Wakina nani walikuwa/wanampiga majungu Makonda? Kauli ya "sisi" na "wenzetu" inihataji jicho la ziada

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Akiwa Simiyu amesema kuna watu walipika majungu kwa muda mrefu kwamba "wale" ni wabaya lakini hawakuweza hata kufanya kazi walipopewa nafasi hali iliyopelekea yeye aitwe kukaa hapo.

Amesema sasa watu hao wana nongwa watu kujaa sana katika mikutano yake, amesema shida kubwa ni "wapambe" wengine wanasema ziara zake akiachwa hivi hivi atakuja kuwasumbua mbele ya safari. Wanakereka hata watu wakijaa katika mikutano yake.

Kauli nzito zaidi kuitoa amesema, "Sisi" kawaida yetu tukipewa kazi tunafanya kazi, "wenzetu" wakipewa kazi wanafanya kazi ya majungu tena.

Maswali kadha ni pamoja na
1. Wapika majungu na wapambe ni kina nani?
2. Wao ni kina nani na wenzao ni kina nani?
 
Makonda anawasema wakina Kinana, Nchimbi na wengine wa sampuli hiyo, wanaomuona anakosea kwenye wkile anachofanya.

Ndio maana anasema wanakereka hata watu wakienda kwenye mikutano yake, ina maana hao jamaa wanataka watu wasiende kwenye mikutano ya Makonda..

Na pale anaposema wao walipewa wakashindwa, nakumbuka kuna wakati Kinana na Chongolo walijaribu kuzunguka mikoani mwishowe zile ziara zao zikaja kufa kifo cha mende.

Samia kwa kutambua hilo ndio maana akaona amuweke Makonda hapo, alijua kazi iliyoko mbele yao sio ya kitoto na wale aliowaamini kuifanya walishindwa.

Hapo ndipo naona madai yake ya kusema wao ni kazi tu yanapopata nguvu, kwasababu ni kweli kuna waswahili walipewa hiyo kazi ikawashinda.

All in all naona 2025 CCM patakuwa na makindi ya wazi kabisa..

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Huyo ni mkabila, nchi hii hakuna msukuma alishawahi kuwa na cheo kikubwa mpaka alipokuja Magufuli alipandikiza chuki na kuigawa nchi, hakuna cha maana alichokamilisha. Makonda yeye binafsi nchi hii amefanya nini cha maana. Hilo ni lifala flani linapalilia ukabila.
Pambaf kabisa wewe kwamba jiwe hakufanya chochote,bloodfool
 
Akiwa Simiyu amesema kuna watu walipika majungu kwa muda mrefu kwamba "wale" ni wabaya lakini hawakuweza hata kufanya kazi walipopewa nafasi hali iliyopelekea yeye aitwe kukaa hapo.

Amesema sasa watu hao wana nongwa watu kujaa sana katika mikutano yake, amesema shida kubwa ni "wapambe" wengine wanasema ziara zake akiachwa hivi hivi atakuja kuwasumbua mbele ya safari. Wanakereka hata watu wakijaa katika mikutano yake.

Kauli nzito zaidi kuitoa amesema, "Sisi" kawaida yetu tukipewa kazi tunafanya kazi, "wenzetu" wakipewa kazi wanafanya kazi ya majungu tena.

Maswali kadha ni pamoja na
1. Wapika majungu na wapambe ni kina nani?
2. Wao ni kina nani na wenzao ni kina nani?
Suku gang vs Msoga gang
 
Huyo ni mkabila, nchi hii hakuna msukuma alishawahi kuwa na cheo kikubwa mpaka alipokuja Magufuli alipandikiza chuki na kuigawa nchi, hakuna cha maana alichokamilisha. Makonda yeye binafsi nchi hii amefanya nini cha maana. Hilo ni lifala flani linapalilia ukabila.
Shujaa alikujeruhi malinda
 
Back
Top Bottom