RPC Morogoro: Sina taarifa ya kukamatwa kwa Wakili Mwabukusi, Mdude na Masonga

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
IMG_8232.jpeg


Kufuatia habari zilizoripotiwa katika mitandao ya kijamii kuhusu kushikiliwa kwa katibu wa CHADEMA kanda ya kati Emmanuel Masonga, Wakili Boniface Mwabukusi na na kada maarufu wa CHADEMA Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA) maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa jeshi la polisi kwa maelekezo ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo Alex Mkama amesema, hana taarifa za kushikiliwa kwa katibu huyo na wenzake wawili.

Akiongea na Mwandishi wa Jambo TV kutoka mkoani Morogoro RPC Mkama ameeleza kuwa, wanaotoa taarifa hizo hawana uhakika nazo.

Katika mitandao ya kijamii mapema asubuhi ya leo zilisambaa kwa kasi taarifa za watatu hao kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa jeshi la polisi maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro hali iliyopelekea kuzua taharuki kwa wananchi wengi.

Pia soma: Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom