Mbeya: Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali waachiwa kwa dhamana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,247
Kama tulivyosema tangu awali , Shetani hajawahi kumshinda Mungu , hatimaye watuhumiwa wote wako huru

Masharti ya Dhamana kwa Mdude na Mwabukusi haya hapa .

Screenshot_2023-08-18-17-37-27-1.jpg


====

UPDATES; 1800HRS

=====

Mdude Nyagali na Boniface Mwabukusi waachiwa kwa dhamana.

Watuhumiwa wa kesi ya uhaini wakili Boniface Mwakubukusi na Mdude Nyagali waliokuwa wakishiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya wameachiwa huru wakibadilishiwa mashtakana na kuwa kesi ya uchochezi.

Wakili Mwambukusi na Mdude wamechiwa majira ya saa 11:30 jioni huku wakiwashukuru watanzania pamoja na mashirika mbalimbali huku wakieleza kuwa watatoa msimamo wao baada ya kukutana na Balozi Dk Wilbroad Slaa.

Wakili Philip Mwakilima anayewatetea Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyagali amesema kutoka na dhamana hiyo kosa la uhaini halipo tena hivyo wateja wake wamedhamiwa kwa kosa la uchochezi

Mwabukusi hivi karibuni aliwawakilisha wadai wanne katika kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), akiwa kiongozi wa jopo la mawakili.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 ilifunguliwa na Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus dhidi ya Serikali.

Agosti 10, mwaka huu Mahakama ilitoa hukumu ya kuitupa kesi hiyo ikisema haina mashiko.

Baada ya kesi kutupiliwa mbali, Jeshi la Polisi lilionya wanaoandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025, likisema waandaaji wanayahusisha na kushawishi jumuiya ya Watanzania kuwaunga mkono katika hoja kuhusu Bandari.

Bila ya kutaja majina au kikundi cha watu, Mkuu wa jeshi hilo (IGP), Camillius Wambura akizungumza na waandishi wa habari alisema kuna taarifa zinasambaa katika mitandao ya kijamii inayohusu maandamano hayo.

Hata hivyo, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya kutoa hukumu katika kesi ya IGA, wakili Mwabukusi alitangaza uwepo wa maandamano.

Polisi: Tumemkamata Mwabukusi, Mdude kwa mahojiano

Jeshi la Polisi nchini lilithibitisha kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama Mdude kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP -David Misime ilisema wawili hao wamekatwa kwa mahojiano ambayo yanaendelea.

“Jeshi la Polisi kama lilivyo eleza jana tarehe 11 Agosti 2023 linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria.

“Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata maeneo ya Mikumi Mkoani Morogoro majira ya saa nane na nusu usiku tarehe 12 Agosti 2023,” ilisema taarifa hiyo.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofumgwa kati ya serikali na Dubai.


Kukamatwa kwa Mwabukusi kulikuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.
 
Kama tulivyosema tangu awali , Shetani hajawahi kumshinda Mungu , hatimaye watuhumiwa wote wako huru

Masharti ya Dhamana kwa Mdude na Mwabukusi haya hapa .

View attachment 2720869
Wananchi walikua wakiogopa kutamka neno Uhaini hadharani, ilikua hata wakilisikia neno lenyewe wanasisimka kwa uoga.

Wakaja Polisi na mikurupuko yao kutoka huko walipokuwa, wakalirahisisha sana kosa la Uhaini, wameli polish, wamelipaka rangi nzuri za kupendeza. Sasa hivi wananchi hawaliogopi tena, wametokea kulipenda, na sasa hivi wanatamani kushiriki uhaini na wapo tayari kuushiriki uhaini wakati wowote ule.

Sasa Kingai amejithibitisha kuwa yeye ndiye Mtunzi Mkuu wa haya matukio ma hozi hadithi ndani ya hii nchi.
Big up sana kwa CDF kwa wito wake kwa Wanajeshi kutojih7sisha na siasa, akishaona mizinguo.
Salute kwa CDF na Jeshi letu Tukufu.
 
Back
Top Bottom