UHAINI: Murtaza Lakha VS Mhando

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,479
11,033
Mhando aliongeza kueleza kuwa pia alikuwa akimtambua mtu mwingine kwa jina la Piu Mtakubwa Lugangira au Father Tom na au Uncle Tom.Alimtambua ,alisema baada ya kumpeleka kwa mganga mmoja wa kienyeji huko Mwananyamala akifuatana na MacGhee mwenyewe pamoja pamoja na Martin Tamimu.

Shaidi huyo alidai kuwa baada ya kumpeleka huyo Lugangira au Father au Uncle Tom kwa mganga wa kienyeji,aliambiwa na MacGhee kuwa alikuwa na bahati na bahati kubwa mno ya kuweza kumwona Waziri Mkuu wa baadaye nchini Tanzania.Kwa wakati huo,Mhando aliongeza Father Tom au Uncle Tom alikuwa akiishi kwenye hotel ya Agip Motel.

Alipokwisha kukamilisha ushaidi wake,Mhando alianza kuhojiwa na Wakili Murtaza Lakha na kwanza alitakiwa kueleza ni kwa madhumuni gani alikwenda Harare,naye alijibu "Nilikwenda huko kwa matembezi".

Lakha:kutetembea tu na kuacha kushughulikia habari muhimu za kutoa taarifa juu ya njama za kutaka kumuua Rais na kupindua serikali? Wewe ni Mzalendo kweli?

Mhando:kimya.

Lakha:Baada ya kurejea kwako kutoka Harare,mbona hukuenda moja kwa moja kuonana na shaidi x?

Mhando:Nilikuwa nikishughulikia matengenezo ya gari yangu ambayo sikuweza kuiacha bila kuisimamia Mimi mwenyewe.

Lakha:kwani hungeweza kumchukua rafiki au ndugu yako kusimamia matengenezo hayo au hata kuiarifu polisi wakati wewe unakwenda kuwasilisha habari muhimu kama hizo kwa taifa?


Mhando:wazi kama hilo halikunijia akilini kwangu.

Lakha:wakati ukiondoka kuelekea Harare ,je ulipata kumwanga shaidi x

Mhando:Hapana,Lakini kwenye kiwanja Cha ndege nilikutana na Kizigha ambaye aliniuliza ni kitu gani nilikuwa nakusudia kumwambia shaidi x,lakini sikumwambia kitu kwa vile nilitaka kumwambia shaidi x mwenyewe.

Lakha:Na unaweza kueleza ni kwa nini hasa MacGhee alikuamini kiasi hicho na kukutapikia yote hayo bila wasi wasi wowote? Kwani wewe nawe ulikuwa mshiriki katika huo mpango?

Mhando alikataa yeye hakuwa yeye hakuwa ni mshiriki kwenye huo mpango lakini iliwezekana MacGhee aliamua kumweliza yote hayo kwa vile walikuwa ni marafiki.

Lakha:kwa hiyo ulimsaliti rafiki yako baada ya hapo? Au uliambiwa kuwa useme haya yote baada ya kuahidiwa kuwa angeachiwa huru?

Mhando:Hapana.
Mhando ambaye alionekana kupata kugwaya na kupata wakati mgumu sana,alipoendelea kujibu maswali ya Wakili Lakha ambayo kwa wingi yaligusia juu ya tofauti mbali mbali zilizojitojeza Kati ya ushaidi mahakamani na maelezo yake aliyoyatoa polisi wakati wa upelekezi wa kesi hiyo,alidai mahakamani kuwa yale ambayo alikuwa akisema humo mahakamani ndiyo yalipaswa kuchukuliwa kama ukweli wa mambo.

Lakha:Na ulianza kuendesha teksi lini?

Mhando:Mwaka 1982.

Lakha:Kabla ya hapo ulikuwa ukifanya kazi gani?

Mhando:Nilikuwa Meneja madai katika kampuni ya bima ya Business Efficiency Limited.

Lakha:Na kwanini uliacha kazi kubwa kama hiyo,unaweza kueleza?

Mhando:kwa sababu nilipenda kufanya Kazi ya biashara ya teksi.

Lakha:Wacha kudanganya.Siyo kweli kwamba uliacha Kazi hiyo baada ya kusababisha kampuni kupata hasara ya Tshs.300,000/= na kwamba ulikuwa ukikabiliwa na kesi ya upotevu wa donge hilo?

Mhando:Hayo sio kweli.Huo ulikuwa uamuzi wangu mwenyewe kuacha kazi.

Lakha:katika hiyo biashara yako ya teksi,ulikuwa ukiokota ngapi kila siku?

Mhando Tshs.1,000/=

Lakha:Hivyo kwa mwezi ulikuwa ukifunikaShs.30,000/= siyo?Na hilo donge kubwa sana eti?

Mhando:Inaonesha na hivyo.Lakini kwa kila siku nilikuwa nikimlipa mwenye teksi yake kiasi Cha Shs.500/= na nyingine zilizobaki zilikuwa ni ununuzi wa mafuta na chakula changu.Isitoshe gari yenyewe ilikuwa haifanyi kazi kila siku.

Akianza kujibu hoja ya Wakili T.J Tarimo ambaye alimtaka aeleze ni kwanini mara kwa mara alikuwa akitoa majibu ya kusema:hakujua chochote juu ya kile alichotakiwa kueleza,Mhando alijibu "sasa sikumbuki kila kitu kilichotokea Kati ya kipindi cha Juni 1982 na Januari 7,1983, wakati nilipokuwa nikimchukua MacGhee na wenzake kwa sababu muda mrefu umepita tayali"

Aliongeza kuwa wakati akiandikisha maelezo yake polisi wakati huo,alikuwa akikumbuka sana matukio yote na tarehe zake kuliko alivyoweza kukumbuka wakati akitoa ushaidi wake mahakamani kwa sababu zile zile kuwa muda mrefu ulikuwa tayali umepita tangu mambo hayo yatokee.

Tarimo:Umeieleza mahakama jinsi ulivyokuwa ukimchukua MacGhee na wenzake,je,uliwahi pia kumchukua Mbogoro?

Mhando:Ndiyo

Tarimo:ulimchukua lini?

Mhando: Sikumbuki tarehe.

Tarimo:Hukumbuki sasa,mbona ulisema hapo awali?

Mhando:Ilikuwa tarehe Desemba,lakini kabla ya tarehe 15.

Tarimo:Ikiwa kweli ulipata kumchukua Mbogoro, kwa nini hukupata kusema hayo wakati ukiandikisha maelezo yako polisi kuhusu kesi hii?

Mhando:Lakini nilimchukua.

Tarimo:Ndiyo kama kweli ulimchukua,Mimi nakuuliza kwanini unakumbuka vizuri sehemu zote ambazo ulikuwa ukimchukua MacGhee na kumpeleka na siyo Mbogoro?

Mhando:Nasema Sikumbuki kwa vile siwezi kukumbuka kila kitu.
Kadhalika Mhando alipozidi kuandwamwa kwa maswali,alisema,bila kutoa jibu la maana kuwa hakupata kutambua ni kwanini MacGhee aliamua kumweleza habari juu ya mpango huo"Ilikuwa ikitokea tu ananieleza",alidai Mhando.
Mhando alizidi kudai kuwa,kwa mara zote kuwa kwenye gari akimwendesha MacGhee,Kazi yake ilikuwa ni kumsikikiza tu MacGhee akiongea na Wala yeye (Mhando) hakuwa akisema chochote Wala kutoa majibu.

Tarimo:Je,Siyo kweli kwamba umeweza kumtambua Mbogoro hapa mahakamani kwa sababu mliwekwa nyote kwenye kituo Cha polisi Cha Buguruni wakati mlipokamatwa kuhusiana na kesi hii,na siyo kuwa ulikuwa ukimwendesha akiwa na MacGhee?

Mhando:Hiyo sio kweli

Tarimo:Na si kweli kwamba hapo mapema ulipotakiwa kumtambua Mbogoro ulihesabu mpaka ulipofikia Saba ndipo ukalipuka na kusema:ndiye huyo?

Mhando:Hiyo siyo kweli na Wala sitambui ikiwa wanakaa kizimbani kwa nambari.

Tarimo:Unataka mahakama haya yameze upuuzi huo unaosema? Mbona MacGhee ulimtambua kwa kusema ni mshtakiwa wa kwanza?Sasa hiyo haionyeshi kuwa unafahamu washtakiwa wanaketi kwa namba?

Mhando: Hapana.

Tarimo: Hapana nini?
Baada ya Mhando kukaa kimya bila kujibu swali hilo huku akitweta,Wakili Tarimo aliamua kumuuliza swali jingine akisema"je,una hakika na yote unayosema au umefundishwa nini Cha kusema hapa?

Mhando:Hapana mtu yeyote aliyenifundisha kitu Cha kusema.Nasema kama nilivyoona"
Alipoulizwa na Wakili Thomas L.Mkude kueleza ni kitu gani kilimfanya adhanie kuwa washtakiwa walikuwa na wakifanya mikutano yao kwenye kikosi Cha jeshi la Anga,Ukonga,alisema "Nilidhani hivyo kwa vile kila nilipowapeleka huko,walikaa muda mrefu sana wakizungumza".

Mkude:Na unakumbuka ni tarehe gani MacGhee alipokutuma ukawachukue vijana wawili kutoka kikosi hicho?

Mhando:Sikumbuki.

Mkude:Umesema ulikwenda Harare,je,kabla ya kwenda Harare ulipata kuwachukua?

Mhando:Ndiyo.

Mkude:Na baada ya kurejea kutoka Harare Desemba 31,1982 kama unavyodai,je,ulipata tena kufika nyumbani kwa Robert?

Mhando:Sikumbuki.Siwezi kukumbuka.

Mkude:Umesema kwamba siku uliyokwenda kwa Robert,ulikuta watu wengi wakiwa nyumbani kwake.Je,unaweza kueleza walikuwa ni watu wa aina gani?

Mhando:walikuwa ni wanaume.

Mkude:je,wewe ulipata kuingia ndani?

Mhando:La,sikupata kuingia.

Mkude:Sasa iwapo wewe hukuingia ndani,ni kitu gani kilikufanya uamini kuwa walikuwa na mkutano?

Mhando:Ni kwa sababu tu walikuwa wakikaa kwa muda mrefu sana.

Mkude:Je,Uliweza kufaham ikiwa baadahi ya watu waliokuwa ndani walikuwa ni jamaa au ndugu zake?

Mhando:sikuweza kujua

Mkude:Umezungumzia juu ya Biblia ,je,wewe mwenyewe umewahi kupata mafunzo ya Biblia?

Mhando:Hapana

Mkude:Umesema kuwa MacGhee na wenzake walikuwa wakinukuu maneno fulani kutoka kwenye hiyo Biblia,je,unaweza kuyakumbuka maneno hayo?

Mhando:Ndiyo.Walikuwa wakisema "ole wao wanaotawala kwa njia zisizo halali"

Mkude:Hayo maneno walikuwa wakisema hivi hivi tu au walikuwa wakinukuu Biblia kweli?

Mhando:Niliwaona wakifungua Biblia.

Mkude:Wapi?

Mhando:Ndani ya gari.

Mkude:Unakumbuka kuwa ulipoandikisha maelezo y'ako polisi ulisema kuwa Biblia hizo walikuwa wakiziacha nyumbani kwa Banyikwa na kuwa walikuwa hawatembei nazo?

Mhando:Mara nyingi walikuwa wakitoka nazo

Mkude:Sasa sisi tuamini yapi?Kwani hayo maelezo y'ako yamekosewa na polisi?

Mhando:Hapana yote mawili niya kweli.

mkude:Sasa hujioni wewe mwenyewe kuwa unazungumza uwongo na hali uko chini ya kiapo ?Hayo mawili yote yatakuwa ya kweli vipi ?Kati ya mawili ,moja huwa kweli na jingine uwongo.sasa hapa la kweli ni lipi?
Mhando aliposhindwa kabisa kujibu swali hilo,Mkude alizidi kumuuliza"umesema betri ulizoonyeshwa hapa mahakamani zinafanana na zile ambazo MacGhee alinunua je,kabla ya hapo ulipata kuona betri za aina hiyo?

Mhando:Hapana .....hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuziona.

Mkude:Na umesema kuwa MacGhee alikuambia kuwa betri hizo zilikuwa niza "walkie talkie",je,ulimuuliza wewe au alikuambia yeye mwenyewe?

Mhando: Aliniambia yeye mwenyewe.

Lakha Vs Stambuli na Luteni Ndejembi
.....................................................................................

Angalizo:Mod tafadharini sana,watu tunatumia muda mwingi kutafuta materials kuyapata,kusoma na kuandika,lakini mnafunga nyuzi bila sababu za msingi hii inakatisha tamaa ya kuandika.Huu Uzi msije fanya kama ule wa "Madhambi ya Mwl.Nyerere"
 
Kati ya mambo yanayonisikitisha hadi leo ni kushindwa kwa jaribio hili, lingefanikiwa tungekuwa mbali kiuchumi.
 
Back
Top Bottom