Changamoto zipi Jamii (wazazi na wanafunzi) hupitia kipindi wakisubiri baraza la mitihani NECTA lisahihishe na kutoa matokeo ya mitihani ya wanafunzi?

Hamud1988

Member
Aug 10, 2017
14
10
Kipindi cha kusubiri matokeo ya mitihani kwa shule za msingi na sekondari huwa ni mwezi 1-3. matokeo haya ndio uhamua mwanafunzi huyu aendelee na shule (kidato cha kwanza au kidato cha tano/vyuo vya ufundi) au atafute Maisha kwa namna nyingine. Ndani ya kipindi hiki (miezi 1-3) yamekuwepo matukio mbalimbali yaliyolipotiwa kutokea yakiwahusisha wanafunzi hawa wanaosubiri kuendelea na masomo, yakiwemo matukio yanayohusisha wanafunzi hawa kuolewa au kuoa kabla ya matokeo ya mitihani kutoka na hivyo serikali kutumia nguvu kuwatoa kwenye ndoa zao (rasmi au zisizorasmi) ili wakaendelee na masomo.

Wewe kama mdau wa elimu unadhani ni changamoto gani nyingine wanafunzi na jamii kwa ujumla upitia wakati wakisubiri matokeo yatangazwe? Je, ni upi utatuzi sahihi wa changamoto hii?​
Rejea:
MWANAFUNZI ALIYEFAULU KIDATO CHA TANO AOLEWA
Mwanafunzi aolewa kwa Sh30,000, DC aingilia kati

POLISI WAZUIA NDOA YA MWANAFUNZI
Gumzo: Ndoa ya Mwanafunzi yazuiwa Shinyanga, Polisi watinga na mitutu ya Bunduki eneo la tukio

page01.jpg
 
Back
Top Bottom