Wako wapi wanafunzi bora (Tanzania One) wa miaka ya nyuma?

Wapo BOT,Voda, tigo,Aga Khan Hospital, wanafundisha Havard , Wapo US Embassy , Price Water House coopers, ,wachungaji wa makanisa makubwa, na mapadre hasa kutoka seminari ambazo kila mwaka zinaongoza,na akinadada wengi ni masista, Miss Tanzania na makampuni ya urembo,Waliopata Division zero Wengi ni mateja magomeni na mwananyamala,Waliopata division four wengi WANA BETI kwenye meridian sports,na wanaendesha bodaboda, Wanaosha magari kwenye makutano barabara, Wanauza madafu barabani, na wachche wanaomba omba barabarani.


#Kupanga ni kuchagua
 
Mmoja wa Best students kidato cha Nne 1994 katumbuliwa jipu na NAPE huko TBC hivi karibuni kwa utendaji usioridhisha!!

Unao uhakika na ulichoandika humu? Mtaje jina na shule aliyosoma.
 
Nimesoma diploma na Tanzania one alikuja diploma baada ya kuvuruga advance. kwa kifupi wengi wakishakwenda advance husikii Tena ubest student. na hizi mbwembwe zinaishia pale advance ksb huko ndiyo Kuna shule bora za private. Huku mbele hakuna university bora ya private ndipo majanga yanapoanzia wananyakwa Sana



Duh....hiyo mpya hebu weka jina lake
 
Kota alidisco udsm 2009, hakumaliza sheria. Nimeupenda huu uzi, wapo wap wale mato? Kina lusekelo, emily, mwinzarubu n.k, na je wanaperform kwel huko waliko
 
Namfahamu martin chegere tu ambae ni mwalimu wa uchumi udsm kwa sasa.

Pia yupo Marehemu balozi Fulgence Kazaura.Huyu kafariki mwaka juzi akiwa makamu wa mkuu wa Chuo kikuu cha Dare salaam.Huyo alifanya mitihani ya kumaliza sekondari ya Cambridge ambayo hufanyika dunia nzima akashika nafasi ya kwanza duniani akawamwaga hadi waingereza wenyewe.
 
Wapo BOT,voda,tigo,hospitali mbalimbali,wachungaji na mapadre hasa kutoka seminari ambazo kila mwaka zinaongoza,na akinadada wengi ni masista,Waliopata Division zero Wengi ni matejA,Waliopata division four wengi WANA BETI kwenye meridian sports,na wanaendesha bodaboda,
hili ni jipu
 
Waliopata division four wengi WANA BETI kwenye meridian sports,na wanaendesha bodaboda,

Waliopata division four wengi hasa wale waliosoma zile shule za international school wengi ni MA DJ na wafanyakazi wa MA-CASINO.Kwa Ma DJ Utasikia wanaongea kile kizungu cha kubana midomo Everybody say YEEEE wakiwa wamevaa miwani ile mikubwa myeusi usiku kwenye kumbi zenye giza wakiwa wanafanya u-DJ wao
 
Profesa Mukandara yuko chuo kikuu Dar es salaam
Profesa Shivji yupo ni profesa
Profesa Lipumba yupo
Andrew Chenge yupo mbunge na ana nafasi kubwa tu
Profesa Sospeter Muhongo yupo ni waziri wa madini
DK harrison Mwakyembe yupo ni waziri
Dk Tulia ACKSON ni naibu Spika

Kwa ufupi wengi waliokuwa wakali kwenye masomo waliendelea kuwa vipanga na wako vyuo vya ndani na nje na wana nyadhifa nyingi tu serikalini.Mtu kama Profesa Shivji form six tabora alisoma combination ya PMM (Physcs,Pure Mathematics NA ADVANCED mathematics) Akaenda kusoma sheria akawaburuza na kuibuka kinara wa sheria kuwashinda wale waliosoma masomo ya arts kama HGL.Ni mwanasayansi aliyekuwa na akili mno kwenye sayansi na alipoingia kwenye sheria akabaki na akili zake zile zile hadi leo
Mkuu naomba ufafanuzi Dk Harrison Mwakyembe Kwa kumbukumbu zangu ambazo ziko Sawa kabisa,alisoma Diploma ya uandishi wa Habari pale DSJ,Je alisoma diploma baada ya kuwa mwana funzi Bora wa mitihani ya kidato Cha nne au Cha Sita ndio akaenda DSJ??
 
shule na utajiri ni inversely proportinal.

Matajiri wengi bongo wengi hawajasoma na hata waliosoma walikuwa wanafaulu kawaida.

Maisha ni zaidi ya GPA kubwa, maisha ni kutumia akili za ziadaa

Kila mtu ana nafasi yake kwenye hii dunia.Tajiri ana nafasi yake na msomi mkali ana nafasi yake.Fikiria kia mtu angekuwa hakusoma lakini Tajiri.Halafu ikatokea kipindupindu kwenye hiyo dunia ya kufikirika yenye matajiri watupu ambao hawakusoma nani angewatibu? Lazima DAKTARI hapo msomi kipanga mwenye GPA kubwa aingie hapo awasaidie vinginevyo matajiri wote wasiosoma watakufa kwa kipindu pindu na utakuwa ndio mwisho wa utajiri wao!!!
 
Namkumbuka Isaac Manyalla, miaka ya 90 mwanzoni alifumua mbaya A Level pale Milambo Sec Tabora.
Badae aaliendelea kufanya poa sana akiwa pale UDSM, Na alikuja akaajiriwa B.oT akiwa amepewa kitengo.
Mwisho sijui ilikuaje nikaja stukia Akiwa bwana mkubwa kabisa pale Mwananchi Gold hapo miaka ya 2000 mwanzoni.
Then sijui nini ilikua jamaa akatoka pale, now anafanya vizuri kitaa akiwa ni mkurugenzi wa kampuni yake flani
 
Back
Top Bottom