Wakili Msomi Peter Kibatala alivyomkaanga mtoto wa IGP Mahita kwenye kesi ya Mbowe

Lakini ni kwa bahati mbaya sana "kujua sheria" Tanzania, kwenye enzi tulipotoka (enzi za Magufuli), ilikuwa haisaidii chochote. Labda sasa tutaanza kuona maana na uzuri wa kujua sheria kama hali itaendelea kuwa hivi ; yaani mahakama ionekane kufanya kazi bila ya kuingiliwa na yeyote.
Haswaaa!!!,Tutakuwa tumekomaa sasa.
 
Ivi kibatala ana ulinzi kweli? Maana sio kwa za uzo anazo ipiga sirikale hii mara kwa mara jamaa huwa anawa nyoosha sana
Ni kweli kabisa, walicho bakiza ni kumwinda na kumtungua vilevile kama kwa Lissu. Watz tusichoke kumfanyia maombi ulinzi kwa Mungu
 
Wanaumbukaje sasa yani kama mitoto. MBOWE UTATOKA SALAMA MCHANA KWEUPE. MUNGU YUPO
 
Kuna udhalikishaji gani hapo?
Hayo ni matunda ya kudesa....
Maswali ya Kibatala yamenyooka kama rula.
Ukiangalia kwa mbali uta gundua hawa polisi walikuwa na kiburi cha mwenda zake.
Hakuna udhalilishaji wowote bali wakili wa Serikali ni mbumbumbu tu ni wakili kilaza
 
Unajua kesi inayoendelea inahusu nini? Kumbuka wako kwenye kesi ndogo ya ukamataji na kuwatesa watuhumiwa. Je kukiuka taratibu za ukamataji hapa haiwapi watuhumiwa nafuu?
Kwanza walikaa vutuoni zaidi ya saa 48 pasipo kuwafikisha mahakamani, Polisiccm wanaenda kuumbuka waache kutumika na CCM kuwabambikia kesi wapinzani
 
Wanaumbukaje sasa yani kama mitoto. MBOWE UTATOKA SALAMA MCHANA KWEUPE. MUNGU YUPO
Wamezoea kuwabambikia kesi watu wasio na msaada wa mawakili thabiti lakini sasa wanaumbuka kwa ushetani wao
 
Wakili wa Serikali inaelekea hajui kitu ni mbumbumbu
Wapo smart na wanajielewa, tatizo ni kesi wanayoiendesha. Na ukumbuke maandalizi ya mwanzo tangu arrest, investigation na interrogation imefanywa na watu wasiojua wanachofanya. Hata Kibatala angekuwa prosecutor lazima angeonekana hajui.
 
Mwisho wa ubaya ni aibu.

Hilo ndilo tatizo kubwa la kesi za kubambika, Polisi hakumbuki tena kuwa yeye ni mtumishi wa Umma, ambapo anatakiwa afanye kazi kwa kufuata sheria na kanuni.

Katika kesi ya Mbowe, mapolisi hata hizo Police General Orders zao hawakutaka kuzifuata
Hawawezi kuzifuata kwasababu wanajua wanafanya ubatili. PGO nadhani zinakuwa zimenyooka, kwahiyo wakizifuata watashindwa kutekeleza maagizo kutoka juu. Wanaamua kupuyanga tu.
 
Back
Top Bottom