Wakili Pasco Mayalla - A True Story of My Life: Nilitamani kuwa Wakili sababu ya Wakili Murtaza Lakha, sasa ni Wakili. Je, nitakuwa kama Lakha? Part 1

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,
Hii ni Makala ya Jumapili hii,
Screen Shot 2022-07-17 at 8.55.20 AM.png
Screen Shot 2022-07-17 at 8.55.34 AM.png

Wapenzi wasomaji wangu wa safu hii ya "Kwa Maslahi ya Taifa", mimi mwandishi wenu Pascal Mayalla, ni miongoni mwa mawakili wapya 335 walioapishwa wiki iliyopita na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, hivyo hii ni makala ya shukrani kwa Jaji Mkuu na uongozi wote na wanyakazi wa Mhimili wa mahakama wakiwemo wa kitengo cha mawakili, Asanteni sana.

Safari yangu ya kutamani kuwa wakili ilianzia Mwanza mwaka 1976 nikiwa darasa la pili shule ya msingi ya Nyakahoja ambapo Baba yangu Mzee Andrew Mayalla (RIP) alikuwa mtumishi wa serikali tukiishi Isamilo ya Chini nyumba nne za serikali zimepangana baada ya nyumba yetu next ni RPC, next ni u DSO na OCD.

Baba Kuachishwa Kazi
Mara ghafla usiku mmoja tumekuja kusombwa mzobe mzobe mimi sina hili wala lile bila kujua kilichotokea, kutoka nje ya nyumba, kumbe kilichokuta, pia kimewakuta majirani zetu wote wanne tunaopakana nao, RPC, DSO, OCD, na wote ni mara tumerudishwa kijijini tena sisi japo ni Wasukuma wa Mwanza, wanaume wa Kisukuma wakipenda, ni wanapenda, wanakufa wanaoza na kuhamia kule alikopendea kwa kutelekeza kwao, na kuhamia huko alikopendea!. Babu mzaa Baba akikufa kwa mwanamke wa Kinyamwezi, akahama Mwanza jumla na kuhamia Tabora, akaoa Tabora, baba akazaliwa Tabora, akasoma Tabora na akaoa Tabora, hivyo a place of domicile aliyoandikisha kazini ni Tabora kikijiji cha Itonjanda. Hivyo ghafla tukarudishwa kijijini Itonjanda!.

Maisha ya Kijijini, Vijiji vya Ujamaa.
Enzi za Nyerere, Operation vijiji ilipoanza, ile 1975, ilikuta baba tayari ni boss kazini kwake na Baba yangu mdogo, Mzee Kasanga ni mfanyabiashara tajiri, hivyo waliisha mjengea mama yao (Bibi yangu) nyumba ya kisasa ya tofali, kigae, kupigwa chuppingi, rangi, sling board, wakati nyumba nyingi zilikuwa ni za udongo na nyasi.

Hivyo operation vijiji ilipoanza, ilikuta tayari nyumba nzuri ya kisasa ya block na kuezekwa kigae kijiji kizima ndio ilikuwa bonge la mjengo, hivyo kutakiwa kuvunja na kuhamia kijijini upande wa pili wa barabara, kwa wale wanaonijua mimi Pasco kuwa ni mbishi, mimi sio mbishi, kuna watu wabishi nchi hii walimbishia hadi Nyerere, hivyo wazee waligoma kuvunja nyumba, na kijiji kizima kilihamia upande wa pili wa barabara, hivyo nyumba yetu kubaki pekee yake upande huo.

Just imagine, mtoto unazaliwa, familia bora, unakuta baba na mama ni ma boss wa serikali, asubuhi ni mwendo wa chai ya maziwa, mkate na siagi kwa mayai ya kukaanga, baba anaendesha gari Volvo, mama Vockswagoon moja tuu ya kibanda wazi Mwanza nzima, mtoto unasoma English Medium Nyakahoja, mara ghafla mnahamishwa usiku usiku na kutupwa kijijini!, ndipo unagundua kuwa kuwa hata ile nyumba ya Isamilo sio nyumba yenu ni nyumba ya serikali!, kumbe yale magari ni magari ya serikali!, kumbe hadi fenicha za ndani, makochi, vitanda hadi magodoro vyote ni mali ya serikali commeworks!. Mnahama na masanduku tuu ya nguo zenu!.

Nikaandikishwa Shule ya Msingi ya Itonjanda. Enzi za maisha ya Mwanza, miongoni mwa vitu nilivyorithi kwa baba ni roho nzuri, kupenda starehe, na kupenda…, kula vizuri na kustarehe, soda, kuku na keki vilikuwa ni vyakula vya kawakaida enzi za Mwanza, sasa huku kijijini, soda na kuku ni mpaka siku ya sikukuu au wakija wageni, na kijijini sasa hakuna tena starehe!, Starehe pekee ilikuwa ni kusikiliza muziki wa santuri, sisi ndio pekee tulikuwa na muziki wa santuri kijiji kizima tena betri zikiisha unafanya kuzianika juani!.

Baba Kufuatwa Kuchukuliwa Kupelekwa Kusikojulikana!
Siku moja usiku, baba alifuatwa na watu wa kazini kwake, mimi nikidhani ni amesafiri, enzi hizo tukiishi na mama Mdogo, moja ya sifa ambazo sio nzuri niliyorithi kwa Baba, ni kupenda warembo, Mambo ya Wasukuma na wanawake wengi, yaliisha mshinda mama yangu kitambo, akasepa zake, hivyo mimi nimelelewa na wamama wadogo waliokuwa wanapishana. Wasukuma wanapenda watoto, tukiwa Mwanza, mimi ndie mtoto wa pekee niliye opt kubaki na baba, wakati ndugu zangu waliopt kuishi na mama.

Hivyo mimi nilikuwa ni mtoto best wa baba, hivyo trips za baba kwenda bar kunywa, nakwenda nae, usingizi ukinishika, napelekwa kulala kwenye gari, baba anapokuja tunarejea nyumbani, kutokana na ninayoyaona Dingi anaamini mimi ni mtoto mdogo sijui kinachoendelea, na kwenye gari anaamini nimelala, hivyo naona jinsi wamama wanavyopishana!. Lesson kwa wazazi, "don't underestimates uelewa wa watoto wadogo, mkawa mnafanya vitu vya ajabu ukijua mtoto ni mdogo haelewi!.

Nimelelewa na wamama wadogo watatu tofauti tofauti kila mmoja kwa wakati wake!, naomba tusiwaite mama wadogo kuwa ni mama wa kambo, kutokana na a bad connotation ya jina "mama wa kambo" kwasababu hawa wamama wadogo wangu, hawakuwahi kunitesa, and in fact walinipenda kuliko hata mama yangu mzazi!. Siku nikimtembelea mama, kule ndugu zangu wanafundishwa kufanya kazi za nyumbani, mimi nimewekewa mfanyakazi, mpaka darasa la pili, sifui chochote!, nyumbani sifanyi kazi yoyote, hata nikivua nguo, naiacha hapo chini, mtu wa kuiokota yupo.

In short niliishi kama a prince fulani, na sikuwahi kuchapwa na baba kwa kosa lolote, ila pia Baba alikuwa anajua kuchagua, maana hao mama zangu wadogo wote ilikuwa sio mchezo!. Hilo la kutochapa watoto na kujua kuchagua, pia nimelirithi!. Baada ya Mzee kuchukuliwa, Mama mdogo wa mwisho alirudi kwao, hivyo mimi kubaki na bibi, peke yetu!, mjumba wote ule!.

Development of Extra Sensory Powers
Tulipohamia kijijini, hatukuweza kuajiri mfanyakazi, hivyo ndio nikaanza kufundishwa kufanya kazi ndogo ndogo ikiwawemo kufua zile nguo zangu "zile", na soksi ila nguo za shule bado nilifuliwa na mama mdogo. Baba alianza kuwa mlevi, hivyo nilikuwa nikitumwa kuchukua pesa kutumwa dukani, nachukua na extra, bada hawawezi jua. One day nikatumwa kuchukua pesa mfukoni kwa baba, akasema angalia mfukoni kwangu kuna coin ya sent 50 (sungura), nikamnunulie sigara. Kule kwenye suruali, nikakuta kuna coins 2 za senti 50, nikakomba zote, nikaenda dukani kumnunulia sigara, na mimi nikanunua pipi, biskuti na maembe 10!.

Sikujua kuwa kumbe dingi aliisha note pesa zake zinayeyuka, hivyo this time was a trap!. Niliporudi nikampa sigara zake, akaniuliza kwenye mfuko kuna nini, nikasema hakuna kitu ni vitu vyangu, leta tuone!. Nikashangaa dingi hanaga time na vitu hivyo!. Nilipomuonyesha nikaulizwa umevipata wapi, nikajibu Chale ameninunulia!. Huyu Charles Lyochi, ni mtoto wa msaafu mingine, hivyo na wao ni maisha bora.

Mtu akatumwa amuite Chale, alipokuja akashangaa!. Kilichofuata ni kipigo!, hiyo ndio ikawa mara yangu ya kwanza kupigwa!. Siku hiyo nililia usiku kucha, nikamkumbuka mama, kwa mama ni maisha mazuri kuliko kwa baba. Katikati ya usiku na giza nene nikaona kama mwanga mweupe baadae ukapotea, sasa usiku gizani nikawa naona kama mchana!.

Macho yangu yalipata uwezo wa ajabu wa kusoma kwenye mwanga hafifu. Toka hapo siku za mbalamwezi, mimi nilikuwa nasoma vitabu vya hadithi usiku kucha, hivyo ku develop insomnia. Hivyo nimevisoma vitabu vyote vya Elfu Lela Ulela usiku kwa mwanga wa mbalamwezi.

Safari ya Kuhamia Dar es Salaam
Mara baada ya muda sii mrefu, baba yangu mdogo Mzee Mathew Kasanga, akanifuata kjijini Itonjanda, akanileta kwake Dar es Salaam, tena tulikuja kwa ndege ya kukodi, enzi hizo, ndege za kukodi ni ndege za jeshi tuu, ndege hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Captatain Sande, from there nikasema mnikiwa mkubwa, nataka kuwa pilot, kurusha ndege!. Hivyo mimi mwana jf mwezenu nilianza kukwea pipa at 8 years!.

Maisha Mapya Familia kwa Mzee Kasanga.
Wakati najiunga na familia ya Kasanga, mimi ndio nillikuwa mtoto mkubwa, dada yangu Maria yeye aliishatangulia kuchukuliwa akisoma sekondari ya Jangwani, hivyo kutokana na kulelewa na wamama wadogo, na siku zote wamama wa kambo wana sifa mbaya za kutesa watoto wa wenzao, hivyo ili kuepuka kuonekana wananitesa, nikajikuta mimi nimelelewa kwa kudekezwa!. Hivyo nimeingia nyumbani kwa Mzee Kasanga as a spoilt kid!. I’m who I’m today, credits ni kwa Mke wa Mzee Kasanga, mama wa Kiganda, Nora Katusabe Kasanga, kwa sababu kiukweli alininyorosha!. Thanks to this family!.

Dar tulikuwa tunaishi nyumba nzuri, eneo la Drive In Flats, nikajiunga shule ya Msingi ya Oyster Bay na kurejea kwenye maisha bora zaidi yay ale ya Mwanza, maana Mzee Kasanga kwenda ulaya ni kama kwenda Dodoma, enzi hizo za ile miezi 18 ya kukaza mikanda, sisi kuanzia sabuni, dawa za meno, nguo, viatu na raba vyote ni kutoka mamtoni.

Kipindi chote hiki, mpaka ninatua kwa Mzee Kasanga, sikuwahi kuelezwa rasmi baba alienda wapi, ni nini kilimtokea.Jee ni nini kilimtokea Mzee Mayalla, na kina uhusiano gani na uwakili wa Pasco Mayalla?. Tukutane Wiki Ijayo Kuendelea na simulizi hii ya ndoto ya uwakili ya Pasco Mayalla.

Paskali
 
Kumbe ulikuwa mtoto wa kota za polisi mnacheza kwenye tope na mabata ya kota! Bata wana chuki sana kwani wanaamini hawapendwi kama kuku, ila hawajui kuwa kupendwa kwa kuku ni kwa ajili ya kuchinjwa mgeni akija au sikukuu ya Iddi, sasa na Paskali naye akaiga chuki dhidi ya Chadema na wafuasi wake na kuamua awe wakili ili aje kusaidia kuwafunga kwa kuandaa na wenzake kesi za kugushi, ole wao wanachadema watakaoingia kwenye kumi na mbili zako.
I like your likes.
 
Katiba mpya itazuia kupotea ovyo KWA WATU hata Maafisa usalama wakigawanyika kimtazamo kuhusu vyama vya siasa na wagombea wao urais watalindwa na SHERIA mama ya katiba mpya ya nchi yetu!!!

Baba YAKO Sio wa kwanza kupotea KWA kuwa na mtizamo tofauti na utawala uliokuwepo na chama Tawala kilichoshika hatamu!!

Nakukumbusha RIP KOLIMBA,IMRAN KOMBE,Mwangosi Ben saanane na wengineo!!


"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!!
 
Katiba mpya itazuia kupotea ovyo KWA WATU hata Maafisa usalama wakigawanyika kimtazamo kuhusu vyama vya siasa na wagombea wao urais watalindwa na SHERIA mama ya katiba mpya ya nchi yetu!!!

Baba YAKO Sio wa kwanza kupotea KWA kuwa na mtizamo tofauti na utawala uliokuwepo na chama Tawala kilichoshika hatamu!!

Nakukumbusha RIP KOLIMBA,IMRAN KOMBE,Mwangosi Ben saanane na wengineo!!


"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!!
Noma sana!
 
Back
Top Bottom