Waliokosa mikopo miaka ya nyuma mpo wapi?

Abdy Misen

Member
Feb 4, 2021
12
16
Mimi ni mwanafunzi niliemaliza kidato cha 6 mwaka huu na kama kawaida niliomba mkopo kwa sabab natokea katika familia duni ili pengine niweze kuokoa jahazi nyumbani na kipindi tunasoma tuliaminishwa kuwa kufanya kwetu vizuri kungetupa fursa nzuri ya kupata mkopo ndio tumefanya vizuri lakini kinachosikitisha zaidi mpaka sasa SIJAPATA walau ata 0% na ada ni Mil1.3.

Mpaka sasa nimekosa matumaini ya kuendelea na masomo katik ngazi ya elimu ya juu na kwa hadhi ya elimu hii ni kama nilpoteza muda kwa zaidi ya miaka miwil wakat mwingine nawaona bora hata walosoma vyuo vya kati maana hata wana diploma na sio mimi tu wapo weeengi mno ambao mpaka sasa wapo mtaani na hawana uelekeo wowote wa kimaisha yaani miaka miwili tulioipoteza sasa ni kama tunajutia kupoteza huu muda na hali ya kuwa hatujui mtaani tunaingiaje sasa ndipo nimeona niletee huu uzi pengine waliokosa mikopo miaka ya nyuma watupe experience maana ni kundi ambalo halizungumziwi na ni kama waliachwa wapambane na hali zao.
 
Mimi ni mwanafunzi niliemaliza kidato cha 6 mwaka huu na kama kawaida niliomba mkopo kwa sabab natokea katika familia duni ili pengine niweze kuokoa jahazi nyumbani na kipindi tunasoma tuliaminishwa kuwa kufanya kwetu vizur kungetupa fursa nzuri ya kupata mkopo ndio tumefanya vizur lakin kinachosikitisha zaidi mpaka sasa SIJAPATA walau ata 0% na ada ni Mil1.3

Mpaka sasa nimekosa matumaini ya kuendelea na masomo katik ngazi ya elimu ya juu na kwa hadhi ya elimu hii ni kama nilpoteza mda kwa zaidi ya miaka miwil wakat mwingin nawaona bora ata walosoma vyuo vya kati maana ata wana diploma na sio mimi tu wapo weeengi mno ambao mpaka sasa wapo mtaan na hawana uelekeo wowot wa kimaisha yaan miaka miwili tulioipoteza sasa ni kama tunajutia kupoteza huu muda na hali ya kuwa hatujui mtaan tunaingiaje sasa ndipo nimeona niletee huu uzi pengine waliokosa mikopo miaka ya nyuma watupe experience maana ni kundi ambalo halizungumziwi na ni kama waliachwa wapambane na hali zao!!
Nilikosa nikaandika barua ya kughairisha mwaka japo nilikua na vigezo vya yatima ila sikuwa na cheti kimojawapo cha kifo cha mzazi mmoja...

Mwaka uliofuata nikaomba tena kwa kuweka vyeti vyoote nikapata

Aise sitosahau maumivu niliyopata kuona wenzangu wananendelea na chuo, wamepata mikopo na hawana vigezo vyovyote

Kila kitu na muda wake nilihitimu na kazi sijapata mpaka sasa.
 
Umehitimu mwaka gani
 
Daah Hongera na pole pia ambacho naona hapa tunapewa elimu inayotufanya tuwe tegemezi na sasa inapofika muda unategemea bodi ya mikopo ndio unapigwa tiktak ambay unaweza hisi dunia nzima haipo na wewe kabisaaa
 
Jiwe alisema tunyimwe na ikawa hivo, ila ki roho safi fresh tu nilimaliza masomo

Hii nchi ukisoma shule za private za milioni mbili kwa mwaka kwa sababu ya umasikini watu wanaamini umetoka familia nzuri kumbe hakuna kitu watu.
 
Wakati mwingine nadhan wazazi waliosomesha watoto wao private wanafaa kupongezwa saana maan wamejinyima meeng saaan na kupambana kwa kila hali ili mtoto wao asome lakin bado serikali inakosa fadhila hata kwao na kuona wana uwezo wa kuwasomesha hata Vyuoni
 
Moja ya mambo ya hovyo serikali inafanya ni swala la kusimamia elimu ya juu, hivi inaingiaje akilini wanafunzi wanachaguliwa kwenda vyuo vikuu halafu wanashindwa kujiunga kisa mikopo?

Hivi serikali haitambui kwamba yenyewe ndo ina wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wote hasa waliochaguliwa kwenda vyuo vikuu vya umma wanawezeshwa kufanya masomo yao?

Nilileta hoja humu kwa nini serikali wasianzishe mfuko wa elimu ya juu utakaochangiwa na tozo zitakazowahusisha makundi yote ya jamii (wakulima, wafanyakazi, wafanyabishara nk.) ili kuhakikisha pesa za kusomesha wanafunzi elimu ya juu zipo za kutosha badala ya utaratibu wao wa sasa wa kuweka vigezo visivyo na uhalisia ambavyo vinabagua wanafunzi wengine!​
 
Mimi nilikosa mkopo. Kwa kweli ni jambo jema sana, maana mpaka sasa sidaiwi na serikali.
 
Jiwe alisema tunyimwe na ikawa hivo, ila ki roho safi fresh tu nilimaliza masomo

Hii nchi ukisoma shule za private za milioni mbili kwa mwaka kwa sababu ya umasikini watu wanaamini umetoka familia nzuri kumbe hakuna kitu watu.
Wengine unakuta wamesaidiwa tu na ndugu, wazazi ni choka mbaya, sasa msaada wa ndugu siyo wa kutegemea mwanzo mwisho.......

Hiki kigezo cha private naona hakina uhalisia wowote na kinaweka tu matabaka kutaka kunyima haki ya elimu ya juu kwa vijana walio wengi. Shule za private zipo nyingi sana kwa sasa na siyo kwamba wote wanaosoma shule hizo ni watoto wa matajiri, asilimia kubwa ni watoto wa wazazi wenye uwezo wa kawaida tu ambao labda muda wa kulipa ada ukifika wanakuwa wanahangaika huku na kule ikiwemo kuomba msaada wa ndugu na marafiki.​
 
Ukiwacheki wanao uliosoma nao o level kila mtu kapata, wale wa advance kila mtu kapata ukilogin kwako unaona Hamna kitu una-refresh Hamna kitu
 
Mimi ni mwanafunzi niliemaliza kidato cha 6 mwaka huu na kama kawaida niliomba mkopo kwa sabab natokea katika familia duni ili pengine niweze kuokoa jahazi nyumbani na kipindi tunasoma tuliaminishwa kuwa kufanya kwetu vizuri kungetupa fursa nzuri ya kupata mkopo ndio tumefanya vizuri lakini kinachosikitisha zaidi mpaka sasa SIJAPATA walau ata 0% na ada ni Mil1.3.

Mpaka sasa nimekosa matumaini ya kuendelea na masomo katik ngazi ya elimu ya juu na kwa hadhi ya elimu hii ni kama nilpoteza muda kwa zaidi ya miaka miwil wakat mwingine nawaona bora hata walosoma vyuo vya kati maana hata wana diploma na sio mimi tu wapo weeengi mno ambao mpaka sasa wapo mtaani na hawana uelekeo wowote wa kimaisha yaani miaka miwili tulioipoteza sasa ni kama tunajutia kupoteza huu muda na hali ya kuwa hatujui mtaani tunaingiaje sasa ndipo nimeona niletee huu uzi pengine waliokosa mikopo miaka ya nyuma watupe experience maana ni kundi ambalo halizungumziwi na ni kama waliachwa wapambane na hali zao.
Kuna mwanajamii ameandika Uzi ,ana GPA 4 na miaka kibao Hana kazi.
Swali langu ni Nini kinakuhakikishia kupata ajira baada ya kumaliza degree Yako?
Ushauri,jitolee sehemu au ktk industry unayoipenda na ukisha pata uzoefu omba uajiriwe na baada ya kuajiriwa katafute degree iwe kama license.
Lakini wengi hufanya kinyume
 
Mimi pia nilikosa mkopo nililalama sana zaidi ya ujuavyo.
Nilizunguka sana ofisi za bodi ya mikopo pasi na mafanikio lakini mungu si athumani namshukuru sana mbunge wa Jimbo la morogoro mjini mh abood na sitomsahau HoD wangu wa EMPs na Kila siku ntawashukuru classmates wangu walisimama na Mimi waliakikisha ada inalipwa kwa miaka yote mitatu na hatimaye NAMI nilifanikisha ndoto yangu nilihitimu kwa stress nyingi sana chuo
 
Wengine unakuta wamesaidiwa tu na ndugu, wazazi ni choka mbaya, sasa msaada wa ndugu siyo wa kutegemea mwanzo mwisho.......

Hiki kigezo cha private naona hakina uhalisia wowote na kinaweka tu matabaka kutaka kunyima haki ya elimu ya juu kwa vijana walio wengi. Shule za private zipo nyingi sana kwa sasa na siyo kwamba wote wanaosoma shule hizo ni watoto wa matajiri, asilimia kubwa ni watoto wa wazazi wenye uwezo wa kawaida tu ambao labda muda wa kulipa ada ukifika wanakuwa wanahangaika huku na kule ikiwemo kuomba msaada wa ndugu na marafiki.​
nina mashaka saana kama wahusika wa Bodi wana uelewa wa hakika yale ambayo wanafunzi tunayapitia pengine wao hawakusoma katik mazingira magumu kwa hivo kwao inakua vigumu kutathmini uhitaji wa mtu na kuamua kusingizia vigezo
 
Mimi pia nilikosa mkopo nililalama sana zaidi ya ujuavyo.
Nilizunguka sana ofisi za bodi ya mikopo pasi na mafanikio lakini mungu si athumani namshukuru sana mbunge wa Jimbo la morogoro mjini mh abood na sitomsahau HoD wangu wa EMPs na Kila siku ntawashukuru classmates wangu walisimama na Mimi waliakikisha ada inalipwa kwa miaka yote mitatu na hatimaye NAMI nilifanikisha ndoto yangu nilihitimu kwa stress nyingi sana chuo
Pole na Hongera mkuu naona ss ndio njia ninayoiendea
 
Jiwe alisema tunyimwe na ikawa hivo, ila ki roho safi fresh tu nilimaliza masomo

Hii nchi ukisoma shule za private za milioni mbili kwa mwaka kwa sababu ya umasikini watu wanaamini umetoka familia nzuri kumbe hakuna kitu watu.
Hawajui kama wazee wanajibana na kupambana ili mtoto wao asome...ni hivyo tu hakuna mikopo ya sekondari wangeona namna watu wangeapply pia.
Kinachofanyika ni mzazi kupambana walau mtoto wake avuke sekondari na aingie chuo ambapo anajua serikali itampokea mzigo, lakini wao wanachoona ni kama vile wazazi wanosomesha watoto wa pvt wan helaaaaa
 
Wengine unakuta wamesaidiwa tu na ndugu, wazazi ni choka mbaya, sasa msaada wa ndugu siyo wa kutegemea mwanzo mwisho.......

Hiki kigezo cha private naona hakina uhalisia wowote na kinaweka tu matabaka kutaka kunyima haki ya elimu ya juu kwa vijana walio wengi. Shule za private zipo nyingi sana kwa sasa na siyo kwamba wote wanaosoma shule hizo ni watoto wa matajiri, asilimia kubwa ni watoto wa wazazi wenye uwezo wa kawaida tu ambao labda muda wa kulipa ada ukifika wanakuwa wanahangaika huku na kule ikiwemo kuomba msaada wa ndugu na marafiki.​
Wenye hela zao wanasomesha wtt wao IST huko na FEZA sie wengine tunopishana hizo shule za pvt nyenginezo ni wa kawaida tu. mtu mpaka uchukue mkopo bank ndio ulipe ada. Unatamani mtt amalize form 6 fasta angalau serikali ikupokee mzigo. Lakini ndio hivyo, kila pahali mpaka uwe na mtu wa kukupenyeza
 
Back
Top Bottom