Wako wapi wanafunzi bora (Tanzania One) wa miaka ya nyuma?

Wako wapi wanafunzi bora (Tanzania One) wa miaka ya nyuma?

Mmoja wao ni mimi.

Natokeo kundi la wale wasiosoma twisheni kabisa, shule nzima olevel ilikuwa na walimu 6, kwa shule ya wanafunzi 470.
Kila muhura tulikuwa tunawahi kufunga kati ya wiki tatu hadi nne kwa kuwa wazabuni wamegoma kuleta chakula.
Nikafanikiwa kupata division 1:16, nilipoenda Advance maji yakawa marefu nikapata 2:12, sababu ni kuwa sikuwa na msingi mzuri kwa kuwa olevel ilikuwa ni kusolve past paper tu. Necta waliporudia maswali nikawaumiza.

Makofi kwangu tafadhali

Duh, wewe nawe...MAKOFI YA NINI HAPO.
 
Wale wa zamani kuna mmoja inasemekana amefia marekani lkn hakuna ajuaye kaburi lake lilipo wala hakuna aliyehudhuria mazishi yake na Mwingine mwenye macho ya nyoka yenye makengeza anaongoza Bunge letu akiwa ni mmoja wa wenyeviti hii ikiwa ni zawadi aliyopewa baada ya kupiga dili za maana
 
Kuna mmoja alimaliza miaka ya 90 kama sijakosea ni Christina Tungaraza alikuwa mwanafunzi bora halafu ana ushape wa hajaa. Mwaka juzi kama si mwaka jana nimemuona nje ya standard chartered bank sikujua kama ni mfanyakazi au alikuwa mteja. Pia anaonesha alikuwa hajaolewa (hakuwa na pete kidoleni) lakini pia sikuwa na uhakika wengi wao wanafeli mapenzi.
Sijui nilichoandika kimeeleweka.......
Kasie.
 
Nadhani umechanganya Jina.
Aliyekimbiza mitihani hiyo ni Sir George Kahama tena Mitihani hiyo ya Camridge ndio iliepelekea akaitwa na Malkia Elizabeth akatunukiwa cheo cha SIR!! Huyu alikuwemo kwenye Baraza la kwanza la Mwalimu Nyerere na hata kwenye Utawala wa Mzee Mkapa alipata kuwa Waziri wa Kilimo na Ushirika.
G Kahama sio Sir acha story za mapokeo alipewa tu na Mwalimu kwa utani kwa jinsi alivyokua na mbwembwe za kinshomile
 
Mmoja wa advanced aliishiaaa kutapel wanafunzi eti atawaleteaa vitini vya biology na chemistry
 
Profesa Mukandara yuko chuo kikuu Dar es salaam
Profesa Shivji yupo ni profesa
Profesa Lipumba yupo
Andrew Chenge yupo mbunge na ana nafasi kubwa tu
Profesa Sospeter Muhongo yupo ni waziri wa madini
DK harrison Mwakyembe yupo ni waziri
Dk Tulia ACKSON ni naibu Spika

Kwa ufupi wengi waliokuwa wakali kwenye masomo waliendelea kuwa vipanga na wako vyuo vya ndani na nje na wana nyadhifa nyingi tu serikalini.Mtu kama Profesa Shivji form six tabora alisoma combination ya PMM (Physcs,Pure Mathematics NA ADVANCED mathematics) Akaenda kusoma sheria akawaburuza na kuibuka kinara wa sheria kuwashinda wale waliosoma masomo ya arts kama HGL.Ni mwanasayansi aliyekuwa na akili mno kwenye sayansi na alipoingia kwenye sheria akabaki na akili zake zile zile hadi leo
Naongeza huyu mtu. Prof. Luhanga habari yake ndefu sana.
 
Alitupitiaa akala zetuu ihungo high school
 
Nchi hii hajapata kutokea T.O kama the late Prof. Justinian Rweyemamu. Huyu alikuwa T.O wa Dunia nzima enzi zile Tanganyika inafanya mitihani ya Cambridge pamoja na dunia nzima. Amepata kuwa scholar Havard University na Lecturer Havard University. Pia aliwahi kuwa Mwalimu UDSM na Permanent Secretary Ministy of Economic Planning wa Serikali ya Awamu ya Kwanza.

Kwa Tanzania sijapata kumuona msomi wa kweli kama huyu katika mchango wake kwenye elimu. Labda kidogo Prof. Shivji
Unajua kirefu cha T.O? Eti T.O wa Dunia nzima!!!!!! T. O= Tanzania One sasa inakuaje awe Tanzania one wa Dunia nzima? Ila nimekuelewa ndg yangu wa Mupe.......Muruke.....!!! Huyo Prof alikuwa na firm yake ya Auditing baada ya kufariki kuna wahuni mpaka leo wanatumia Signature na Muhuri wake kukagua vitabu vya hesabu kutokana na Reputation ya jina lake!
 
Kuna mmoja alimaliza miaka ya 90 kama sijakosea ni Christina Tungaraza alikuwa mwanafunzi bora halafu ana ushape wa hajaa. Mwaka juzi kama si mwaka jana nimemuona nje ya standard chartered bank sikujua kama ni mfanyakazi au alikuwa mteja. Pia anaonesha alikuwa hajaolewa (hakuwa na pete kidoleni) lakini pia sikuwa na uhakika wengi wao wanafeli mapenzi.
Sijui nilichoandika kimeeleweka.......
Kasie.

Wala hakijaeleweka kabisa.

Huku hakukufai wewe. Baki tu kule MMU.
 
Wala hakijaeleweka kabisa.

Huku hakukufai wewe. Baki tu kule MMU.

Hahahahahahaaa Nyani banaa. .... ndo hapo huwa nakupenda. Mie nilijistukia nilichoandika maana nina kitu nataka kukielezea ila jinsi ya kukielezea ndo nimefeli. Sijui lugha labdaa. .....
Ngoja nijarihu kuelezea kwa kisukuma 😉😉😛
Kwanza hata sikuangalia kwani hili ni jukwaa gani?
 
Back
Top Bottom