na kupata kazi nzuri huku yy akiendelea kuhangaika na U TO wake na 1st class, coz kazi anazopata anaona hazilipi.
 
kuna mmoja wa f.six anasoma udsm mwezi uliopita alikuwa anafundisha tuition phy & chem a level old moshi sec, yaani serikali imeshindwa kumpa sponsor? Anategemea bodi ya mikopo! Na likikauka anahemea hela ya tuition yaani hawezi kutumia kipaji chake coz elimu ya bongo imeingiliwa na siasa yaani huko mambo vagarant sio lazima wampeleke nje hata hapa basi wakati wa likizo wampe kazi viwandani apate muda wa kukuza kipaji dah the gguy iz good at chemistry
 
amegundua tindikali mpya? Au ndo zile za kumeza organic? Acha utaira wewe elimu ya bongo ni kumeza tu nenda ud kaangalie vijana wanavyotoboa.
 
amegundua tindikali mpya? Au ndo zile za kumeza organic? Acha utaira wewe elimu ya bongo ni kumeza tu nenda ud kaangalie vijana wanavyotoboa.

Wanatoboa nini??? We ni maandazi!!eeeh acha umang'aa mbuzi mawe wewe ikiwa pyschology yenyewe inatambua kuwa kuna golden boys, silver boys na wooden boys kwa hyo kuna watu obvious wana upeo mkubwa ka vle uwezo wa kujifunza na kuelewa kwa mda mfupi, uwezo wa kushika na kuelewa vitu vingi kwa mda mfupi yaani extra orninary ktk learning, sasa wewe unmbwelambwela ka ma****ya alieona mzinga wa konyagi yaani inadhihirisha jinsi gani wewe ulivyo wooden
 
nyie si ndio walewale mnaotufanya ma-highest performers mabaasha zenu,kwanini ukae unishobokee kwa kufaulu mitihani? Ni bora ningekuwa nimegundua kitu chenye impact kwa jamii ningesema sawa,sasa jamani hata mitihani yani just piece of papers unasema mimi ni golden? Fikiria maisha kaka usipoteze mda kusema dah yule kichwa,huo ni ushule ya msingi ujanja ni kusaka ela na mwenye ela ana haki ya kusifiwa maana anapunguza idadi ya maskini nchini.
 
Wengi wao wanapigishwa kazi ngumu tu.Na hii thread by the way haina maana kabisa, kwa sababu huwezi kutoa mawazo ya kujadili watu waliofanya vizuri kwenye mitihani, naona huu ni utoto,inabidi ujitofautishe na watoto maana hizi ndio stori zao.

Kingine wanafunzi wanasoma katika mazingira tofauti na kuwapa mtihani mmoja wafanye na kuwapongeza waliofaulu sio haki kabisa,Taifa libadilike.
hata mazingira yakiwa sawa lazima awepo wa kwanza na wa mwisho.taifa libadilike vipi?!
 
Back
Top Bottom