Wakili Pasco Mayalla -A True Story of My Life: Nilitamani kuwa Wakili sababu ya Wakili Murtaza Lakha, sasa ni Wakili. Je, nitakuwa kama Lakha? Part II

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,497
113,592
Wanabodi,

Nipashe ya leo, Story Inaendelea...

Screen Shot 2022-07-24 at 12.39.19 PM.png
Screen Shot 2022-07-24 at 12.42.36 PM.png

Kwa Wasomaji wapya, hii ni stori ya safari yangu ya ndoto ya kuwa wakili, iliyonichukua iliyoanzia Mwanza mwaka 1976 takriban miaka 45 iliyopita, hatimaye nimekuwa wakili mwaka huu, hivyo kujiuliza jee sasa, bado naweza kuwa kama Wakili Murtaza Lakha?. Kwa ambao hawakubahatika kusoma mwanzo, anzieni hapa Wakili Pasco Mayalla - A True Story of My Life: Nilitamani kuwa Wakili sababu ya Wakili Murtaza Lakha, sasa ni Wakili. Je, nitakuwa kama Lakha? Part 1

Wiki iliyopita story ilishia baba yangu Mzee Andrew Mayalla, aliyekuwa ofisa wa serikali Mwanza, tulihamishwa usiku usiku kurejeshwa kijijini. Kisha huko kijijini, akafuatwa na watu wa kazini kwake akachukuliwa na kupelekwa kusikojulikana, mimi nikidhani amesafiri, nami kufuatwa na Baba yangu mdogo, Mzee Mathew Kasanga kuja kuishi nyumbani kwake Dar es Salaam, bila kuambiwa nini kilimtokea Mzee Mayalla… sasa tuendelee.

Kwanza niwarudishe kidogo nyuma, kwenye ile kisanga ya kuhamishwa usiku, usiku!. Kumbe ile hama hama ya usiku usiku kwa majirani 4 wa eneo la Isamilo ya chini ya mwaka 1976 na majirani zetu wote, RPC, RSO, DSO na OCD ambao tuliishi nyumba zilizofuatana, haikuishia kwetu tuu, bali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter Kisumo naye alistaafishwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Samweli Pundugu alistaafishwa, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena alistaafishwa!, hawa ni maofisa wa kiutendaji serikalini.

Wanasiasa nao hawakubaki Salama, Makamo wa Pili wa Rais, Rashidi Kawawa, aliondolewa, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, aliambiwa kuandika barua ya kustaafu mwenyewe. Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa naye alimriwa kuandika barua. Ni kisa hiki cha 1976 ndicho kilileta reforms kubwa za kwanza kwa Idara!.

Mwaka 1979, Nikiwa darasa la 5, Shule ya Msingi ya Oyster Bay, Vita vya Kagera vimeisha, Tanzania tumeshinda,
tayari nimeisha anza kusoma magazeti ya Mzalendo siku za Jumapili, Kesi ya Mauaji Mwanza ilipoanza kurindima, na kuripotiwa kwenye kipindi cha Majira cha RTD na Jumapili kwenye gazeti la Mzalendo, kwanza hiyo ndio ikawa mara yangu ya kwanza kujua Baba yangu Mzee Mayalla, alikuwa ni nani, alikuwa anafanya kazi wapi, baada ya kuona jina lake gazetini kuwa ni miongoni mwa washitakiwa kesi hiyo ya Mauaji Mwanza!.

Unapokuwa unadhani baba yako yuko safari, unapokuja kujua, kwa kusoma gazetini na sio kuelezwa rasmi nyumbani!, what a shock!. Kitendo tuu kusikia mtu mwenye upendo wa type ya Mzee Mayalla, hata kuua tuu panya hawezi (me too) kuja sikia anahusika na kesi ya mauaji ya binadamu!, huwezi amini!. (Wazazi don’t under estimates uelewa wa watoto, muwe mnawaeleza watoto wenu vitu vinavyowahusu na sio wavisikie nje!)

Kitu cha kwanza, nilipata frustration, kwanini sikuambiwa mpaka kuja kusikia redioni na kusoma gazetini!. Nilipata stigma fulani!. Nyumbani ulikuwa ukifanya kosa kubwa adhabu yako ni kupigwa na kuambiwa kulala njaa. Kwa vile mimi sio mtoto wa kuzaliwa na Mama Kasanga, mimi angalau adhabu za bakora, ziliniepuka, ila kiukweli mama K, ni mkali, hataki ujinga ujinga. Kwa vile kulala njaa kwao ilikuwa ni adhabu, mimi nika develop eating disorders nikawa sili usiku.

Nilikuwa bonge, hii kesi ya Baba ikaanza kunikondesha. Baada ya kujua baba ana kesi, nika develop investigations skills za kuanza kufanya uchunguzi, kuhusu murder case, kumbe hukumu yake ni kunyongwa mpaka kufa!. What if baba atakutwa na hatia?. Kiukweli ni very traumatic!.

Shuleni kwetu nako kukaja mabadiliko ya uongozi, Mwalimu Mkuu alikuwa Ngalawa, akabadilishwa, akawa Mwalimu Nyalali, mke wa Jaji Mkuu, Francis Nyalali, shuleni kwetu tulikuwa na listi ndefu ya wake wa vibosile wa wakati huo, Mwalimu Rulegula, Mwalimu Sepeku, Mwalimu Apson, Mwalimu Linjewile, Mwalimu Toroka, Mwalimu Basimaki, Ramadhani, Sikwese, Sheushi, Liwali, Marealle, Nunduma na wengine wengi. Nikajisemea baba akikutwa na hatia, sitakubali, nitamshitaki huyu jaji kwa Jaji Mkuu!.

Darasani nilikuwa kipanga wa somo la hesabu, kuna swali la kutafuta eneo la umbo fulani la chombo cha chakula cha kuku. Darasa zima, wakapatia hilo swali, mimi pekee ndio nikakosea!. Tuliporudishiwa mtihani nilipokuta nimekosa, nikafanya upya na kupata jibu lile. Sikukubali, nilinyoosha kodole kuuliza nimekosaje?. Mwalimu akauliza darasa, jibu ni ngapi, darasa zima wakajibu jibu sahihi, mwalimu akasema umesikia jibu, bado nikamgomea, ila kwa vile nilikuwa kipanga, mwalimu akaniita niende mbele nikalifanye hilo swali ubaoni.

Kulifanya, likaja jibu lile lile jibu langu, mwalimu akamuita mwanafunzi mwingine, afanye ubaoni, akafanya na kupata lile jibu la wote, nikaambiwa nimekosea na kuzomewa!. Nilimgomea mwalimu na kusema hilo jibu limekosewa. Mwalimu akaangalia jibu kwenye kitabu cha Kiongozi kwa Mwalimu, kule jibu likakutwa ni lile la darasa zima!. Nikamuomba mwalimu tulifanye wote ubaoni!. Mimi ndio nikaitwa, kulifanya kipengele kwa kipengele, jibu likaja jibu langu!. Mwalimu akagundua jibu la kwenye kiongozi cha mwalimu limekosewa!. Akauliza mbona wengine wote wamepata jibu hilo hilo?. Ndipo ikakundulika darasani kwetu kuna mtoto wa mwalimu, amekuja na kiongozi cha mwalimu darasa zima waka copy, I was the only one who got it right. Papers za wengine wote zikusanywa, wakapigwa mikasi, mimi nikapewa pata, na from there nikawa ndio top wa vipanga wa hesabu!.

Kufuatia hii kesi, ukipanga ukaanza kuyeyuka!, darasani nilikuwa zivuki top ten, majibu kuja niko 10 la mwisho. Usiku kucha nilikuwa kama silali kwa mawazo. Hii bad performance ilimtibua sana mama. Jumapili moja nilitakiwa kusoma, nikaenda kwenye kochi kusoma kumbe nikasinzia!. Mzee K, akanikuta nimelala huku nimeshika daftrari, niliamshwa na mboko kutoka usingizini!, mpaka namaliza darasa la Saba, nilikuwa mwembamba!

Kwa jinsi ninavyomfahamu Mzee Mayalla, kuambiwa huyu ni muuaji, unajua kabisa sio kweli. Baba alikuwa anatetewa na Wakili Murtaza Lakha, nadhani kwa wakati huo he was the best. Na nadhani baba aliweza kutetewa na Murtaza Lakha kwasababu wakati huo Mzee Mathew Kasanga tayari ni tajiri mkubwa.

Enzi hizo magari ya mawaziri yalikuwa Peogeot 504, hiyo ndio ilikuwa gari ya Mzee Kasanga, mama nae ana gari lake, Renault, kuna gari la kuhudumia familia Volkswagen Combi, na kuna gazi la shamba, Landrover 109 short chasisi ya kibanda wazi. Hapo Drive In, nyumbani kwetu ni moja ya nyumba chache kuwa na TV na video. Japo life ilikuwa ni maisha bora, lakini mimi nilikuwa nakonda kwa kuhofia hatma ya baba yangu.

Faraja yangu pekee enzi hizo,ilikuwa ni kusoma gazeti la Mzalendo, lenye muhtaasiri wa kesi nzima, na kufurahi sana jinsi Wakili Lakha anawaumbua watu wa DPP, DPP wa enzi hizo akiwa ni William Sekule. Kesi ilikuwa inasikilizwa na Jaji Kiongozi Nasoro Mzavas.

Huu ukawa mwanzo wa mimi ku develop interviewing skills za maswali magumu, wale viongozi walio kalia kipindi change cha TV cha Kiti Moto, wanayajua maswali yangu, mwalimu wangu wa maswali yale sii mwingine ni Murtaza Lakha.

The Role ya Mzee Mayalla kwenye Kesi ya Mauaji Mwanza.

Kesi hiyo ilihusu oporesheni maalum ya kuwasaka watu wanaofanya mauaji ya vikongwe, ambapo watuhumiwa wawili, Masaga Mabula Mazegenuka wa mjini na Issack Ng'wana Ng'hoboko, walifariki, baada ya mahojiano, yaliyoendeshewa eneo la Kigoto, nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Jee ni kweli Mzee Mayalla alihusika?, jee Wakili Murtaza Lakha, alifanya nini katika kumtetea Mzee Mayalla?, Je ni nini kilichomfanya mtoto wa Mzee Mayalla, Pascal Mayalla atamani kuwa wakili?.

Tukutane jena juma lijalo katika sehemu ya tatu nay a mwisho ya simulizi hii ya Safari ya miaka 45 ya Uwakili ya mwandishi wa safu hii, Wakili Pascal Mayalla.

Wasalaam.

Wakili Pasco
 
Paskali ukiweza andika kitabu, kastory kako kananoga hutakosa chenchi kadhaa.

Au kwa heshima ya ukongwe wako huku jf. ikiwapendeza mods waiweke hii story sticky.

Hope itawavutia vijana wengi kwenye kufikia ndoto zao na wasikate tamaa hata wakikaribia uzeeni.
 
Paskali ukiweza andika kitabu, kastory kako kananoga hutakosa chenchi kadhaa.

Au kwa heshima ya ukongwe wako huku jf. ikiwapendeza mods waiweke hii story sticky.

Hope itawavutia vijana wengi kwenye kufikia ndoto zao na wasikate tamaa hata wakikaribia uzeeni.
Thanks kwa ushauri, I'll think about it.
P
 
Sasa nimeelewa kwanini unang'ang'nia kuwa mhe. Mbowe ni gaidi, ila kumbuka kama ulivyoumia wewe na kwa Mbowe wapo walioumia japo tofauti ni kwamba wewe umejikita kwenye hasira za tofauti ya vyama, hili halikubaliki.
Mkuu elvischirwa, nakuomba sana usinilishe maneno, sijawahi kutamka popote kuwa Mbowe ni gaidi, ila kufuatia mimi kuwa ni mtu wa Audio Visual (30 years, experience), nilithibitisha ile video ni bonafide genuine, kwa vile mimi sio mamlaka ya uchunguzi jinai, (DCI) na wala sio mamlaka ya kuendesha kesi jinai, (DPP) na sio mamlaka ya uthibitisho wa jinai, (mahakama) nilitoa tuu angalizo hili kuhusu Chadema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!
P
 
Una kumbuka full citation yake niiangalie Tanzlii?
This case licha ya kuwa na public interest, it's surprising it's unreported!. Haipo kwenye law reports as a result, haipo Tanzil!.

Hata police files zake zilikuja kutupwa. Nikiwa sekondari Tambaza, nikaenda kwa rafiki yangu mmoja anaitwa Martin Mpinga, dingi yake ni polisi, nikakuta lundo la police case files, ile sense of inquisitive yangu, nikafungua kusoma
..la haula!. Police files za Kesi ya Mauaji Mwanza!. Nikamuuliza Martin akasema ni ma fail ya kazini kwa baba yamehifadhiwa hapo!. Kumbe baadhi ya mafaili ya kazini ya polisi wetu wanaenda nayo home na kuyaacha yana zagaa zagaa, watoto wa polisi wanakuja na rafiki zao na kujisomea tuu kilichomo!.
P.
 
Back
Top Bottom